Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Wote waliofanya sikukuu na kushangilia kwa mbwembwe kifo cha JPM wataishuhudia 'KARMA' ikifanya kazi yake bila shuruti au kushawishiwa na ama nguvu ya asili ama nguvu ya binadamu. Kifo cha JPM kiliwaumiza sana Watanzania wa hali za kawaida ambao ndio wengi lakini wenye fedha, wafanyabiashara wasio waadilifu na wanasiasa maslahi iwalifurahi wakifikiri wanauwezo wa kuhodhi hewa na mwanga wa jua; Mungu aliye hai anamhesabu mwema na muovu kuwa wote ni sawa na bila kumkiri kwa kinywa na matendo kwamba yeye ndiye Mungu na ukabadilika ni ubatili mtupu pamoja na wema wako.Kama viongozi wa Taifa hili hawatosimama leo na kukemea kwa dhati kabisa kuhusu Siasa za chuki zinazoendelea ndani ya CCM yangu basi gharama ya kuweza kuthibiti hali kuelekea mwaka 2025 zinaweza zikawa kubwa!Vihatarishi hivi vya amani vinapaswa kukemewa na viongozi wa Siasa,viongozi wa dini na hata viongozi wa kimila Nchi nzima!
Niliwahi kuandika kuwa kama Chama changu CCM hakitakuwa tayari kukabili Siasa hizi za chuki ndani ya Chama,hakika tunaweza tukawa tunajichimbia shimo kubwa kwa Siasa za baadae!Gharama za kutubu makosa ni ndogo sana kuliko gharama za kuja kupambana na chuki hizi za wazi ambazo zinaendelea kuota mizizi wazi wazi!
Tulifanya makosa makubwa sana kuruhusu personality kuwa above Institution matokeo yake ndio haya!Nadhani ili liwe somo kwa Siasa zetu.
Napenda kuwa bold kabisa na kuwataka vijana wa kitanzania kuachana na siasa za chuki ndani ya Chama chetu!Mpasuko ambao tunautengeneza leo unahatarisha sana safari yetu ya kushika dola!
Wote kwa Mungu tutarejea!Tuwaombee waliotangulia bila kudhihaki wala kuwanenea mabaya!
Kwaheri Mzee wangu Bernard Kamilus Membe,Kachero bora wa enzi zote katika Ulinzi na Diplomasia ya Taifa!
Kwake,wote tutarejea!
+255746726484.
Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Viongizi walioshiriki kumdhalilisha JPM wajitokeze na kutubu hadharani maana Mungu sio fedha, sio madaraka, sio kisomo na sio familia tajiri yenye kujivuna na kiburi. Mapigo yataendelea hadi mwasisi wake afikiwe. Jifunzeni namna anavyoishi Mzee Mwinyi ni mstaarabu na mfano wa kuigwa na viongozi wengine wa kisiasa. Hana majivuno anamheshimu mdogo na anasamehe hata anapotendwa vibaya ndio maana Mungu amemruhusu kujionea waliomfuata kiuongozi wanaendaje kwa manufaa ya wananchi.