Taja jina la shule ya msingi uliyosoma enzi hizoo

Sindanii atakua alikufundisha kupika Mangararumo. Baada ya Ramadhani hebu upike basi halafu unialike nije nionjeπŸ€ͺπŸ€ͺπŸ€ͺ

Kama ulibeba fagio na kidumu cha maji basi tutakua tunaongea lugha moja. Wakati huo wanafunzi wanashindana kutunza bustani za maua. Wayajua mauwa saa sita Shadeeya ?
 
Huo ni uchokozi ujue Shadeeya. Yaani unataka unitoe kwenye Ukayumba unipeleke ushuani mtoto wa mkulima na mkwezi mieπŸ€ͺπŸ˜‚
Mbona hufananii sasa?

Mi ntakuwekaga tu huko ushuani. Potelea pwete. πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 
Lugoda Primary 1 - 3, nikahamia Uhuru Mchanganyiko 3-4 Nikahamia Uzuri primary 4-5 nikamalizia mugabe 5 - 6
 
Mbona hufananii sasa?

Mi ntakuwekaga tu huko ushuani. Potelea pwete. πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
Mamii wa ushuani hawajui kucheza kombolela, hawajui kupinga "ganda ganduka", hawajui kucheza "hakiombeki", hawajui kucheza mpira wa makaratasi(chandimu), hawajui kuruka kamba, hawajui kupinga "msingi bong'oa" hawajui kidali poo kalale nacho, hawajui "kula mbakishie baba", hawaju mchezo wowote. Washazoewea kucheza tennis, golf, swimming na game

Kwanza nikuulize Shadeeya waeza kuta wewe wakishua kabisaa unatuchemsha tu hapa. Ushawahi kucheza ready(nage), dama(lile la kuchora chini na kuruka na mguu mmoja), umeshacheza mdako? Kama hukuwahi kucheza wewe ni wa kishua tuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hiyo Paragraph ya kwanza imefanya nimebakia nacheka mwenyewe tu hapa. 🀣🀣🀣

Hamna mie nimecheza sana hiyo sijui rede tena Arusha miaka hiyo kulikuwa na rede inaitwa mateka. Na hiyo Dama sisi tulikuwa tunaita esta esta.

Huo mdako ndo usiseme kabisaa. πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Kama umecheza hayo basi wewe kweli Kayumba mwenzanguπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…