Takriban wiki ya pili sasa hatuoni dalili ya yeye kutafuta hata shughuli, yaani yupo tu

Umaskini tu na roho za uchoyo ndio kimesababisha uandike uzi humu.
Umejaribu kununiia jembe na kumuonesha shamba akakataa kulitumia?
Je umemuonesha kazi ya kufanya akagoma?

Acha UCHOYO wali utakuotesha kutambi tu ufu kwa kisukari
 
Mnywee pombe then mchane asepe
[emoji2][emoji2][emoji2]umenikumbusha mbali sana mkuu hii comment yako,by the way hata Mimi sometimes nikitaka nimchane live mtu ninaemheshimu huwa namnywea za kutosha halafu namchana mbaya ,kesho huyoo mwenyewe anasepa
 
N
KUNA JAMAA MMOJA WA KIPARE NAMJUA
KWAKE MLANGONI KUNA TANGAZO KABISA
KUHUSU NDG,WAGENI WAKIJA
KATIKA MAKAUZU HUYO NI KAUZU
AISE😂😂

ova
Na ndo inatakiwa ivoo..mtu umekuja c kwamba unasoma au kuna issue serious imekuleta...unakuja na kukaa kwa mme wa dada yako wk nzimaa..sion kama ni ustaarabu...hii nmeiona sanaa usukuman
 
Mtafutie mahali pa kuanzia aweze kuingiza kitu chochote hata kama ni buku mbili kwa siku.

Si kwamba na yeye anapenda kuishi kwa shemeji wala kuitiwa wa kengele bali amekwama pa kuanzia.

Ni ngumu sana kuelewa mazito aliyoyabeba ikiwa wewe hukuwahi kukivaa KIATU chake.

Mpambanie huyo ni JEMEDARI mwenzio, Hata kama si kwa KESHO na KESHO KUTWA lakini siku moja atakuinua wewe ama mmojawapo katika familia yako.
 
Mkuu tafuta fremu mjini hapo ulipo anzisha kibanda/duka au tafuta laini za uwakala M-Pesa, tigo pesa & Airtel Money siku hizi ni masaa 2 tu kutengeneza laini za uwakala ukiwa na documents zote weka vitu sawa i mean mtaji na mkabidhi awe busy na ofisi, kama unajiweza zaidi mpangishie na chumba kabisa hata cha 20k-30k aanze maisha..

Haya maisha yana fumbo kubwa sana yana ups & downs, yaweza kua kapigika huko alikotoka hata mlo wa siku imekua shida ku afford, usimchukie na usiwe na ROHO ya "KWANINI NA UBINAFSI" hujui kesho yako huyo jamaa anaweza kuja kua msaada mkubwa sana kwako kwa life la baadae.


Misho: si vizuri kusemelea mambo sensitive ya familia yako huku je kama yuko humu au dada ake yuko humu na kaona hii unafikiri watajisikiaje?!
 
Mwanaume mlaze chumba cha watoto wa kiume na mke wake mlaze chumba cha watoto wa kike wawe wanakutana sebuleni tu na muda wa kula, wala hawawezi kukaa muda mrefu wataondoka.

Akianza kuwaingilia watoto ndo utaelewa kwanini jamaa kamuweka nje
 
Inasikitisha sana kuona watu tunajali sana chakula kiasi cha kuwachukia ndugu zetu wanapotutembelea majumbani mwetu tukihisi kuwa wamekuja kutumalizia chakula.

Chakula ni nini ?? Chakula ni mavi tu na siyo zaidi. Tuwe na upendo na tuwe na amani katika kushiriki na wenzetu katika kile kidogo tulichonacho.

Kaka yake na Mkeo hata akikaa kwako mwaka mzima kuna shida gani? Ni chakula gani atakachokula kwa mwaka mzima kitakachokufanya wewe uwe maskini??

Sisi Wakristo tumefundishwa upendo, imeandikwa; "mpende jirani yako kama nafsi yako".

Jirani yako ni nani? Jirani yako ni mtu yeyote yule hata huyo Shemeji yako ni jirani yako.

Ukiona mtu anakukwaza, mwambie na siyo kunung'unika chini chini au kumsengenya mitandaoni. Usengenyaji ni dhambi pia.
 
Mtu mzima kuenda salimia na kuvusha usiku mmoja tu naona nayo imekaa kizembe unless iwe kuna shughuli .

Mimi hata kwa ndugu huwa hata sikanyagi unless kuna tukio.

Mtu mzima ndevu zako upo upo tu
 
Nyumba mkiishi family kubwa inachangamka sana,wengine tushazoea kupokea wageni. Maana wengine siyo ndugu lakini huko kijijini wanaambizana ukienda mjini kutafuta maisha kafikie kwa mama fulani,,,hivyo yaani amani tupu[emoji120],
 
Kwanza pole mkuu kwa KUTOKUWA na Falsafa inayoendesha maisha yako ya nyumbani kwa kiasi kikubwa,hili ni tatizo la watu wengi kuishia kulalamika||kulaumu||kunung'unika pasipo kuishi vile wanavyotaka wao 'kama kitu hukipenda kiseme kwa muhusika kama kilivyo kuliko kuishi nacho huku kinakutesa'_In short tengeneza 'honest philosophy' itakayoongoza maisha yako wakati wote[emoji41]...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…