Hivyo ndivyo ilivyo kwa taifa lolote ambalo litatoa uhai wa kiongozi wake ambaye anakuwa madarakani ili kulinda na kutetea mali za umma na maslahi ya taifa lake.
Angalia laana iliyoikumba Congo Drc mpaka leo laana hiyo inawaandama. Baada ya kumuua Lumumba, Mobutu na genge lake waligeuka mafidadi na walafi wa kutafuna mali za umma. Taifa lao pamoja na utajiri wa mali asili lakini lina umaskini mkubwa. Vita vya wenyewe kwa wenyewe visivyokwisha na matatizo lukuki.
Hui ni mfano tu wa namna damu ya kiongozi wa taifa ambaye ni mzalendo anapouwawa na kisha laana kulikumba taifa.
Watanzania tujitafakari sana.