TAKUKURU: CHADEMA badala ya kulalamika wanapaswa kusoma sheria, mwisho wa uchunguzi waweza kuwa mwanzo wa uchunguzi mwingine

Shida ya takukuru wanna Nia ovu hivyo ndivyo inavyoonekana machoni pa watu Nia Yao ni kuipaka matope cdm kuibrand jina baya lakini dunia inaona na inajua Nia zao za kishetani na ndio maana taifa likipatwa na shida watu wanafurahi kwasababu Kuna upande unaonewa wazi wazi na mwingine unapendwa .
 
Naona ccm mnajua sana sheria.

Unaweza nunua ndege bila bajeti kupitia bungeni?

Katika hili sheria inasemaje?

Au nyie mnajua sheria ya takukuru tu?
Kwani daraja la kiegea barabara ya Dodoma lilikuwa na bajeti yake iliyopitishwa bungeni ?
 
Wanasubiri kampeni zianze ndio watoe matokeo ya uchunguzi wao wa akina Lijualikali & company Ltd.))
 

1. CHADEMA hawalalamiki. Kama kulalamika ni huko, basi hata TAKUKURU kwa taarifa yao hii, nao wanalalamika....

2. TAKUKURU hawa wanawaambia CHADEMA wakasome sheria inayounda TAKUKURU na majukumu yake. Yaani kwa akili zao wanaamini CHADEMA hawaijui sheria hiyo?

3. Hii kitu ya TAKUKURU vs CHADEMA dhidi ya kile kinachoitwa "uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha CHADEMA" ni sawasawa na kesi nyingine zozote tunazoziona zikilindima mahakamani...

4. Hapa kwa kweli kinachofanywa na TAKUKURU wala hata siyo uchunguzi bali ni mshtaki/mlalamikaji kutaka kumtia hatiani mlalamikiwa kwa LAZIMA....!

5. CHADEMA, nawashauri litendeni jambo hili si katika namna ya kuwa "MNACHUNGUZWA" bali tambueni kuwa hapa "TAYARI MMESHITAKIWA" na kinachotaka kufanywa si muda mrefu ni kuwatangaza kuwa "MNA HATIA" na kisha maamuzi kutolewa. Ni vyema mmeshtuka mapema kabla ya plan yao ku - mature. Hii inaweza ku - divert kila kitu under your favour..!!

6. Hii njia ya KUJIBIZANA NAO HADHARANI ni nzuri sana. Ndiyo maana mmewakurupua huko walikokuwa na kuanza kujitetea. Lakini hapo kabla mlikuwa mnawaandikia barua kuwaomba ufafanuzi wa mambo fulani fulani ktk uchunguzi wao, walinyuti bila kujibu barua zenu. Lakini kwa njia hii, tayari wako hadharani nao wanalalamika....!!

Ndiyo; hiki walichofanya leo ni kwa hakika kabisa ni kujitetea. Na mtu anayeplan kukutendea baya, ukamgundua mapema na kumtangaza hadharani, lazima atoke tu kujibu na kujitetea. Hiki ndicho walichofanya TAKUKURU....

Na hili ni jema kwenu. Endeeleni hivi hivi. Wakisema jambo ktk public kuwahusu, immediately kabla ya uharibifu kuenea, nanyi jitokezeni public kwa njia kama waliyotumia wao na kujibu....!!
 
Vyombo vya dola vyote siasa
 
Ubadhirifu ni kosa la jinai la kawaida tu ambalo lingechunguzwa na polisi. Hawa Takukuru kuifanya hii ni big issue ni rahisi sana kwa jamii kuhitimisha kuwa inatumika kisiasa katika suala hili. lakini kikubwa ni kwamba hizi tuhuma za ubadhirifu zinazozungumziwa sio mambo mapya, yameandikwa sana muda mrefu tu, kwanini Takukuru waibuke sasa baada ya wabunge waliofukuzwa Chadema kusema bungeni, tena kwa namna ambayo Bunge lenyewe chini ya Ndugai lilikuwa lina back up? Takukuru wanajua kuwa CAG kapitia matumizi ya Chadema akaridhika, michango inayolalamikiwa na akina kulialia Lijuakali ipo kikatiba ndani ya chama!
 
Unaijua sheria ya TAKUKURU lakini?
Ndiyo, ni ile iliyowazuia kuchunguza suala la rushwa kwa aliyekuwa D. C wa meru na sasa R. C wa Manyara Alexander Mnyeti, japo walipelekewa ushahidi wa video. Sote tunajua kilichotokea, ni kweli kabisa sheria ya Takukuru inaona kwa makengeza.

Waanze kwanza na Mnyeti ndo tujue kweli kuwa wako huru kama wanavyojinasibu
 
Tatizo chadema wanapiga hela wakidhani wanaishi kwenye space .wakiulizwa break ya kwanza ni kwenye mic .nchi imebadirika hii si kila kitu siasa. Zingekuwa siasa kandambili na shuka zingekamatwa?
 
Eti chombo kilichobobea. Hawa takukuru wanalipi la kujivunia kuwa wamelifanya.

Wakuu wanatumia madaraka vibaya hadi kutumbuliwa na Rais wengine wakipewa onyo wao wapo tu.

Ufisadi umetamalaki,lakini wao wanajivunia weledi kubaki maofisini.

Ununuzi unafanyika bila kuzingatia sheria za manunuzi ya umma...wao wapo tu.

Hii taasisi inajishushia heshima sana. Nilidhani kupewa bwana afande walau itanyoosha uhuni wote kumbe maweeee.
 
Takukuru ni vyema mkae pembeni na shinikizo la ccm kuwashurutisha kawaonea chadema kwani mnaendelea kuonekana waonevu wa wazi pasipo shaka
 
Tatizo chadema wanapiga hela wakidhani wanaishi kwenye space .wakiulizwa break ya kwanza ni kwenye mic .nchi imebadirika hii si kila kitu siasa. Zingekuwa siasa kandambili na shuka zingekamatwa?
CCM zimepigwa pesa nyingi ni kwa nini Takukuru hawaendi huko?
 
Hata aliyekuwa mhasibu wa Takukuru yupo jela kwa kujipatia mali kinyume cha sheria, Takukuru nao wana mapungufu yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…