ostrichegg
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 12,050
- 6,199
WE shall overcomeAudit report ya CAG inatoa reasonable assurance not absolute. Hii ya TAKUKURU ni investigation ambayo itatoa absolute assurance. Tulia taasisi ifanye kazi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
WE shall overcomeAudit report ya CAG inatoa reasonable assurance not absolute. Hii ya TAKUKURU ni investigation ambayo itatoa absolute assurance. Tulia taasisi ifanye kazi
Kumbe uliishahama CHADEMA? Basi yafaa ujitahidi sana kutumia nguvu yako kupajenga huko ulikohamia.Inatategemea mkuu, maana unaweza ukakutwa uko Safi na ukaendelea kushuka vilevile,
Yako mengi mno yanayochangia Chama changu cha zamani Chadema kushika,
Kufukuza watu kinyume na Sheria na bila kosa
Na cha msingi kabisa bila kuficha na sio kubebwa na mihemko ya kisiasa, Chadema mtakwepaa weee, lakini ukweli utabaki palepale kuwa, Kwa sasa, Chadema inahitaji kiongozi Msomi ngazi ya Digree angalau
Shida zote zilizoko huko ni za kitalaamu zaidi,
Ni miaka mingi sasa, Chadema haijajieneza kimatawi nchi nzima mpaka Leo tunazungumzia miaka zaidi ya Ishirini na... Chama hakina jengo linaloashiria nguvu ya Chama,
Nipondeni, lakini, Elimu, Elimu, Elimu, huwezi kuliepuka hilo
Hapana mkuu, mpaka SASA sina Chama, baada ya kuhama nikaamua kuwa mshabiki mzuri wa mtu mmojammoja toka chama chochoteKumbe uliishahama CHADEMA? Basi yafaa ujitahidi sana kutumia nguvu yako kupajenga huko ulikohamia.
Toka lini? PCCCB ina Auditors wenye weledi huo? nani kakudanganya? kama wataalamu wa sheria tu ni sheeda, PCCCB ina mawakili kibao ambao mwisho wa siku wanapeleka majalada kwa DPP ambayo yana makosa kibao na mwishowe kesi wanashindwa au mawakili wa DPP wanagoma kuendelea na kesi maana mwisho ni kushindwa. Hivi ile issue ya hela za serikali zilizodaiwa zimeliwa na TFF ilihali hazikuingia kwenye akaunti za TFFwamemalizana nayo kwanza?Tatizo ni akili ndogo. Kwa hiyo unadhani Pccb hamna Auditors?
Ccm wanaogopa uchaguzi mkuu ujao kuliko chadema.TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imeanza kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, inazokikabili Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
“Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo, kuna matumizi mabaya ya fedha za michango ya wanachama, ambayo kwa mujibu wa katiba yao wanadai imeanishwa wachangie.”
“Lakini, matumizi yake ndio wanatilia mashaka, kuna fedha nyingi zinatumika ndivyo sivyo, kwa mujibu wa makubaliano yao,” amesema Jenerali Mbungo.
“Kwa hiyo, tunachunguza matumizi yasiyo sahihi ya fedha zao, Takukuru inayomamlaka ya kuchunguza taasisi yoyote iwe ya umma, watu binafsi, chama, klabu, iwe chochote Takukuru wanaingia kufanya uchunguzi, ilimradi kuwe na ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha na rushwa,” amesema bosi huyo wa Takukuru.
Mbungo amewataja baadhi ya watakaohojiwa ni; Dk. Vincent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema, ambaye kwa sasa amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM), John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje Chadema, pamoja na mhasibu mkuu wa chama hicho, Dk. Roderick Lutembeka.
Aidha, Jenerali Mbungo amesema wameshindwa kumhoji Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuhusu sakata hilo, kwa kuwa aliieleza TAKUKURU kwamba yuko nje ya jiji la Dar es Salaam.
Amesema, taasisi hiyo imeshaanza kukusanya nyaraka mbalimbali, zinazohusiana na tuhuma hizo.
“Tumeshapata nyaraka kutoka sehemu mbalimbali, wametupatia nyaraka, wamekuwa wanatoa ushirikiano katika hili,” amesema Mbungo.
Jumamosi ya tarehe 23 Mei 2020, Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, alikanusha tuhuma hizo, akisema kwamba, hakuna uthibitisho unaoonesha chama hicho kina matumizi mabaya ya fedha.
Kigaila alisema, fedha za michango ya wabunge na zinazotoka kwa wadau wengine wa Chadema, matumizi yake hupangwa na vikao vyake vya chama, wakati bajeti ya matumizi hayo ikipitishwa na baraza kuu, kisha taarifa zake hutolewa na kamati kuu ya chama hicho.
Kigaila alisema, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hukagua taarifa za matumizi ya Chadema, na kwamba kwa mujibu wa ukaguzi huo, hakuna ushahidi kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.
Mkuu nimepitia prevention and combating of corruption Act nimejiridhisha kuwa nilichokuwa nafikiria sicho. Jamaa wanamajukumu ambayo sikudhania hapo mwanzo. Wako sahihi kukichinguza chama cha demokrasia na maendeleo kutokana na zile allegations.na wewe umejiona umetoa pointi kama watu wangekuwa wanajiunga jamiiforums kwa kufanya mtihani hata wa uelewa wa mambo sidhani kama ungekuwepo na kuongea upuuzi wako
Mkuu mimi sio mwanachama wa hiko chama ila huwa nasimamia ukweli nakupinga pale panapohotajika kwa maslahi mapana ya utanzania wangu. Nimejiridhisha baada ya kusoma PCCB act upande wa key responsibilities nimeelewa mkuuHivi unajua siku hizi listi za za EFD zinanunulika mkuu, Ni rahisi kununua listi za matumizi ili kumficha mkaguzi, Ila TAKUKURU huwezi kuificha Kwa mambo hayo ndugu
Tulizana, ni namna ya kumjua mwizi wa pesa za Chama chako ili pia sasa Chama kijitanue, kifike na kwenye matawi vijijini huko
Shida ya nini Wakati unasaidiwa mkuu
Mkuu PCCB husimamisha watu/taasisi mahakamni au hupeleka jalada kwa DPP then DPP akiona kuna haja ya kesi ndiyo huenda mahakamani? kwa maana nyingine PCCB lazima apitishe mambo yake kwa mwendesha mashtaka wa serikali then ndiyo yaende mahakamani. Si kweli kuwa PCCM in watu wa kila taalamu na yenyewe inategemea taarifa za idara/taasisi mbalimbali ambazo ni mahsusi kwenye utaalamu fulani. Maana ingekuwa ina watu wa kila taaluma ingekuwa balaa!PCCB ina wahasibu, mainjinia, wanasayansi, kila taaluma! Maana yake huwa ni hiyo na wana uwezo wa kukusimamisha mahakamani. CAG hana madaraka hayo.
Hata hivyo, huyo boss wa CHADEMA, Mbowe, kwa nini busara yake iko kwenye kunyamazia tuhuma na matatizo ya kifedha? Akisimama huwa anajibu mambo ya mitaani tu! Fedha huwa anakwepa utadhani ni mara ya kwanza kumtaja ktk ufisadi. Sasa yanakuja ya Lijualikali juu ya kukwepa kulipa kodi ya magari kwa udanganyifu. Hayo ndo matatizo ya kutoheshimu waovu wenzake.
Sio kweli TRA wamekuwa wakifanya special audit kibao watu wanadaiwa Kodi kibao za miaka ya nyuma yakiwemo mashiririka ya ummaMajukumu ya CAG ni ya kikatiba wakati TAKUKURU ni suala la kipolisi. Kwa mujibu wa katiba yetu CAG akisha kagua mahesabu hakuna mamlaka nyingine ya kumkagua.
Cheki makengeza yake utafikiri mjusi kabanwa na mlango!! Lazima wakaguliwe mnahangaika ya nini tulieni
Mtaokoteza sana viandiko uchwara mwaka huu, pelekeni document, ajabu sana watu wanaibiwa then kuna mtu anajitolea kuwasaidia kumjua mwizi Mara wanamgeuka hawataki kusaidiwa, nyie watu vepe
Takukuru wanakamata, ila CAG hakamatiKwa hiyo TAKUKURU wameamua kufanya kazi ya CAG?
[emoji12][emoji12][emoji12][emoji44]Acha kulalama..
Si tunataka kuwakomesha ccm?
Yani kwa vile sisi chadema ni safi, ngoja takukuru watuchunguze ili tuwafunge domo ccm.
Hivi aliyechunguza zile trillion 1.5 aliteuliwa na mwenyekiti wa Chama gani?Uchunguzi unaofanywa na aliyeteuliwa na mwenyekiti wa ccm...majibu lazima yawe ni ya kumpendeza aliyemteua..majibu gani hayo yatakuwa ya kumpendeza mwenyekiti wa ccm,stay tune
kikwete hakuteua makada wajumlajumla waccm kushika nyadhfa za juu za vitengo serikalini...but ckuhz mwenyekiti wa ccm amekua akiteua makada kutoka chama chake..hao makada ndo mnataka wakawakague chadema???Hivi aliyechunguza zile trillion 1.5 aliteuliwa na mwenyekiti wa Chama gani?
Sent using Jamii Forums mobile app
We una akili timamu?
Inashangaza. Nilitarajia TAKUKURU waingie kazini baada ya ripoti ya CAG kuonyesha kuna hitilafu.Kwa hiyo TAKUKURU wameamua kufanya kazi ya CAG?