ni takribani wiki 2 zilizopitata nilipata ugeni wa kaka yake mke wangu na tulimpokea vizuri tu.
Alifika mida ya saa 2 bila taarifa na niwe muwazi kwamba hata mgao wa chakula ulivurugika,
Usiku ule ule tukiwa chumbani nilikuwa namhoji wife kwanini ndugu yake kaja bila taarifa ila nikapotezea nikijua labda atakaa siku 2 au 3.
kuna vyumba vya wageni vimejitenga na nyumba kuu ndiko tulipompa hifadhi, na choo / bafu ni humo humo.
sasa ni takribani wiki ya pili sasa hatuoni dalili ya yeye akitafuta hata shughuli, yani yupo tu.
Wife akimuuliza hali, yeye anasema kaja kutusalimia na binafsi sina tatizo na hilo bali huyu ni mtu mzima ambae pengine ilibidi awe anafanya shughuli za kumuingizia kipato