Taja tabia yako/mazoea yako fulani hivi ambayo huyapendi na unasumbuka kuiacha/kuyaacha please don't be shy someone might give you a solution here

Taja tabia yako/mazoea yako fulani hivi ambayo huyapendi na unasumbuka kuiacha/kuyaacha please don't be shy someone might give you a solution here

Kuna tabia nyingine ambayo kwa % kubwa naelekea kuondokana nayo. Nilikuwa siwezi kumnyima mtu hela au kitu kama ninacho, kuna siku kuna kauli ilimtoka mtu niliona kama kanidharau sana na nikaona haja ya kuanza kubadilika. Tulipishana kidogo akaniomba hela nikamwambia sina, akaniambia najua utanipa tu hujuagi kumnyima mtu hizo ni hasira tu zikipoa utanipa, alisema ukweli ila niliona nna haja ya kubadilika.
Huna majukumu Bado,
Ukipata utaacha,I used to be like that.
 
Kuna tabia nyingine ambayo kwa % kubwa naelekea kuondokana nayo. Nilikuwa siwezi kumnyima mtu hela au kitu kama ninacho, kuna siku kuna kauli ilimtoka mtu niliona kama kanidharau sana na nikaona haja ya kuanza kubadilika. Tulipishana kidogo akaniomba hela nikamwambia sina, akaniambia najua utanipa tu hujuagi kumnyima mtu hizo ni hasira tu zikipoa utanipa, alisema ukweli ila niliona nna haja ya kubadilika.
Mazoea yalizidi
 
Kuna muda nawazaaaa afu nikishtuka naanza kujiuliza nilikuwa nawaza nini,hii tabia siipendi hivi
 
Yaani mpaka kwenye pochi nabeba, au nanunua kabisa hata nusu kilo na inaisha ndani ya dk 20 tu. Najitahidi kujizuia nashindwa
Yaaani shida sio mchele..
Ishu ni kuwa kumbe unakula officials..
Mpaka inafikia kipindi unanunua aiseee very serious 😂😂😂😂😂

Alafu makavu oooh
 
Pengine ntapata msaada hapa.
Mimi tabia nisiyoipenda ni kutokua serious na kufunguka sana yaani nikienda mahali sichelewi kuzoeana na mtu kirahisi yaani hiyo inapelekea mda mwingine naona watu hawanieshim labda ama wananichukulia poa (cjui) lakini sipendi vile ambavyo nazoeana na watu kirahisi, sipendi vile ambavyo nachekacheka lakini nimeshashindwa kujicontroo nifanyeje jamani ili kubalance Mambo, nicheke panapostahili na pasipostahili Basi nibakie kawaida.
 
Back
Top Bottom