TAKUKURU mchunguzeni Mkuu wa Wilaya Morogoro, anaitumia ofisi yake vibaya

Anajiharibia sana

Anajiharibia kwa nani mkuu? Kumbuka hicho cheo ni kichaka cha upigaji na hakuna hatua zozote za maana huwa zinachukuliwa. Huyu aliingia CCM kipindi cha siasa za uzalendo wa kiki. Lengo lake la kujiunga CCM ilikuwa ni kusaka ulaji, na sasa amepata nafasi hiyo.
 
Mbona unaleta hoja halafu ni wewe huyo huyo unajibu na kutetea hoja? Nina mashaka na wewe utakuwa umetumwa.

Sisi wanyonge ametundea makubwa na tunamshukuru mno. Endelea kuhongwa na wanasiasa wanaohofia ubunge wao

Unataka kuspin mjadala? Hebu kuwa serious. Hoja hapa ni uhuni unaofanyika kinyume na sheria. Kuiomba TAKUKURU kuchunguza madai haya kutasaidia kujua mbivu na mbichi. Hutaki?
 
Kumiliki law firm ndio sababu ya kuvunja sheria na kufanya ulaghai? Unajua hii ishu iko serious sana na pengine ikamgharimu nafasi yake? Umeandika kama ni jambo la mzaha vile
Ikiuma chomoa.
 
Aliuaminisha umma. Naachaje kumuamini kiongozi aliyepewa dhamana na taifa?

Hapo ndio unapokwama, mtu akipewa dhamana ndio umwamini? Kwenye mfumo ambao wanaoteua wanaingia madarakani kwa wizi wa kura tena wa wazi unategemea uadilifu gani hapo?
 
Hapo ndio unapokwama, mtu akipewa dhamana ndio umwamini? Kwenye mfumo ambao wanaoteua wanaingia madarakani kwa wizi wa kura tena wa wazi.

Ukipewa dhamana tafsiri yake umeaminiwa.
 
Ukipewa dhamana tafsiri yake umeaminiwa.

Uko sahihi, lakini nasema wanaokupa hiyo dhamana ni wasafi? Unadhani Msando hajui kuwa mfumo umeoza? Kwa taarifa yako Msando alikuwa ni mtu mwenye shughuli zake zinazomuingizia kipato, mshahara wa uDC kwake si kitu, bali alikubali hicho cheo kwa kujua fika ni wapi atapigia pesa.
 
Stendi ya Mafiga ameigeuza bar. Huyu jamaa hatari sana, yaani kachukua stendi kaifanya bar.
 

Najaribu kuelewa position yako kwenye hili; unamsifia DC kwa kupiga pesa za umma?
 
Stendi ya Mafiga ameigeuza bar. Huyu jamaa hatari sana, yaani kachukua stendi kaifanya bar.

Basi inawezekana ana makandokando mengi sana. Ndio maana nashauri achunguzwe kujua mbivu na mbichi.
 
Si waliambiwa wale kwa urefu wa kamba zao!! Wana kibali cha kufanya hayo wafanyayo.
 
Najaribu kuelewa position yako kwenye hili; unamsifia DC kwa kupiga pesa za umma?

Nasema hivi, Msando alikubali hicho cheo sio kwa ajili ya mshahara, bali ni sehemu ya upigaji. Sijawahi kusifia wahuni wa aina ya Msando.
 
Mbaya zaidi, inasemekana Mkurugenzi na watumishi wa Halmashauri wametishiwa kufukuzishwa kazi endapo hawataidhinisha malipo hayo batili.
Nilipoona mkurugenzi kutishiwa kufukuzwa kazi na mkuu wa mkoa wakati mamlaka ilyomteua ni raisi nikapata wasiwasi huenda hizi ni fitina za kumchafua Msando.

Hii habari inaweza kuwa ya kweli lakini kwa maneno hayo hapo juu inaonekana ni ya kimchongo majungu.
 
Tafuta Hela bwana mdogo !
 

Kuna tofauti kati ya kufukuzwa na kufukuzishwa. Soma kwa umakini.

Halafu migogoro ya DCs na Wakurugenzi haipo Morogoro tu, unajua sababu ni nini?

Think.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…