Taja kipaji chochote unachokiona kwa mwana JF mwenzako

Nashukuru kwa jicho lako.

Karibu kwa mwali apate mafunzo shatashata shurti baada ya hekaheka za maisha ukaliwazwa na wako mwanadani hata usingizi ukaja ukiwa unatabasamu.

Dunia ni yetu, Mapendo ni yetu, Mahaba ni kwa wateule....🤪🤪.
Kwahiyo siku hizi unajiamulia tu bila kuomba ruhusa ya babu wa Butiama?
 
Hujawahi Kunikubali hapa Jamiiforums hivyo ningeshangaa sana kama katika huu Uzi ungenipongeza.
Mimi sikukubali ila unapowatandika mautopolo unageuka kuwa mkombozi wangu wa mbinguni na duniani. Mitano tena kwa my fellow tablet
 
Ahahaha tatizo lako babu hutaweza mibinjuko hata nikikupea ?
Kajamaa wala hakana tabu hata ukipeana maana huondoki nayo
Nimekuelewa na tayari niko inbox nasubiria PM yako. Mambo ya mbinjuko tutayajua mbele ya safari
 
ROBERT HERIEL FaizaFoxy GENTAMYCINE hapo hakuna mwenye kipaji.

Ni design ya watu wanaokuforce uamini wale wao wanachoamini.

Hakuna mtu anaeshindwa kuandika chochote humu JF

Sema tu hao watatu wana muda mwingi wa kuandika utumbo na mazaga zaga na kufanya watu wenye dull minds waburudike.

😂😂😂
Naamini hata mkeo angekuwa humu jamvini asingekutaja Kwa lolote.
Umeambiwa utaje watu wenye vipaji alafu Kwa akili yako ndogo ya nzi unataja wasio na vipaji. Nani alikuuliza?

Kwa nini usianzishe Uzi wa watu wasio na vipaji humu jamvini alafu ukawataja, lakini ulichokifanya hapa ni Akili ndogo ambayo kama ni mtihani umejibu OP.
 
Na mimi nifagilie kwa kimombo basi Paula. Mi nshachoka kufagiliwa kienyeji
In all seriousness though, you are extremely funny.
Being able to bring pleasure and happiness to those around you is a great skill to have. You can make people laugh and It's impossible not to like you.

Thank you, Asprin.
 
Hapa jukwaani pamesheheni vijapi vya kila aina na vya kila namna. Kuna vipaji hai na vipo mfu.
Kuna vipaji ambavyo vinatuburudisha, na vipo vipaji vinatuelimisha. Kuna vipaji vinatuonya na kutuadilisha, na pia kuna vipaji vinavyoyaelezea vyema maisha yetu ya usoni ambayo hayujayaishi bado nanhatujayafikia.
Huu ni uzi wa kutambua jambo kwa ufupi tu, vipaji tunavyovionesha kupitia maandishi yetu. Karibu na wewe utie nyama kwenye uzi huu. Asanye.

  • Mshana Jr ni visionary, ndiye nabii wa jamvi letu. Jicho lake kali linaona miaka kumi elfu nyuma, na miaka mia elfu ijayo. Iwe kwenye siasa, uchumi, utamaduni, matibabu, elimu ya mzungu na elimu ya rohoni amesheni uoni angavu usio na mawaa yoyote.
  • Bill Lugano, huyu ni jamaa mmoja mweledi sana. Nasema mweledi sababu nimekaa naye na ni mtu wangu wa karibu sana. Kijana mpole, mtaratibu, mcheshi, muungwana na ana elimu ya juu sana. Jamaa ana kipaji kikubwa sana cha kusimulia jinsi gani baba yake anavyokasirishwa na Laissez-faire, tabia aliyo nayo kijana wake.
  • Pia anaelezea utajiri wake kwa tambo za kipekee huku akituvunja mbavu kwa bichekesho na akituhurumia. Jamaa ni mwandishi mzuri sana wa riwaya na tenzi za Kingereza (poems) wengi hukasirishwa na aina yake ya uandishi kupitia characters wake Kidukulilo na Bill Lugano.
  • Pascal Mayalla, huyu ni Nabii mzee. Jamaa ameandika makala nyingi sana zenye maslahi kwa taifa, jamaa ni mwandishi mbobezi, aliyepitia misukosuko mingi ikiwemo kuhojiwa na kamati ya maadili ya bunge. Paskali, pia ni mwanasheria na ni kichwa kwelikweli, kwani katika wanafunzi 633, yeye ni miongoni mwa wanafunzi 26 tu waliofaulu.
  • UMUGHAKA, huyu jamaa ni bonge ya story teller, aina yake ya usimuliaji umejaa msisimko usio elezeka, muda wote unatamani kusoma maandishi yake huku ukitokwa na vipele vya msisimko. Maandishi yake yanayosha kabisa kumfanya mama aende nayo Ulaya akatuletea msaada wa matrilioni usio na.masharti yoyote.
  • GENTAMYCINE, huyu jamaa ni wa kipekee. Ndiye anayeongoza kwa kufahamika na mods wote na members wote hapa jukwaani. Jamaa ana akili za kurithi ambazo pia ameziongezea na elimu ya darasani na ya mtaani. Huyu akitoa ushauri hapa jukwaani, wizara zinaufanyia kazi ushauri wake, je ni nani mwingine kama yeye?
  • DeepPond , ukiyataka masimulizi ya mahaba hapa ndio mahali pake. Hii mashine haina mfanowe kwenye hiyo sekta aisee, simulizi zake lazima zikuache mdomo wazi. Hebu fikiria, mchepuko wa rafiki yako umemtia rumande mke wa rafiki yako, unafanyeje hapo?
  • FaizaFoxy , huyu mtu mmoja anaweza kufanya ligi na watu laki moja na akawaburuza. Sio uwongo, FaizaFoxy ni kichwa balaa, mpeleke kwenye dini, siasa, sayansi na teknolojia, kote yuko vizuri sana, hapendi ujinga, wee hata ukosee herufi moja tu, kwa jicho la tai ataona makosa yako.
  • ROBERT HERIEL, mwalimu wa walimu, kuhani mweusi. Atakufundisha kama mwalimu na kukuadilisha kama kasisi. Kupitia makala zake tumekuwa tukiyaona mapungufu yetu, na tulipoweza kujikosoa tukajikosoa, tulipowe kujisamehe tukajisamehe na tulipoweza kujirekebisha tukajirekebisha.
  • Kasie, hili toto chotara la Kimanyema na Kinyamwezi limebarikiwa maneno matamu, akili za darasani na za kitandani. Je una matatizo ya kimahusiano? Maneno yake matatu tu hayatakufariji kabisa, bali yataleta suluhusho la kudumu kwenye mahusiano yako. Je biashara yako haiendi vizuri? Kila unachokishika kinapotea? Umeenda kwa waganga wa kila aina na kwa Mwamposa lakini hujapata jibu? Hebu mcheki Kasie, hutojuta. Je una hela nanhuvijui viwanja classic vyenye watoto wakali na decent? Basi yeye ndio Google Map yetu.
Mshana Jr mzee wa matambiko huyo.
 
@mkwepu jr bila like ya huyu jamaa katika Uzi wako wowote ule basi,nyuzi zako ni batili..ana kipaji cha kusambaza upendo kwa ku like..

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom