Takwimu za Kibu D Vs Mayele zinatia uchungu

Takwimu za Kibu D Vs Mayele zinatia uchungu

Mara ya mwisho Kibu D kufunga sidhani kama tulikua tumesha hesabiwa waTz
JamiiForums-1049870428.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka muda huu matokeo yaliyopatikana ni haya hapa:-

Kibu D aka Kibudenga magoli 0

Mayele Kalala Fiston magoli 8.

Hivyo naomba kuchukua nafasi hii kumpa tu Kibu Denis aka Kibudenga ushindi wa mezani. Maana nguvu na uwezo wa kushindana na Fiston Mayele, kwakweli hana.
Ligi bado mbichi Mkuu tusimalize maneno yote tuweke na reserve
 
#THROWBACK

1- KINDOKI..
2- PAUL GODFREY.
3- MASHOTO..
4- DANTE
5- YONDAN..
6- TSHIMBI..
7- NGASA
8- MAKA EDWAD..
9- MAKAMBO..
10 - AJIBU..
11- MOLINGA..

Yanga mbovu kuwahi kutokea tangu Tanganyika iwe Tanzania..
Lawama kila siku kwa waamuzi na TFF.. Wachezaji waligoma kila uchwao.. Maisha magumu, watumishi wa hii taasisi kubwa Tanzania na Afrika walikopwa mishahara yao. Ikafika hatua bakuli likatembezwa ili kupatikane chochote kitu.

Club kila mechi ina jezi mpya, watu walichuma pesa kupitia nembo ya Yanga SC.. Uhuni, umafia ulitumika kuchuma pesa za watu wenye mapenzi wa timu yao. Lakini baadaye nuru ikaangaza gizani, mvua ikanyesha kwenye ukame. Mbazi ikamea jangwani.
Timu ikajengwa zaidi ya mara tatu ikawa ina bomoka.. Wachezaji wa buku jero wasio na hadhi wakaondolewa. Mwiko kukata tamaa.. Hivi sasa hakuna hakuna timu inayo tamani kukutana na Yanga wala hakuna mchezaji asiye penda kucheza Yanga.
Adui akikushinda ungana naye, porojo za kwamba Yanga ananunua mechi hazito kusaidia chochote. wachezaji aina ya Kibu Denis hawawezi kukupa ubingwa.
Utaishia kulia lia huku wahuni wakiendelea kugonga mvinyo kwenye timu yenu. Siku mtakuja kukumbuka shuka kumekucha wakati huo Yanga wana makombe 60 kabatini na makombe matatu ya kimataifa.

Kalaga baho..
 
Back
Top Bottom