Polepole kujiuzuru:
➡Sababu alizozitoa sio za kidiplomasia, ni za hali ya kisiasa na utawala wa ndani ya nchi...
➡Tukio hili la kujiuzulu balozi ni la pili sasa. La kwanza ni miaka ya 1960s ambapo Christopher Kassanga akiwa balozi kule Uingereza, alitofautiana na Rais Hayati Mwl Julius K. Nyerere miezi mitatu baada ya uteuzi wake na hivyo akaona hataweza kufanya kazi naye, hivyo akabwaga manyanga...
➡ Aidha Ili kulinda taswira ya nchi, kulitokea tukio jingine linalofanana na hili miaka ya 1980s. Hayati Rais J. K. Nyerere walitofautiana na Waziri wake wa fedha wakati huo Edwin Mtei (Baba mkwe wa Freeman Mbowe) juu ya kukubaliana au kukataa masharti ya na sera za IMF na WB juu ya kuipatia Tanzania mkopo wa fedha ili kuimarisha uchumi wake mara baada ya kutoka ktk vita vya Tanzania na Uganda maarufu kama vita vya Kagera 1978/79...
➡Nyerere hakukubaliana na masharti ya WB na IMF kupunguza thamani ya shilingi ili Tanzania ikopesheke. Waziri wake Edwin Mtei, alikubaliana na sharti hilo. Kwa tofauti hizo, ikaonekana kuwa Waziri hawezi kufanya kazi pamoja na boss (Rais) wanayetofautiana naye...
➡Ili kulinda taswira (image) ya Rais na nchi, ilibidi Edwin Mtei ajiuzulu uwaziri na sbb zilizotolewa ni za kiafya lakinI ukweli ulijulikana baadaye sana kuwa sababu haikuwa hiyo bali ni kutofautiana kisera na boss wake Rais Nyerere..
➡Hili la Humphrey Polepole ni jiwe la kushitukiza. Sio la kawaida na linaharibu taswira si tu ya Rais Samia bali ya nchi kwa jumla ktk diplomasia ya kimataifa. Hakuna crisis management ndani ya serikali ya Rais Samia. Ni mwendo wa kuviziana tu na kupigana marungu...
➡Haya marungu lazima yawafurushe baadhi toka kwenye nafasi zao. Bila shaka unabii wa mtumishi wa Mungu Steven Jacob Gumbo toka Arusha juu ya kijana huyu Humphrey Polepole👇🏻👇🏻 unaenda kutimia. Labda ndiye PM au Minister For Foreign Affairs ajaye huyu chini ya Rais Josephat Mathias Gwajima au Tundu Lissu