Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Punguza hasira tafuta helaHapa inaonekana Kuna makubaliano halali yalifanyika kati ya GSM na Makonda kuhusu ununuzi wa kiwanja.Na yalifanyika wakati Makonda Ni mkuu wa mkoa.Sasa GSM amegeuka hayo makubaliano.Anaanza uongo.GSM anashirikiana na Ridhiwani Kikwete kudanganya umma.GSM inaonekana hana elimu .
Hawawezi washa kiwanda chao maana mapato yatapungua, ile ni bahati mbaya imetokeaGSM ni mwanadamu pia ana udhaifu wake ila kwa historia yao ya ujanja janja kwa hili nakubaliana nawe, huu ni mchezo, na kile kiwanda chao Mwenge wakatia kiberiti kuzidi kuwadanganya wajinga.
tunataka atuoneshe malipo ya kiserikali na sio risitiGSM anadai kafanya mkataba wa ujenzi wa milioni 640 na kampuni ya Group 6 International mnamo mwaka 2016, hapohapo Makonda anadai yeye ndiyo anafanya ujenzi pale unaosimamiwa na mdogo wake tokea 2018 na kanunua kila kitu kwenye eneo hadi AC na vifaa vingine vya ujenzi na risiti anazo. Hapo nani anadanganya?
mbona hueleweki kaka! ebu pitia vizur bandiko lakoWanasheria walishatoa angalizo kuwa, GSM alimuuzia Makonda, na ktk mauziano GSM hakuweka vitu sahihi mfano alihakikisha picha na mihuri tofauti na pia alihakikisha mamlaka zingine hazijaweka sahihi lakini pia GSM alihakikisha anaweka sahihi za uongo na baada ya hapo akatangaza kupotelewa hati. Kwa ufupi GSM ni tapeli.
Namuona mtu akipinduliwapinduliwa mithili ya chips kwenye kikaangioAkifafanua zaidi, Kayera alisema GSM alishatoa taarifa idara ya ardhi kuhusu kupotea kwa hati ya kiwanja hicho, na alipewa nakala ya uthibitisho mwingine.
"Baada ya kutoa taarifa kuwa amepoteza na kwa mujibu wa sheria, ukipoteza hati unaleta taarifa, inatangazwa kwenye gazeti la kawaida, inatolewa certified, kwa mujibu wa kumbukumbu, hatua hizo zilifuatwa, lakini kwa sasa si rahisi kusema nani ni halali," alisema.
hakuna uhuni hapo! uyo bashite ndio kwikwiKwa mtu yeyote mwenye akili akiangalia issue nzima,utagundua tu kulikuwa na makubaliano kati ya hao wawili.Huyu anayejiita GSM ni marafiki wa Kikwete wanaotumia vibaya ,madaraka ya Kikwete Kama Rais msataafu kupora mali za watu.Yaan bongo ,mambo mengi yanaendeshwa kihuni tu.Unaingia mkataba ,baadae utawala umebadilika.Unadai umeibiwa hati.Watu wa aina hii ni hatari Sana.Swali .Kwann GSM aliuza hicho kiwanja?Kwanini amebadilika?Eti Sasa ameibiwa hati.Huo ni uhuni.
GSM wameshapeleka bado mzee wa kolomijeWanachobishana ni kitu simple sana..
Kila mtu apeleke vithibitisho kwenye mamlaka husika... Au kuna ugumu gani hapo????
Au ndio wanataka kumaliza tu muda wa watu.
Hakuna biashara iliyofanyika hapo ila labda makubaliano kwa shingo upande !!Wanachobishana ni kitu simple sana..
Kila mtu apeleke vithibitisho kwenye mamlaka husika... Au kuna ugumu gani hapo????
Au ndio wanataka kumaliza tu muda wa watu.
Serikali imesema inalichunguza sakata la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) la kugombea kiwanja Na.60 kilichopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni jijini hapa.
Akizungumza mwisho wa wiki iliyopita, Wakili wa GSM, Alex Mgongolwa alisema mteja wake ana vielelezo vyote, huku Makonda akimtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mai yake.
Akizungumza jana na Mwananchi kwa simu, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni alisema suala hilo wanalifanyia kazi.
"Uchunguzi upo wa namna nyingi. Na mimi taarifa nimezisikia kupitia vyombo vya habari lakini tunaona kuna kazi ya kufanya katika hilo. Kwa hiyo tumelichukua tunalifanyia kazi," alisema Hamduni.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu uhalali wa vielelezo vya wawili hao, Kamishna wa Ardhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Idrisa Kayera alisema vyombo vya Serikali vinavyochunguza suala hilo.
"Zinachunguzwa (hati) na mamlaka nyingine ili kujua uhalali wao. Sisi tukipata wakishatoa maelekezo tutaendelea na hatua nyingne.
"Kwa mujibu wa utaratibu ni kwamba mtu ukifanya uhamisho anatakiwa awasilishe ofisini, ili ijulikane, lakini hilo tumeziachia mamlaka zifanyie kazi ili kujua," alisema.
Alisisitiza kuwa hizo ni mamlaka za uchunguzi, bila kuzitaja, huku akizitaka pande mbili kwenda kushtaki kwenye vyombo vya Dola.
"Kwa sababu wao wenyewe ndio walihusika kwenye mkataba baina ya Makonda na GSM, wao wapeleke kule, majibu tutaletewa, wakisema hivi vitu havina uhalali tutachukua hatua," alisema.
Akifafanua zaidi, Kayera alisema GSM alishatoa taarifa idara ya ardhi kuhusu kupotea kwa hati ya kiwanja hicho, na alipewa nakala ya uthibitisho mwingine.
"Baada ya kutoa taarifa kuwa amepoteza na kwa mujibu wa sheria, ukipoteza hati unaleta taarifa, inatangazwa kwenye gazeti la kawaida, inatolewa certified, kwa mujibu wa kumbukumbu, hatua hizo zilifuatwa, lakini kwa sasa si rahisi kusema nani ni halali," alisema.
Chanzo: Mwananchi
Hakuna biashara iliyofanyika hapo ila labda makubaliano kwa shingo upande !!
Huwa simpendi tangu alipompiga WariobaBashite ni empty kichwani kabisa, ameshapigwa tayari
GSM wameshapeleka bado mzee wa kolomije