Takriban wiki ya pili sasa hatuoni dalili ya yeye kutafuta hata shughuli, yaani yupo tu

Dah!!,Hao ni Wanyakyusa Nini??.
 
Ufala huu sifanyi, utakuta alikuwa anaumia moyoni kimya kimya tu
 
Extended family inatutesa sana Africa, ndiyo maana hatuendelei maana akitoka huyo atakuja Shangazi then Mjomba
 
Naomba ufanye kitu kimoja mkuu.

Kwanza tambua kwamba maisha ni kupanda na kushuka,unaweza ukafa leo watoto wako wakaja kulelewa na huyo jamaa(mjomba wa wanao) hivyo hakikiaha unahukumu mambo kwa kuepuka vinyongo kwa hao unaowahukumu.

Kiukweli asoli ya aisi wanaume wengi huwa hatupendi ndugu wa kiume wa wake zetu,tunapenda sana ndugu wa kike wa wakw zetu.


Cha kufanya jitahidi siku moja moja utoketoke naye out alafu siku moja ukitoka nae muulize kuhusu maisha zaidi huko alikotoka na wewe muulize viswali vidogo vidogo

Ila kabla ya kutoka nae muulize mkeo kwamba kaka yake alikuwa anafanya shughuli gani akikuambia happ utapata pa kuanzia na kumuuliza maswali yafuatayo..

Dada yako alinambia k2amba unajishughulisha na shughuli fulani kule nybani,vipi inaendeleaje sasa hivi ?

Anakujibu....
Kisha unamuuliza tenaa vipi biashara/shughuli yako jmemuachia nani huko nyumbani...? Hapa ndio utajua mzizi wa jambooo loooteeeeee
 
Week mbili tu unapiga kelele mkuu, sa Mimi kaja baba,mama na mtoto mmoja wa Dada wa kazi wakamaliza mwezi home unafanyaje
 
Una uhakika nibkaka Ake kweli?! Isije ikawa ni mchepuko wake.
 
Binafsi nilishajiongeza kitambo, nikisafiri mikoani sifikii kwa ndugu, nina bajeti yangu ya hotel na isitoshe napenda freedom.

Nitafanya misele yangu iliyonileta nikijisikia nitakuja kuwatembelea nyumbani na kuondoka au ikibidi tukutane maeneo ya town tupige chupa tuachane.

Dunia imeshabadilika binadamu siyo watu.
 
Week mbili tu unapiga kelele mkuu, sa Mimi kaja baba,mama na mtoto mmoja wa Dada wa kazi wakamaliza mwezi home unafanyaje
Mwanaume mlaze chumba cha watoto wa kiume na mke wake mlaze chumba cha watoto wa kike wawe wanakutana sebuleni tu na muda wa kula, wala hawawezi kukaa muda mrefu wataondoka.
 
Binafsi mimi naona uchoyo ndiyo unamsumbua mleta mada,kama umejaaliwa kuwa na sehemu ya kulala mgeni sidhani kama chakula ni shida sana,kwani anakula sado ngapi za mahindi kwa mlo mmoja hadi umchoke kiasi hicho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…