Taja mwiko, mila au desturi za kabila lenu au mahali ulipokulia

Desturi ya nyumbani kwetu ukisonga ugali ukimaliza mwiko lazima uuoshe. Marufuku kuacha mwiko mchafu. Hata sijui ina maana gani ila nimekua nayo mpaka leo nikimaliza kusonga ugali lazima nioshe mwiko kabla hata chakula hakijafika mezani.
Nadhani hii inasidia kuimarisha suala la usafi mkuu.
 
Hapa tupo tofauti si mila zetu ila ni utaratibu wa familia yetu ,hatulali na chombo kichafu hata 7 usiku vitaoshwa ..
 
Jirani zangu
Ni mwiko kutumia choo wao ni vichakani tu
 
yote uliyotaja isipokuwa namba tatu tu ni mwiko kwetu, nyongeza;
1. Mwanamke huruhusiwi kula firigisi, huu ni mwiko kwa jamii yetu
2. Mama mkwe hali kuku ukweni, huu ni mwiko kwa jamii yetu
3. Ukienda kuomba deni ama msaada hasa mfugo ukaenda na kamba, kama hutapata huo mfugo huruhusiwi kurudi na hiyo kamba, unaiacha sehemu husika uliyoenda
4. Mbweha kubweka jirani na nyumbani ni mkosi, tegemea msiba muda wowote
5. Mtoto wa kike kubeba mimba kabla hajakeketwa ni laana, hivyo inatakiwa umtupilie mbali na asirudi nyumbani (zamani)
6. Kuzaa mtoto akatanguliza miguu ni laana kwa ukoo wako
7. Mwanaume kuolewa na mwanaume mwenzake ni laana
8. Kijana kumpiga baba/mama yako ni laana kwa ukoo wako


Na mengine mengi, japo sababu ya mengine sijui maana tumerithi kwa wazee wetu
 
Asante kwa nyongeza mkuu. Bila shaka wewe ni mtu kutoka "Kanda Maalumu" Hiyo namba 3 hata kwetu ipo (unaacha kamba hadi mfugo ukipatikana kamba hiyo itatumika kuufunga). Hiyo ya kutooa binti asiyekeketwa au binti huyo kuzaa, ni kutoka kanda maalumu kabisa.

Halafu hiyo ya mtoto kutompiga baba yake kama ikitokea inakuwa ni laana inayoendelea kizazi hadi kizazi hadi lifanyike tambiko maalumu kuitengua.

Ni hivi ukimpig baba yako, nawe pia utapigwa na watoto wako nao watakaokupiga nao wao pia watapigwa tu....yaani unakuwa ni mwendelezo wa milele.

Hii nimeishuhudia pale kijijini kwetu. Kuna mzee mmoja alikuwa akimpiga baba yake. Naye watoto wake walimpiga na wale watoto wake waliompiga nao pia walipigwa na wao pia wanapigwa. Ni laana isiyofutika hadi tambiko lifanyike kutengua laana hiyo.
 
Kwenye kabila letu:
1. Ni mwiko mwanamke aliyejifungua kula nyama ya kuku. Inasemekana akila kuku maziwa yatakuwa hayatoki.
2. Ni marufuku mjamzito kula mayai. Ikiwa atakula mayai, atamzaa mtoto kipara (asiyekuwa na nywele).
 
hata ukimtusi Mama/Baba yako nawe lazima ijirudie kwako..
Ila mengine ni mazuri sana ili kuishi kwa kuheshimiana, mfano Dada yako kukuachia laana, au kuheshimu mali au kitu chochote kutoka kwa mtu mliyeoa sehemu moja, hivi ni baadhi ya vitu ambavyo wazazi wanatusihi sana. Wanasema fanya yote lakini epuka kutapeli mtu mliyeoa pamoja ama mali yake kupotelea kwako
 
Hiyo ya kumvuka mtu ipo na kwetu pia,

Kwetu huruhusiwi kulala kwenye kitanda shingoo ielekee kusini mwa kitanda bali ulale kaskazini mwa kitanda, mzungu wa nne kwetu ni marufuku.

Kwetu hurusiwi kushona nguo usiku.

Unapofiwa na mpendwa wako wote hamruhusiwi kuoga mpaka matanga yaishe kabisa.
 
Kurians.
 
Desturi ya nyumbani kwetu ukisonga ugali ukimaliza mwiko lazima uuoshe. Marufuku kuacha mwiko mchafu. Hata sijui ina maana gani ila nimekua nayo mpaka leo nikimaliza kusonga ugali lazima nioshe mwiko kabla hata chakula hakijafika mezani.
Mmelelewa vizuri sana, kama una mdogo wa kike niunganishe naye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…