Hizi takwimu zipo sahihi, ila unachosahau ni kitu kimoja mtani, mambo ya msimu sio sawa na ya msimu uliopita.
Msimu uliopita round ya kwanza, Yanga walikuwa unbeaten lakini ulikuwa ukiangalia uchezaji wao wala haukuwa na mipango. Magoli hayakuwa ya kutengenezwa. Msimu huu japo ni mapema sana, ila dalili zinaonekanaga asubuhi. Yanga pasi wanapiga, magoli wanafunga, beki zinakaba na kumlinda kipa vizuri.
Tukiwaangalia watani wetu, nyie ndio mmekuwa kama Yanga ya msimu uliopita, matokeo mnapata ila kwa jasho sana. Tuweke ushabiki pembeni katika ili mtani.
Yanga wamesajili wachezaji wengi, lakini wamezingatia sana mahitaji yao uwanjani. Wameondoa wachezaji wengi, na wamekuwa replaced na wengi.
Simba mmesajili wachezaji wengi lakini sidhani kama mliangalia mashimo au uhitaji wenu. Wameondoka Chama, Miquison na Chikwende, lakini mliowaleta ni wengi mno as if viongozi walikuwa wanajaribu kuwalidhisha mashabiki badala ya kuangalia uhitaji.
Wawa, Nyoni, Onyango, Kagere na Boko hawa wote hawatakiwi kucheza dakika 90 kama ilivyokuwa hapo hawali. Walau Onyango ni mzee lakini anajituma sana uwanjani, ila hao waliobaki wakipigiwa pass mbali na walipo, hawajisumbui kukimbia. Wawa anakabia macho, Boko anasimama sana uwanjani.
Mtani unajaribu kuficha madhaifu ya timu yako kwa kuangalia takwimu za mwaka jana. Basi ili kujisaidia, chukua takwimu zenu za mwaka jana pia alaf zilinganishe na mwaka huu, hapo utaona wazi msimu kuna tofauti sana.