Kitendo cha kusema vitabu vya dini kuwa vipo sawa muda wate na havipitwi na wakati kwenye baadhi ya mambo ni uongo
Kuna baadhi ya aya kwenye vitabu viliwakilisha mila na desturi za watu wa maeneo ambayo dini husika ilianzia na kwa nyakati zile za kizamani na hsikumaanisha kuwa ni Maelekezo wala maneno ya Mungu.
Suala la mavazi, kanzu kwa wakristu na waislamu hilo ni vazi la kawaida tuu kwa sehemu ambapo imani hizo zilianzia hazimaanishi kuwa ni amrisho la Mungu tuzae hivyo
Suala la mikate ilinayotumika kwenye biblia, suala la tende kwa waislam, divai kwa wakristu hivyo vyote ni vyakula na vinywaji vya asili vya sehemu dini hizo zilizoanzia na haimaanishi tukiviiga tutakuwa karibu na Mungu hapana , madhalani dini hizi zingeanzia Tanzania ungekuta maneno ya vyakula kama ugali, mlenda, makane nk na vinywaji kama togwa , mbege ulanzi nk
Suala la haki za mwanamke lilivyoandikwa kwenye vitabu hivi kweli ni kandamizi kabisaa hata kama atakuja mtafsiri na kusema kuna haki ni uongo, vitabu hivi kiasili viliendana na mila na desturi za jamii hizo na kwa wskati huo mwanamke alikuwa ni second degree human being na sio first kama mwanaume na wakati mwingine alionekana sio binaadamu bali kama mali ya mwanaume
Lakini kwa sasa dunia imebadilika, tayari wamejua haki zao hata wakifungiwa ndani ni sawa na kuzuia mafuriko kwa mikono kuna social media wataibuka tuu
Kutegemea vitabu vya dini viwe ndio statute za kuongoza nchi wakati havina kipengele cha ammendment kwenye nyakati hizi za technology na information ni uongo