TAKUKURU yaanza kuichunguza CHADEMA kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

TAKUKURU yaanza kuichunguza CHADEMA kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Kapeleke hoja bungeni si mnaowawakilishi
Ndo Yale yalee!

Kaa kwenye hoja mkuu, la kama unaona uchungu tafuta kamba jitundike, Mzee atazaa watoto wengine,

Kila taasisi, kila mahali ambapo hapaeleweki kuhusu matumizi ya Fedha za walala Hoi patachunguzwa,

Zamu iliyopo sasa ni Chama kinachopianiwa na wanachama wake kuwa ni Safi!!! Ndiyo kipo kwenye zamu ya uchunguzi wa Takukuru na huwezi kuwapangia

Shida iko wapi mkuu
 
Wewe mwenyewe mchafu jichunguze wewe kwanza ukiwa msafi ndipo unaanza kuwachunguza wengine waanze na kivuko cha Dsm Bagamoyo bilion 12 za Ndungai, bilion 251 wizara ya ujenzi na zingine nyingi huko CCM kwanza kabla hawajaenda popote
😂
Mkuu, Mimi hata nikiwa mchafu nachafukwa na Mali zangu binafs, namshukuru Mungu ktk Hilo, Mimi ninauhuru wa nitumie nini na Kwa kiasi gani leo, sina kizuizi

Ila hao tuliowaamini wanapoanza kutugeuka, tunalipa Kodi bafala ya kutumika kama inavyopasa, Wao wanaanzisha Miradi ya Matrecta na mashamba huko Ifakara, wanajinunulia magari kupitia migongo ya Vyama vyao, hao ndio wanaorudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu

Hatuwezi kuwa nchi ya hovyo kiasi hicho, ni Bora kabisa tusiwe na viongozi, maana viongozi waizi hatuwataki popote pale
 
  • Thanks
Reactions: mmh
TRA pia wadai Chao kwa Mbowe kwakinachoitwa walikilikopesha chama kwa riba.Je Mbowe kasajiliwa benki kuu akapewa leseni ya kuendesha biashara ya mikopo? Wote wanaosema walikopesha chadema kwa RIba TRA na BOT washukieni Kama mwewe.TRA daini chenu na malimbikizo ya Kodi ya hiyo riba

Na msajili wa makampuni awe shahidi Kama aliwapa leseni ya kukopesha hao wanaosema walikopesha chadema
Huu ujinga bakia nao kwanza elezea zipo wapi bilion 12 alizochukua Ndungai kabla hatujauliza 10% ununuzi wa Ndege na miradi mingine
 
CAG alidanganywa kuna deni la chama linalipwa. Kumbe ni deni hewa ambalo mmiliki wa Chadema alijitengenezea. Acha Pccb wapate ukweli alafu watu waende lupango.
Ahahahaaaa [emoji3][emoji23][emoji1787]. Umeshabikia na hili ?! Mahojiano ya kina Lugora na pccb yalikomea wapi ?!.
 
TRA pia wadai Chao kwa Mbowe kwakinachoitwa walikilikopesha chama kwa riba.Je Mbowe kasajiliwa benki kuu akapewa leseni ya kuendesha biashara ya mikopo? Wote wanaosema walikopesha chadema kwa RIba TRA na BOT washukieni Kama mwewe.TRA daini chenu na malimbikizo ya Kodi ya hiyo riba

Na msajili wa makampuni awe shahidi Kama aliwapa leseni ya kukopesha hao wanaosema walikopesha chadema
Kabisa anakopesha wasiokopesheka anajilipa ndani kwa ndani
 
Kwamba Mashinji huyu anayesusiwa salamu na akina Halima atahojiwa kuhusu chama cha akina Halima.

Kama hakuna upigaji ni vizuri au huo upigaji umhusu Mashinji pia tofauti na hapo hana sababu ya kutokuwachomea!
Mashinji ni key witness. Maana alishuhudi ulaghai ukifanyika.
 
Wewe mwenyewe mchafu jichunguze wewe kwanza ukiwa msafi ndipo unaanza kuwachunguza wengine waanze na kivuko cha Dsm Bagamoyo bilion 12 za Ndungai, bilion 251 wizara ya ujenzi na zingine nyingi huko CCM kwanza kabla hawajaenda popote
Unalinganisha serkali na chama
 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imeanza kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, inazokikabili Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo, kuna matumizi mabaya ya fedha za michango ya wanachama, ambayo kwa mujibu wa katiba yao wanadai imeanishwa wachangie.”

“Lakini, matumizi yake ndio wanatilia mashaka, kuna fedha nyingi zinatumika ndivyo sivyo, kwa mujibu wa makubaliano yao,” amesema Jenerali Mbungo.

“Kwa hiyo, tunachunguza matumizi yasiyo sahihi ya fedha zao, Takukuru inayomamlaka ya kuchunguza taasisi yoyote iwe ya umma, watu binafsi, chama, klabu, iwe chochote Takukuru wanaingia kufanya uchunguzi, ilimradi kuwe na ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha na rushwa,” amesema bosi huyo wa Takukuru.

Mbungo amewataja baadhi ya watakaohojiwa ni; Dk. Vincent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema, ambaye kwa sasa amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM), John Mrema, Mkurugenzi wa Itifaki na Mambo ya Nje Chadema, pamoja na mhasibu mkuu wa chama hicho, Dk. Roderick Lutembeka.

Aidha, Jenerali Mbungo amesema wameshindwa kumhoji Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuhusu sakata hilo, kwa kuwa aliieleza TAKUKURU kwamba yuko nje ya jiji la Dar es Salaam.

Amesema, taasisi hiyo imeshaanza kukusanya nyaraka mbalimbali, zinazohusiana na tuhuma hizo.

“Tumeshapata nyaraka kutoka sehemu mbalimbali, wametupatia nyaraka, wamekuwa wanatoa ushirikiano katika hili,” amesema Mbungo.

Jumamosi ya tarehe 23 Mei 2020, Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, alikanusha tuhuma hizo, akisema kwamba, hakuna uthibitisho unaoonesha chama hicho kina matumizi mabaya ya fedha.

Kigaila alisema, fedha za michango ya wabunge na zinazotoka kwa wadau wengine wa Chadema, matumizi yake hupangwa na vikao vyake vya chama, wakati bajeti ya matumizi hayo ikipitishwa na baraza kuu, kisha taarifa zake hutolewa na kamati kuu ya chama hicho.

Kigaila alisema, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hukagua taarifa za matumizi ya Chadema, na kwamba kwa mujibu wa ukaguzi huo, hakuna ushahidi kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.
Tunaamini ataifanyia kazi hata ile ripoti ya ufujaji wa fedha na mali za CCM. Ripoti hii alihusika kuchunguza na kuandika ndugu yetu Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally. Tunaamini hata mambo yale ya Mkuu wa wilaya ya Hai nayo yatachunguzwa tu. Hapo tutaona anatenda haki kweli kweli.
 
Hujui kazi ya CAG na TAKUKURU hizi shutma zinaukweli naona woga sana
Kama CAG alishafanya ukaguzi na ikaonekana hakuna ubadhilifu, TAKUKURU wanaingiaje hapo?
Kwani kuna tuhuma za rushwa ndani ya chama cha CHADEMA mpaka hii taasisi ifanye uchunguzi?
Naomba tueleweshane kama hizi taasisi mbili zinaingiliana kimajukumu.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
TRA pia wadai Chao kwa Mbowe kwakinachoitwa walikilikopesha chama kwa riba.Je Mbowe kasajiliwa benki kuu akapewa leseni ya kuendesha biashara ya mikopo? Wote wanaosema walikopesha chadema kwa RIba TRA na BOT washukieni Kama mwewe.TRA daini chenu na malimbikizo ya Kodi ya hiyo riba

Na msajili wa makampuni awe shahidi Kama aliwapa leseni ya kukopesha hao wanaosema walikopesha chadema
Lazima tukubali takukuru ni genge la ccm ule ushahidi wakina nasari na hizi kelele za wakina lijualikali zinatofauti gani? Badala ya kumsulubu mwizi wa fedha za umma kangi lugola wameachia huko kwa kuwa ni mwanachama mwenzao
 
😂
Mkuu, Mimi hata nikiwa mchafu nachafukwa na Mali zangu binafs, namshukuru Mungu ktk Hilo, Mimi ninauhuru wa nitumie nini na Kwa kiasi gani leo, sina kizuizi

Ila hao tuliowaamini wanapoanza kutugeuka, tunalipa Kodi bafala ya kutumika kama inavyopasa, Wao wanaanzisha Miradi ya Matrecta na mashamba huko Ifakara, wanajinunulia magari kupitia migongo ya Vyama vyao, hao ndio wanaorudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu

Hatuwezi kuwa nchi ya hovyo kiasi hicho, ni Bora kabisa tusiwe na viongozi, maana viongozi waizi hatuwataki popote pale
Kuwa Nchi ya hovyo ni pamoja na kutafuna bilion 12 na Ndungai ni Taifa lipi Duniani wamewahi kutumia pesa nyingi kiasi hicho kwa matibabu ya mtu mmoja?
 
Back
Top Bottom