TAKUKURU yaanza kuichunguza CHADEMA kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Kumbe uliishahama CHADEMA? Basi yafaa ujitahidi sana kutumia nguvu yako kupajenga huko ulikohamia.
 
Kumbe uliishahama CHADEMA? Basi yafaa ujitahidi sana kutumia nguvu yako kupajenga huko ulikohamia.
Hapana mkuu, mpaka SASA sina Chama, baada ya kuhama nikaamua kuwa mshabiki mzuri wa mtu mmojammoja toka chama chochote
Mfano, mimi ni mshabiki mzuri wa Siasa za Mbowe ingawa mahali padoogo Sana ninapotofautiana naye

Kwingine, Mimi ni mshabiki mzuri Sana wa JPM na Kasimu Majaaliwa waziri mkuu, pia John mnyika namkubali sana huyu jamaa
 
Tatizo ni akili ndogo. Kwa hiyo unadhani Pccb hamna Auditors?
Toka lini? PCCCB ina Auditors wenye weledi huo? nani kakudanganya? kama wataalamu wa sheria tu ni sheeda, PCCCB ina mawakili kibao ambao mwisho wa siku wanapeleka majalada kwa DPP ambayo yana makosa kibao na mwishowe kesi wanashindwa au mawakili wa DPP wanagoma kuendelea na kesi maana mwisho ni kushindwa. Hivi ile issue ya hela za serikali zilizodaiwa zimeliwa na TFF ilihali hazikuingia kwenye akaunti za TFFwamemalizana nayo kwanza?
 
Ccm wanaogopa uchaguzi mkuu ujao kuliko chadema.

Hizi figisu ni maandalizi ya kupita bila kupingwa
 
na wewe umejiona umetoa pointi kama watu wangekuwa wanajiunga jamiiforums kwa kufanya mtihani hata wa uelewa wa mambo sidhani kama ungekuwepo na kuongea upuuzi wako
Mkuu nimepitia prevention and combating of corruption Act nimejiridhisha kuwa nilichokuwa nafikiria sicho. Jamaa wanamajukumu ambayo sikudhania hapo mwanzo. Wako sahihi kukichinguza chama cha demokrasia na maendeleo kutokana na zile allegations.
 
Mkuu mimi sio mwanachama wa hiko chama ila huwa nasimamia ukweli nakupinga pale panapohotajika kwa maslahi mapana ya utanzania wangu. Nimejiridhisha baada ya kusoma PCCB act upande wa key responsibilities nimeelewa mkuu
 
Mkuu PCCB husimamisha watu/taasisi mahakamni au hupeleka jalada kwa DPP then DPP akiona kuna haja ya kesi ndiyo huenda mahakamani? kwa maana nyingine PCCB lazima apitishe mambo yake kwa mwendesha mashtaka wa serikali then ndiyo yaende mahakamani. Si kweli kuwa PCCM in watu wa kila taalamu na yenyewe inategemea taarifa za idara/taasisi mbalimbali ambazo ni mahsusi kwenye utaalamu fulani. Maana ingekuwa ina watu wa kila taaluma ingekuwa balaa!
 
Majukumu ya CAG ni ya kikatiba wakati TAKUKURU ni suala la kipolisi. Kwa mujibu wa katiba yetu CAG akisha kagua mahesabu hakuna mamlaka nyingine ya kumkagua.
Sio kweli TRA wamekuwa wakifanya special audit kibao watu wanadaiwa Kodi kibao za miaka ya nyuma yakiwemo mashiririka ya umma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…