TAHURI: Tumuunge mkono Rais Magufuli katika vita dhidi ya Corona

TAHURI: Tumuunge mkono Rais Magufuli katika vita dhidi ya Corona

Bollen Ngetti na wenzako msimamo wangu ni MAISHA YANGU NI JUKUMU LANGU, hakuna wa kunifanyia kampeni za kisiasa kuhusu ulinzi wa afya yangu.
Tanzania kushindana na World
Health Organization (WHO) hakuna tija kwani sisi pia ni mwanachama na tulikubali masharti, Tanzania inategemea chanjo nyingi za watoto, kuzikataa wakati hatuna uwezo wa kuzitengeneza ni kujichimbia kaburi.
Nikipata Korona Bollen na wenzako hamtakuwa pembeni ya kitanda changu kuniuguza wala kuilisha familia yangu.
Ngeti kaamua kujitoa fahamu zote akisaka uteuzi kwa njia haramu za kishetani
 
Achani kujifanya mnatupenda na kutusemea kila kitu kwa ujinga wenu wa kufikiri mnayajua sana mahitaji yetu. Acha mimi nichanjwe hata kwa hela yangu.
CCM hawakuwa na huruma kwenye uchaguzi waliwapora wapiga kura haki za kuchagua wakajisimika ubunge udiwani kujipeleka ikulu kienyeji kwa kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu bila Aibu, cha ajabu sasa wanajidai kuwa na huruma juu ya Chanjo wakati pesa za corona wamezitafuna kifisadi hakuna ajuae zilipotelea wapi
 
Malawi NI Malawi na Tanzania ni Tanzania.
Nakukumbisha tu hizo ni nchi mbili tofauti
Hata Tanzania nayo corona inaua sana lakini CCM wanaficha takwimu taarifa ili watanzania waambukizane wafe kwa wingi baada wachukue pesa nyingi tokea WHO kimya kimya wazipige kama walivyofanya awali
 
Kama bwana wao anadhani kila gonjwa linaweza kuwa na chanjo unadhani wao akili zao zitakuwa tofauti? Kwangu mimi ukiniambia Magufuli alifika kidato cha sita nitakataa katu katu. Kuna namna iliyofanyika. Upeo wa form six hauwezi kuwa mdogo namna hiyo.
Kwa sasa CCM yote hawafikiri kwa Akili zao binafsi mpigie Sele 0787132277 yupo huko Dsm kwa mliopo Dsm atakupa jibu kuwa sasa ni zidumu fikra zisizo sahihi za mtukufu mwenyekiti wa CCM tu hakuna zaidi, Sele ni mmojawapo wa washauri wakuu wa CCM makao makuu na pia ni mwakalishi na Rais mambo ya jamii mpigieni simu awape michakato yote
 
Taasisi ya Haki za Binadamu, Tanzania Human Rights-Foundation (TAHURI) imetoa tamko la kuwataka Watanzania kuungana pamoja katika vita dhidi ya Shirika la Afya Duniani, WHO na Rais Magufuli huku likiwataka wananchi kumuunga mkono Rais wao.

Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Bollen Ngetti amesema;

"Tunaweza kutofautiana katika mambo mengi ya kiitikadi, kimtazamo na maono lakini katika mambo ya msingi kwa nchi kama hili la chanjo ni sharti tuungane kuwa kitu kimoja".

Aidha, Ngetti ambaye ni mwandishi wa habari nchini amesema Watanzania wasikimbilie tu athari za kiafya kwa chanjo hiyo na badala yake waangalie athari za kiuchumi.

"Tutambue kuwa dunia iko katika vitu kubwa ya kiuchumi. Kama Tahuri hatutajikita sana katika athari za kiafya za chanjo hiyo lakini tufikirie ni fedha kiasi gani chanjo hiyo itaswaga?"

"Ikumbukwe kwamba, kwa mujibu wa WHO ili nchi za ki-Afrika kupata chanjo kutoka makampuni yaliyojiorodhesha kwenye mkataba wa COVAX ambayo ni BioNTech na Moderna itazigharimu kiasi cha Dola za Marekani kati ya 7-11 kwa chanjo moja".

Ngetti ameendelea kusema, "kwa Tanzania pekee kama Rais Magufuli ataruhusu chanjo itatugharimu Tsh104Trilioni kwa idadi ya watu wetu nchi nzima. Hii ni fedha nyingi sana kwa nchi changa kama sisi".

Ngetti amefafanua kuwa fedha hizo zitatakiwa kukopwa kutoka Benki ya Dunia kwa udhamini wa ADB na itachukua miaka zaidi ya kumi kuzirejesha kwa riba ya asilimia 7.2.

Aidha, Ngetti amehoji, "kama nia njema kwa nini wazungu wamekimbilia kutafuta chanjo badala ya tiba kamili? Walijua kwa tiba utahitaji dozi chache sawa na idadi ya walioambukizwa ambao kwa sasa ni milioni 100 lakini kinga utacheza namba ya watu duniani".

"Jambo la pekee kama Taifa tunalotakiwa kufanya ni kufuata masharti ya kujikinga huku tulifanya kazi kwa bidii, huu ni upepo unaovuma na kupita, tusiondoshwe kwenye reli".

Ngetti amemaliza kwa kusema, "Magufuli si kichaa, wala hana historia ya ukichaa, anatutakia mema tusimvunje moyo. Lakini pia wataalamu wetu nao wakeshe maabara kukuna vichwa aidha kuchunguza chanjo hizo au kugundua za kwetu kama Waganda wanavyofanya"

My Take: Kwa vita hii tutashuhudia na kusikia mengi. Vita hii ya Magu na wanasayansi itaibua makubwa. Subiri tuone!
etu haki ya binadamu, kachukueni yakwenu mjichome,
 
Propaganda!

Hoja ya JIWE kuwa tusikubali mambo kichwa kichwa mradi yametoka kwa wazungu ni ya msingi. Hawa wanasayansi wetu wanatakiwa wawe msaada wakati huu kama sio kutafiti juu ya chanjo wajitahidi kuangalia kama hizo chanjo zinaweza kuwa na madhara gani kwetu!! Hakuna taasisi yenye moral authority kutulazimisha juu ya chanjo ambayo hatuna uhakika nayo.

Ni kweli nchi yetu ukiifananisha na majirani zetu hatukupoteza watu wengi huko nyuma [ maybe because of HERD IMMUNITY!}; tuangale kama zile hatua za NYUNGU na kuvaa barakoa na social distancing zilikuwa na msaada kuweza kuepuka vifo vingi!

Wale mataga wnaojipendekeza waache kabisa tabia ya kuwadanganya watu kuwa corona haipo nchini bali wawahimize watu kulinda maisha yao kama wanasayansi wanavyotuhimiza; tabia ya kuwanyanyapaa wanao vaa barakoa ni lazima ikemewe na viongozi wa nchi. Hizi chanjo mpaka sasa hakuna mtu mwenye uhakika nazo kuhusu umahili wake wa kuzuia hivyo sio vibaya tukawa na subira wakati tunajihakikishia kuwa uamuzi tutakaofanya juu ya chanjo utakuwa na faida za muda mrefu kwa nchi!

Swali la kizushi " KWANINI BILL GATES; MFADHILI MKUBWA WA HIZI CHANJO , YEYE NA FAMILIA YAKE HAWAJAONESHWA WAKIPATA HIZO CHANJO?"
 
Bourgeoisies wamekusudia kuodhoofisha Afrika na nchi maskini kwa gharama yoyote. Tuwe makini sana na hao jamaa maana hawana utu wala uhisani wa kweli wala urafiki. Oooooohoooo!
 
Hapo ndipo mtaona umuhimu wa kuweka budget kwenye mambo ya maana na sio kuspend pesa kwenye vitu ambavyo ulazima ni 50 percent haya yasingetukuta.
Afya pamoja na ulinzi.

Kama tungekuwa na chanjo yetu wenyewe yenye viwango na high quality tanzania then tunaisambaza africa nzima basi tungekuwa powerful in africa in 3 month.
Fedha siyo lazima iwe ilikuwa budgeted, inakopwa WB -- tatizo unairudisha at your own costs
 
Taasisi ya Haki za Binadamu, Tanzania Human Rights-Foundation (TAHURI) imetoa tamko la kuwataka Watanzania kuungana pamoja katika vita dhidi ya Shirika la Afya Duniani, WHO na Rais Magufuli huku likiwataka wananchi kumuunga mkono Rais wao.

Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Bollen Ngetti amesema;

"Tunaweza kutofautiana katika mambo mengi ya kiitikadi, kimtazamo na maono lakini katika mambo ya msingi kwa nchi kama hili la chanjo ni sharti tuungane kuwa kitu kimoja".

Aidha, Ngetti ambaye ni mwandishi wa habari nchini amesema Watanzania wasikimbilie tu athari za kiafya kwa chanjo hiyo na badala yake waangalie athari za kiuchumi.

"Tutambue kuwa dunia iko katika vitu kubwa ya kiuchumi. Kama Tahuri hatutajikita sana katika athari za kiafya za chanjo hiyo lakini tufikirie ni fedha kiasi gani chanjo hiyo itaswaga?"

"Ikumbukwe kwamba, kwa mujibu wa WHO ili nchi za ki-Afrika kupata chanjo kutoka makampuni yaliyojiorodhesha kwenye mkataba wa COVAX ambayo ni BioNTech na Moderna itazigharimu kiasi cha Dola za Marekani kati ya 7-11 kwa chanjo moja".

Ngetti ameendelea kusema, "kwa Tanzania pekee kama Rais Magufuli ataruhusu chanjo itatugharimu Tsh104Trilioni kwa idadi ya watu wetu nchi nzima. Hii ni fedha nyingi sana kwa nchi changa kama sisi".

Ngetti amefafanua kuwa fedha hizo zitatakiwa kukopwa kutoka Benki ya Dunia kwa udhamini wa ADB na itachukua miaka zaidi ya kumi kuzirejesha kwa riba ya asilimia 7.2.

Aidha, Ngetti amehoji, "kama nia njema kwa nini wazungu wamekimbilia kutafuta chanjo badala ya tiba kamili? Walijua kwa tiba utahitaji dozi chache sawa na idadi ya walioambukizwa ambao kwa sasa ni milioni 100 lakini kinga utacheza namba ya watu duniani".

"Jambo la pekee kama Taifa tunalotakiwa kufanya ni kufuata masharti ya kujikinga huku tulifanya kazi kwa bidii, huu ni upepo unaovuma na kupita, tusiondoshwe kwenye reli".

Ngetti amemaliza kwa kusema, "Magufuli si kichaa, wala hana historia ya ukichaa, anatutakia mema tusimvunje moyo. Lakini pia wataalamu wetu nao wakeshe maabara kukuna vichwa aidha kuchunguza chanjo hizo au kugundua za kwetu kama Waganda wanavyofanya"

Mmeanza kuchungulia chungulia kama mtoke mashimoni mapanya buku nyie? Kumbe hakuna hela, yote ilikwenda cash kwenye midege midege?

Kumbe hata ya kuwa chanjo haifai, kina Bill Gates wanataka kutufuta duniani ni kisebu sebu na kiroho papo na sizitaki mbichi hizi?

Acheni upotoshaji wa wazi huu. Kwani chanjo ni lazima kwa watu wote kwa sasa? Si ni kwa makundi yaliyo hatarini zaidi tu kwanza na hata huko walikoendelea ndivyo wanavyofanya?

Nia yenu ya kututelekezea hili janga kwani hata inajificha? Hatudanganyiki!
 
Porojo, ulongo, hearsay, uzandiki, uzushi nk, vyote vimerundikwa pamoja na kutunga story isiyo na kichwa wala miguu, hatimaye ikawa thread hapa JF. Ama kweli, jf is the home of great jingas
 
Wanaokufa wanazikwa wapi?.
tutaanza lini kuzagaa Kama maiti za kuku mitaani?
Hata Tanzania nayo corona inaua sana lakini CCM wanaficha takwimu taarifa ili watanzania waambukizane wafe kwa wingi baada wachukue pesa nyingi tokea WHO kimya kimya wazipige kama walivyofanya awali
 
Tumuunge mkono mtu ambaye alituma ndege ikachukue dawa kule magangaska halafu wakaishia kuinywa yeye na wapendwa wake ??
 
Ngeti amefika bei
Kama huamini chanjo hiyo kwa nini usigundue yenu
Chanjo zote wanazopewa watoto wetu unadhani zinatengenezwa Chato?
 
Back
Top Bottom