Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,042
- 17,320
Huko Mbeya tumeona watumishi wa TRA wakichepusha hela ya umma kuingia kwenye mtandao wa watu binafsi na kupiga hela. Huko Arusha tumeona mkutano wa Makonda mwananchi mlipa kodi (Halmashauri ya Arusha) akilalamika kodi zinachepushwa na kuingia katika mtandao wa wapigaji na wala haziingii serikali kuu. Hata Rais katika hotuba zake aliwahi kusema kwa mujibu wa ripoti ya CAG mifumo ya ukusanyaji kodi haisomani.
Sasa mimi hebu niwaelekeze mahali palipo na wizi wa kuchepusha hela za michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma ni wizara ya fedha (HAZINA). Hakuna mwajiriwa hata mmoja ambaye katika utumishi wake anaweza kukuta hakuna kasoro ya malipo yake ya mwezi ya 20%. Utakuta miezi kadhaa wamepeleka pungufu au hakuna kabisa. Ukienda kudai malipo lazima uandike barua ya mapunjo na haya madai huwa hayalipwi kabisa! Utadai na kuandika barua mpaka unaamua kuacha na kukata tamaa kabisa!
Nina jamaa zangu wengi kabisa katika taasisi za umma hawakupelekewa 15% ya michango yao kwa zaidi ya miaka kadhaa. Walikuwa wanapelekewa 5% nyingine inachepushwa kusikojulikana. Wengine wamestaafu, kuachakazi, kufariki wamedai hela yao mpaka wamechoka. Hebu wahusika sijui TAKUKURU, PSSSF, NSSF sijui nini wawaangalie hawa jamaa wa HAZINA katika suala zima la michango ya watumishi.
Nina uhakika na wao wamejitengenezea kamfumo kakuchepusha na kuiba kiasi fulani cha michango kwa kila mtumishi wa umma. Nasema hivyo kwasababu ukienda kudai hulipwi mpaka utachoka! Ukienda ofisini kwao utaambiwa sijui nani na nani anahusika sijui hayupo sijui tutalifanyia kazi! NARUDIA! Michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma kwa ujumla inapigwa sana!