TAKUKURU yaingilia kati sakata la Makonda na GSM. GSM aliripoti hati ya kiwanja kupotea

TAKUKURU yaingilia kati sakata la Makonda na GSM. GSM aliripoti hati ya kiwanja kupotea

Gsm hati ilipotea !!! Makonda aliiba Kama anayo ni Useless wezake wajanja inaonesha walimpa ili ufanyike transferring kulala kwa Mwendazake ndo problem
 
Serikali imesema inalichunguza sakata la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) la kugombea kiwanja Na.60 kilichopo Regent Estate Manispaa ya Kinondoni jijini hapa.

Akizungumza mwisho wa wiki iliyopita, Wakili wa GSM, Alex Mgongolwa alisema mteja wake ana vielelezo vyote, huku Makonda akimtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mai yake.

Akizungumza jana na Mwananchi kwa simu, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni alisema suala hilo wanalifanyia kazi.

"Uchunguzi upo wa namna nyingi. Na mimi taarifa nimezisikia kupitia vyombo vya habari lakini tunaona kuna kazi ya kufanya katika hilo. Kwa hiyo tumelichukua tunalifanyia kazi," alisema Hamduni.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu uhalali wa vielelezo vya wawili hao, Kamishna wa Ardhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Idrisa Kayera alisema vyombo vya Serikali vinavyochunguza suala hilo.

"Zinachunguzwa (hati) na mamlaka nyingine ili kujua uhalali wao. Sisi tukipata wakishatoa maelekezo tutaendelea na hatua nyingne.

"Kwa mujibu wa utaratibu ni kwamba mtu ukifanya uhamisho anatakiwa awasilishe ofisini, ili ijulikane, lakini hilo tumeziachia mamlaka zifanyie kazi ili kujua," alisema.

Alisisitiza kuwa hizo ni mamlaka za uchunguzi, bila kuzitaja, huku akizitaka pande mbili kwenda kushtaki kwenye vyombo vya Dola.

"Kwa sababu wao wenyewe ndio walihusika kwenye mkataba baina ya Makonda na GSM, wao wapeleke kule, majibu tutaletewa, wakisema hivi vitu havina uhalali tutachukua hatua," alisema.

Akifafanua zaidi, Kayera alisema GSM alishatoa taarifa idara ya ardhi kuhusu kupotea kwa hati ya kiwanja hicho, na alipewa nakala ya uthibitisho mwingine.

"Baada ya kutoa taarifa kuwa amepoteza na kwa mujibu wa sheria, ukipoteza hati unaleta taarifa, inatangazwa kwenye gazeti la kawaida, inatolewa certified, kwa mujibu wa kumbukumbu, hatua hizo zilifuatwa, lakini kwa sasa si rahisi kusema nani ni halali," alisema.

Chanzo: Mwananchi
Mimi ningelikuwa Makonda, ningelimuachia kiwanja huyo GSM, kwani GSM ni "dhulumati bingwa" na alifanya udhulumati mkubwa awamu ya nne. Awamu ya Tano ali 'hibernate' na sasa amerudi tena kudhulumu. Vyovyote vile GSM atashinda!
 
Kwa mtu yeyote mwenye akili akiangalia issue nzima,utagundua tu kulikuwa na makubaliano kati ya hao wawili.Huyu anayejiita GSM ni marafiki wa Kikwete wanaotumia vibaya ,madaraka ya Kikwete Kama Rais msataafu kupora mali za watu.Yaan bongo ,mambo mengi yanaendeshwa kihuni tu.Unaingia mkataba ,baadae utawala umebadilika.Unadai umeibiwa hati.Watu wa aina hii ni hatari Sana.Swali .Kwann GSM aliuza hicho kiwanja?Kwanini amebadilika?Eti Sasa ameibiwa hati.Huo ni uhuni.
Hata Makonda nae alitumia vibaya madaraka yake wakati wa hayati Magufuli...nae alipora mali za watu na aliwalazimisha wampe hizo n=mali kwa jina la hayati....atulie tu maana Muosha nae Huoshwa.....ni wakati wao huu GSM kumuosha...
 
Kwa hiyo Mr. Makonda hakuona tangazo la kupotea kwa hati?
Possible ! Wakati wa mwendazake, Paul alikuwa busy akishughulika na mambo mengi
Pili, inawezekana aliona lakini alitumaini ulinzi wa muda mrefu tukijua alikuwa na nguvu sana
Tatu, pengine hakujua kuna leo na kesho

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Makonda aliwezaje kuiba hati ya nyumba? Au GSM aliisahau bar ikaokotwa? GSM anaishi na mateja yalipita nayo? Wacheni kumdhulumu dogo
 
Ukiwasoma watu walioko mamlakani pamoja na kwamba wanasema habari ya UCHUNGUZI kuendelea but kuna key words kadhaa hapo kwa hizo pande zilizo hojiwa is like Makonda kuna sehemu kadhaa kakosea so sitapata TABU kusikia baada ya Uchunguzi kwamba bwana Makonda alivamia kiwanja cha watu, just soma tena, kuna key words kadhaa hapo zinazo ashiria kwamba sheria IPO upande wa mfadhiri wa Yanga zaidi kuliko Makonda
Huenda pia bashite alimpora kinguvu bila matKwa yake( akimtishia usiponipa nakufungulia kesi) enZi hizo mtoto wa rais tena utamnyima hujipendi
 
Hata Makonda nae alitumia vibaya madaraka yake wakati wa hayati Magufuli...nae alipora mali za watu na aliwalazimisha wampe hizo n=mali kwa jina la hayati....atulie tu maana Muosha nae Huoshwa.....ni wakati wao huu GSM kumuosha...
Huyu nahisi wanamtakasa.
 
Nashangaa wote wanaotoa mawazo yao kwenye hii mada wanataka Makonda achunguzwe alipata wapi fedha za kununua kiwanja sijasikia hata mmoja akisema huyo GSM achunguzwe alipata wapi hizo fedha za kununua kiwanja au nyie wote ni Yanga? Juzi hapa huyo GSM ameingiza malori mapya kama mwenda wazimu wala hakuna anayestuka au kuuliza au kwa sababu ya rangi yake? Sakala hili la Makonda mwenye akili atafahamu nani yupo nyuma ya hili sakata kuna jamaa alichukia Makonda kuhama kambi yake na kujiunga na kambi ya JPM na hii kazi aliyofanya ya kuwataja wauza unga baadhi wakiwa ni wa kambi ya huyo kigogo imesababisha. Hata huyo aliyefungua kesi ya kumshitaki Makonda inajulikana nani amefadhili fedha za kuendesha kesi. Hili la kiwanja kuna jamaa anahusika kwa njia fulani amefanyaje utakuja kusikia.Tusubiri muda utaongea lakini Tanganyika ya sasa ni ya watu kukomoana tusipoangalia watu wataanza kupoteza maisha kirahisi.
 
Kuhusu maroli ya gsm hata wewe mkinga unaweza kuingiza 100 ni conection tu hatuziju wanatumia dhamana na kupewa mikopo kazi kwako kusimamia hayo maroli card zinabaki kwao mpaka utakapo maliza deni wajanja wa zamani waliifanya sana kutumia Karadha
 
Huenda pia bashite alimpora kinguvu bila matKwa yake( akimtishia usiponipa nakufungulia kesi) enZi hizo mtoto wa rais tena utamnyima hujipendi
Na liwe fundisho kwa vijana wengine; usizurumu cha MTU kwa kumtegemea mtu, sponsor huaga anakufa; ni binadamu
 
Nashangaa wote wanaotoa mawazo yao kwenye hii mada wanataka Makonda achunguzwe alipata wapi fedha za kununua kiwanja sijasikia hata mmoja akisema huyo GSM achunguzwe alipata wapi hizo fedha za kununua kiwanja au nyie wote ni Yanga? Juzi hapa huyo GSM ameingiza malori mapya kama mwenda wazimu wala hakuna anayestuka au kuuliza au kwa sababu ya rangi yake? Sakala hili la Makonda mwenye akili atafahamu nani yupo nyuma ya hili sakata kuna jamaa alichukia Makonda kuhama kambi yake na kujiunga na kambi ya JPM na hii kazi aliyofanya ya kuwataja wauza unga baadhi wakiwa ni wa kambi ya huyo kigogo imesababisha. Hata huyo aliyefungua kesi ya kumshitaki Makonda inajulikana nani amefadhili fedha za kuendesha kesi. Hili la kiwanja kuna jamaa anahusika kwa njia fulani amefanyaje utakuja kusikia.Tusubiri muda utaongea lakini Tanganyika ya sasa ni ya watu kukomoana tusipoangalia watu wataanza kupoteza maisha kirahisi.
Mkuu jitahidi uisumbue akili yako utakuja kugundua kwamba kuagiza magari hata 500 kwa matajiri inawezekana sana tu; nina wafahamu watu kadhaa walipewa tenda fulani, tena wakapewa na muda wa kujiandaa kama miezi 3 hivi, na hawakua na uwezo kiviile kumudu hiyo TENDA, ndani ya hiyo miezi 3 walileta mabasi mapya zaidi ya 25, hadi sasa ni matajiri wa kutupwa. Issue ni wewe kuifahamu dunia vizuri; ni wewe tu ndio unalishangaa hilo la GSM kuleta malori zaidi ya 100, sio AJABU mkuu
 
Kwa mtu yeyote mwenye akili akiangalia issue nzima,utagundua tu kulikuwa na makubaliano kati ya hao wawili.Huyu anayejiita GSM ni marafiki wa Kikwete wanaotumia vibaya ,madaraka ya Kikwete Kama Rais msataafu kupora mali za watu.Yaan bongo ,mambo mengi yanaendeshwa kihuni tu.Unaingia mkataba ,baadae utawala umebadilika.Unadai umeibiwa hati.Watu wa aina hii ni hatari Sana.Swali .Kwann GSM aliuza hicho kiwanja?Kwanini amebadilika?Eti Sasa ameibiwa hati.Huo ni uhuni.
Binafsi nakubaliana na wewe kabisa lakini na wewe umeamua kua na UPANDE; umechagua kua upande wa Makonda; na wewe unaamini kwamba Makonda angeweza kununua kiwanja kwa Tsh 120M mwaka 2013? Miaka hiyo huyu dogo si alikua anapanda bodaboda kama sisi tu, hiyo pesa alipata wapi? Hilo moja, la pili; hivi enzi za Mwendazake dogo akiwa mkuu wa mkoa wa Dar, kuna kitu angekitaka Makonda akashindwa kukipata? Huyu hata jina lake tu ilikuja kudhihirika kua sio hilo, anaitwa vingine kabisa, watu wakaotoa na USHAHIDI lakini mkuu alimlinda; unataka kunambia hili nalo hulijui au umesahau? Siku nyingine usije ukamzurumu mjanja mwenzio ambaye (kwa mtazamo wako kwamba GSM nae ni zurumati) anajua namna zote za kuzurumu, utapoteza mkuu!
 
Makonda kabaki yatima ,sponser wake kashaenda na maji.Sasa apambane na hali yake hana wa kumlilia.

Hili ni fundisho kwa vijana wengine wanaopewa madaraka na kuanza kuwavimbia watu hususani matajiri na viongozi wastaafu.

Bado huyo dogo Ally papi alitoa shits sana enzi za mwenda zake.

Ally Hapi aliniumiza moyo alivyotukana wastaafu watulie waache kuwashwa washwa alimaanisha JK

Mh Raisi kula kichwa Ally Hapi Hana adabu
 
Ally Hapi aliniumiza moyo alivyotukana wastaafu watulie waache kuwashwa washwa alimaanisha JK

Mh Raisi kula kichwa Ally Hapi Hana adabu
Hii kauli aliitoa mwingine sio huyo.
 
Back
Top Bottom