TAKUKURU chunguzeni Wizara ya fedha (Hazina) huenda imetengeneza mfumo wa kuiba hela ya mafao ya watumishi wa umma

TAKUKURU chunguzeni Wizara ya fedha (Hazina) huenda imetengeneza mfumo wa kuiba hela ya mafao ya watumishi wa umma

Huu wizi ni system, na bahati mbaya awamu hii ndio umegeuzwa tabia, jamaa wanaiba na hawaogopi kwasababu wanajua aliyepo pale juu hajielewi wala hajitambui, ni kama mlevi aliyelewa chakari.

Tuna kiongozi dhaifu sana kuwahi kutokea kwenye hili taifa.
aliwambia wale kidogo wasivembewe hatujawai pata kiongozi wa ajabu kama huyu...
 
Huko Mbeya tumeona watumishi wa TRA wakichepusha hela ya umma kuingia kwenye mtandao wa watu binafsi na kupiga hela. Huko Arusha tumeona mkutano wa Makonda mwananchi mlipa kodi (Halmashauri ya Arusha) akilalamika kodi zinachepushwa na kuingia katika mtandao wa wapigaji na wala haziingii serikalini kuu. Hata Rais katika hotuba zake aliwahi kusema kwa mujibu wa ripoti ya CAG mifumo ya ukusanyaji kodi haisomani.

Sasa mimi hebu niwaelekeze mahali palipo na wizi wa kuchepusha hela za michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma ni wizara ya fedha (HAZINA). Hakuna mwajiriwa hata mmoja ambaye katika utumishi wake anaweza kukuta hakuna kasoro ya malipo yake ya mwezi ya 20%. Utakuta miezi kadhaa wamepeleka pungufu au hakuna kabisa. Ukienda kudai malipo lazima uandike barua ya mapunjo na haya madai huwa hayalipwi kabisa! Utadai na kuandika barua mpaka unaamua kuacha na kukata tamaa kabisa!

Nina jamaa zangu wengi kabisa katika taasisi za umma hawakupelekewa 15% ya michango yao kwa zaidi ya miaka kadhaa. Walikuwa wanapelekewa 5% nyingine inachepushwa kusikojulikana. Wengine wamestaafu, kuachakazi, kufariki wamedai hela yao mpaka wamechoka. Hebu wahusika sijui TAKUKURU, PSSSF, NSSF sijui nini wawaangalie hawa jamaa wa HAZINA katika suala zima la michango ya watumishi.

Nina uhakika na wao wamejitengenezea kamfumo kakuchepusha na kuiba kiasi fulani cha michango kwa kila mtumishi wa umma. Nasema hivyo kwasababu ukienda kudai hulipwi mpaka utachoka! Ukienda ofisini kwao utaambiwa sijui nani na nani anahusika sijui hayupo sijui tutalifanyia kazi! NARUDIA! Michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma kwa ujumla inapigwa sana!
Kuna mwezi mmja kwenye makato yangu haujasoma ,niliwahi andika barua kwa.mwajiri sijapata majibu ya Kwa nini nikatwe pesa harafu isisome kwenye michango.

Naunga mkono hoja,hili.lipo.na bila shaka wakubwa kabisa ndio wanufaika
 
Unaangaliaje hiyo michango kama imepelekwa PSSSF, ebu nisanue mimi huwa nafikiri michango inakatwa automatic na kuingia automatic PSSSF
Downlaod app ya PSSSF Playstore au Appstore.... Kisha fuata maelekezo ya kujisajili..
 
Kuna mwezi mmja kwenye makato yangu haujasoma ,niliwahi andika barua kwa.mwajiri sijapata majibu ya Kwa nini nikatwe pesa harafu isisome kwenye michango.

Naunga mkono hoja,hili.lipo.na bila shaka wakubwa kabisa ndio wanufaika
Bora wewe mwezi mmoja! Wengine miezi 18 mfululizo wanapeleka 5% tu badala ya 20%
 
Back
Top Bottom