Botha, aliyekuwa rais wa Afrika Kusini,aliwahi kusema
' The most intelligent black African can not think beyond one year"
Mwafrika anapofikiri jambo anawaza matokeo ya papo kwa papo au anatafuta sifa za muda mfupi na kupigiwa makofi.
Falsafa ya Mwalimu Nyerere kuhusu Elimu ilikua bora sana na ya kiwango cha pekee Duniani.
Mwalimu alikuwa hatumii pesa za Serikali kumwelimisha Mtoto ambaye baadaye anakuwa hana tija kwa Taifa.
Kusomesha Mtoto ni uwekezaji. Uwekezaji wowote ni lazima urudishe pesa iliyowekezwa na ziada.
Tunatumia pesa nyingi kutoa elimu duni kwa watoto na kusababisha tusipate mrejesho wa uwekezaji wetu.
Nyerere alimsomesha Mtoto kwa kulingana na karama za Mtoto kuanzia shule za msingi.
Kila aliyesomeshwa alitumika kikamilifu kulingana na karama zake.
Waliokuwa na karama za utawala, siasa, jeshi, Sayansi n.k waliandaliwa kuanzia shule za msingi.
Wanafunzi wa Kitanzania waliokuwa wanaenda Ng'ambo kusoma masomo ya juu walikuwa na uelewa mkubwa na wazungu walikuwa wanashangaa kuona Watanzania kuwa na akili nyingi.
Sasa hivyo vipaji hivyo havijitokezi kwa sababu ya maandalizi mabovu.