Takriban wiki ya pili sasa hatuoni dalili ya yeye kutafuta hata shughuli, yaani yupo tu

Takriban wiki ya pili sasa hatuoni dalili ya yeye kutafuta hata shughuli, yaani yupo tu

Afu ndugu hawatumiagi akili,maisha ya sasa si ya kuganda kwa MTU muda wote huo afu utashangaa alikuja bila hata taarifa.Kwa kias fulan pia wanachangia kuvuruga amani ya ndoa za watu.Si wanandoa wote wanaweza stahimili kuishi na MTU nje ya wanaomhusu kweli tena kwa muda mrefu
 
We jamaa ungekua ndo mzee wangu mbona ungekufa kama sio kuzirai kabisa,
Nakumbuka mwaka 2009 kipindi tupo shy town mzee alikuwa ni askari na familia yetu kiujumla ilikuwa na watu takribani 7 hvi mara akaja babu yetu na familia yake ya watu 6 kukaa home hapo hapo wazazi wa mke mdogo na mzee nao wakatia timu wakiwa na watoto wao wa2 haya kama haitosh kina binamu watoto wa shangazi nao hawa hapa wa 2 lets calculate 7+6+4+2=19 na mtu anaelisha familia ni mmoja tu broh ungekuwa wewe ungekufaga mazima na iliwachukua takribani miezi zaidi ya miwili mpaka kuja kuondoka.
 
Nilijua umemtafutia kazi kagoma kufanya,kumbe lawama za kimama.
Mambo hayo ili bidi dada zako walete thread hapa...anyway.
Subiri apate ata ujanja wa kuingia na kutoka mjini 3month atajua pakutafutia kazi.
Malalamiko kwa mtu wa wiki 2 hata kuvuka barabara za mwendokasi hajajua kwa kweli hatuezi kukuambia mpe nauli arudi..hilo haliwezekani.
Mjini hpa pana hitaji kujuana ndo upate kazi.
Hata bodaboda tu mgundini utafukuzwa km hawakujui.
 
Asili ya mwanaume ni kujitegemea na kuwa na himaya yake......changamoto za kimaisha na harakati za kiupambanaji wakati mwingine zinapelekea kushindwa kusimama kwenye asili yetu lakini mipango na malengo vinabakia vichwani mwetu.....

Ukimuona mwanaume yupo comfortable na hali ya kuwa tegemezi iwe kwa mwanaume mwenzake au kwa mwanamke basi jua Kuna tatizo kwa huyo mwanaume.......

Kuendelea kwa hali hiyo kunaondoa kabisa au kudumaza Ile spirit ya kiuanaume ndani yake na matokeo yake anaingiwa na haiba za kike na kuanza kufanya matendo yanayoashiria uanamke kwani mwanamke pekee ndio mwenye asili ya kuhudumiwa.........

Zungumza na mwanaume mwenzio kiume na hali ya kimamlaka kama baba na kichwa Cha familia huku ukionesha kwa vitendo kuwa wewe ndio mwenye himaya yako........

Ukiona hakuna muendelezo chanya juu ya mazungumzo hayo unalazimika kufanya maamuzi magumu kama mfalme aliyevamiwa kwenye himaya yake........

Note:

Tuache mazoea ya kupokea wageni wasio na taarifa, wakati mwingine huwa wanakuwa wanakimbia matukio ya uhalifu huko walipotoka......
 
Si ni ndugu wa Mke wako? Maisha yetu Watz ni kwenye Lindi la umasikini hivyo mvumilie na ukiweza mchukue sehemu muongee kiume. Huyu unayetaka arudi alikotoka ndio alimlinda mke wako asiwe KAHABA.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]shemeji mkubwa ni baba mkwe
 
Toka out na shemeji yako mkapige story mbili tatu jaribu kumdodosa utamuelewa tu...

Kama issue ni kupigika, kama una uwezo muwezeshe apate cha kufanya then mtafutie chumba uswazi kodi ya 30k mlipie 6 month achana naye...
Akili hii
 
Wiki mbili mbona chache sana, mpe miezi mitatu bwana abadilishe upepo. Mgeni ni baraka, hakikisha anapata maandazi na mkate wenye blueband.
Phaller wewe, nimecheka sana[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Afu ndugu hawatumiagi akili,maisha ya sasa si ya kuganda kwa MTU muda wote huo afu utashangaa alikuja bila hata taarifa.Kwa kias fulan pia wanachangia kuvuruga amani ya ndoa za watu.Si wanandoa wote wanaweza stahimili kuishi na MTU nje ya wanaomhusu kweli tena kwa muda mrefu
Dunia ya sasa upendo umekwisha.Mimi napenda Sana wageni.
 
Back
Top Bottom