Pre GE2025 Tamaa ya Tundu Antipas Lissu, Kuutaka uwenyekiti wa CHADEMA taifa ni utashi wake binafsi au shinikizo kutoka nje ya nchi kwa wanao mbackup!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Chairman wa sasa wa Chadema Taifa, Freeman Aikaeli Mbowe, akizungumzia kusudio la Tundu Antipas Mughwai Lisu kugombea uenyekiti wa Chadema Taifa, kwa namna yoyote ile atakua ameingia kwenye trap au mtego wa kisayansi alotegwa na kukoleza au kuzidisha joto, uhasama na vita ya madaraka ndani ya chadema hususani dhidi ya nafasi ya uenyekiti wa Chadema Taifa.

Tundu Lisu akijibiwa azma yake hiyo na chairman Freeman Mbowe, atakua amefanikiwa kumuingiza mbowe mtegoni, na ndipo sasa mambo na madudu mengine mazito zaidi na muhimu sana dhidi ya chairman Mbowe yataibuliwa na kuwekwa hadharini.

Na hilo ndilo lengo hasa la Tundu Lisu. Na huo ndio utakua mwanzo wa safari ya kujiengua chadema na kuelekea kwingineko kula maisha au kupata nafasi na fursa ya kugombea urasi uchaguzi mkuu ujao Oct 2025, endapo hoja na tuhuma zake dhidi ya chairman Mbowe zitapanguliwa kwa ufasaha.

Nadhani Tundu Lisu ana mambo mengi mno moyoni dhidi ya uongozi wa chadema Taifa, hata hivyo, mpaka kufikia uamuzi wa kutaka awe mwenyekiti wa Chadema Taifa. Tundu Antipas Mughwai Lisu, anahitaji mambo mawili tu kwenye vita hii. Ni awe mwenyekiti wa Chadema Taifa, au kujiengua chadema na kutafuta fursa za kisiasa kwenye vyama vingine vya siasa nchini.

Na hili linaweza kua ni shinikizo kutoka nje ya nchi, hasa kutoka kwa wale wanao wanaombackup yeye na familia yake huko ughaibuni. Ni dhahiri awali alionekana hayupo serious.

Kukaa kimya kwa Freeman Aikaeli Mbowe, kutampasua kichwa na kutamdhoofisha sana Tundu Lisu anaetamani majibizano, na hapo mbowe atakua ameupiga mwingi zaidi, akiendelea na harakati zake za kutetea kiti chake cha uenyekiti wa Chadema Taifa, kadiri ya mipango mikakati yake na ratiba zake, bila kumzungumzia Lisu hata kidogo.

Kwa kufanya hivi, Freeman Mbowe atakua amemkwaza Lisu, na kumlazimisha amchokonoe zaidi zaidi au kujaribu kupaint uongozi wa Mbowe kama kitu ambacho kiliidumaza chadema na kwamba uongozi wake uligubikwa na sintofahamu nyingi sana.

Na Mbowe akiendelea kukaa kimya zaidi bila kujibu chochote, atakua amemchanganya zaidi Lisu na kumjaza hofu ambayo itamfanya atathmini upya mpango na mtego wake huu wa kumchefua chairman Mbowe ili eti yeye aonekane bora zaidi.

Kiufupi,
katika mpambano na mgawanyiko huu ndani ya chadema, kama wadau wa bobevu, tunajifunza na tutabaini wazi nani miongoni mwa mafahali hawa wawili ndani ya chadema, anatumia sayansi ya siasa kufanya siasa na nani anatumia mihemko, chuki na kukurupuka katika kutafuta uongozi wa kisiasa ndani ya chadema.

Unadhani ni nani aliemshinikiza Lisu kuachana na kugombea umakamu mwenyekiti wa Chadema Taifa, na kuamua kumendea uenyekiti wa Chadema Taifa?

Je, ni shinikizo kutoka ndani ya nchi au nje ya nchi?🐒

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Mbowe akiendelea kung'ang'ania kiti atazidi kupoteza credibility yake.

Siasa ni mahesabu, ni game of attractions, kwa sasa mwenye amsha amsha na anayependwa mtaani ni Lissu.

Wakimpa Lissu CHADEMA itajipatia uhai mpya ambao unaweza kuing'oa Kijani mwakani.

Kijani mkimuweka mama kama mgombea na Lissu awe ndiyo mwenyekiti, basi tegemeeni yasiyowezekana.
 
Korido za Lumumba mnahaha sana
 
Gentleman,
kwanini chairman Mbowe apoteze credibility?

Ni kweli politics is all about numbers,
kwani mwenyekiti wa Chadema Taifa anachagiliwa na wajumbe au na amshaamsha ya mtaani?🐒
 
Korido za Lumumba mnahaha sana
Gentleman,
Yapo mambo muhimu sana kujifunza

kwanza,
ni muhimu kujifunza kwenye hili, Je, ni tamaa au shinikizo la nje, Lisu kuacha kugombea umakamu mwenyekiti na kuutaka uenyekiti Taifa?

Jambo la pili,
Ni muhimu sana kujifunza, kati ya mafahali hawa wawili nani anatumia sayansi ya siasa na nani mkurupukaji katika kufikia azma zao za kisiasa?

Jambo la meisho,
makasiriko si muhimu sana kwenye hoja hii ya maana mno asubuhi hii, kua muungwana 🐒
 
Haiwezekani kuing'oa CCM madarakani kwa vyama hivi vya wachumia tumbo,
Concern ya Lissu ni namna ya kuwa na access na Ruzuku ya Chama basi, hana
uzalendo wowote, Mbowe yupo kimkakati kabisa, iwe jua iwe mvua hawezi kuachia kiti, Lissu ataondoka Chadema kwa aibu kubwa kwa kuonekana anatumika na upande wa pili. Mbowe kashalipwa mahela yake na serikali ya CCM, hana shida ndio maana hata wakati wa maridhiano Mbowe alikuwa anaenda mwenyewe kwenye vikao tofauti na vyama vingine kama ACT WAZALENDO, CUF
 

Yani tangu jana kila chawa anaanzisha angalau uzi mmoja au zaidi kwa siku na vijihoja vyake ishakuwa "ntoke vipi yani" mmepandishiwa dau nini?
 
Tundu Lissu Hana tamaa, ni haki yake ya msingi na kikatiba kugombea nafasi yoyote aitakayo ndani ya chama
 

Safi sana, lete ushahidi chaaap! Otherwise ni uchawi kama mwingine tu
 
Tundu Lissu Hana tamaa, ni haki yake ya msingi na kikatiba kugombea nafasi yoyote aitakayo ndani ya chama
Anajua lakin anachotaka?
umakamu mwenyekiti au uenyekiti Taifa au vyote kwa pamoja?

sio tamaa na shinikizo la mabwenyenye ya magharibi yanayombackup kama kibaraka wao Africa kwa mgongo wa Chadema Tanzania,kweli?🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…