Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

Pure Maasai tradition.
 
Siku moja nikiwa Musoma kulikuwa na mbwa kagongwa na gari barabarani. Basi kila mtu anayepita naona anang'oa majani na kumtupia yule mbwa. Nimeunganisha nukta wewe unatokea wapi mkuu πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Kwetu ni mwiko kumla mbilikimo! Ama albino!!!..... Na vingine vya kufanana na hivyo(aliejichubua/ama emolo!) Kama wewe ni wa hivyo ... kwangu Pita hivi!.... Ama Tafuta ....utampata ...wa kufanana nawe!!!
 
Yani katika tabia ninayo ichukia ndio hii sasa
 
Ni kabila gani?
 
 
Asante kwa nyongeza mkuu. Ila hizo namba 1, 4 na 5 zimenitisha. Na ikitokea mmiliki wa miwa au mahindi akakukuta kwenye shamba lake inakuaje? Anakupongeza au anakuchukulia hatua? Je, akikuchukulia hatua yeye atapata madhira gani?

Na hilo la kumvuka mtu naona lipo kariba kwenye makabila yote aisee!
 
Vingine na onyo tu hakuna laana wala mfano

huruhusiwi kukalia mafiga utaota majipu, kumbe saikolojia tu usiangukie kwenye moto au kuunguzwa na mafiga.

usikalie kinu, kumbe unawezama kwenye kinu ukabanwa uko.

usisimame mlangoni mizimu wakija watakuchukua, kumbe kuepusha msongamano.

usikate mti ovyo ni.mbaya, utunzaji wa mazingira.

Mtu kama amekukusoea akishika jani la isale akikuomba msamaha msamehe, kumbe kuepusha kesi za mda mrefu wakati mwingine ni ujinga unaweza tia katoto ka mtu dudu alafu unaomba yanaisha.
 
ukichinja mbuzi mwaga damu kidogo chini ili mizimu ya mababu nayo ishiriki

hurusiwi kuchinja mbuzi saa sita kamili mchana hadi ipite
 
huruhusiwi kuona uchi wa mzazi wako awe wa kiume au kike ni laana na unapofuka macho. Nashangaa kanda ya ziwa unaoga na dingi yako au maza ako
Kanda ya Ziwa ni kweli wanaoga sana na hakuna shida mkuu. Wala hakuna anayejali.
 
Kwetu mtoto wa kiume hatakiwi aungue kwa moto wa jikoni, akiungua hapati mwanamke 🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…