Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Chairman wa sasa wa Chadema Taifa, Freeman Aikaeli Mbowe, akizungumzia kusudio la Tundu Antipas Mughwai Lisu kugombea uenyekiti wa Chadema Taifa, kwa namna yoyote ile atakua ameingia kwenye trap au mtego wa kisayansi alotegwa na kukoleza au kuzidisha joto, uhasama na vita ya madaraka ndani ya chadema hususani dhidi ya nafasi ya uenyekiti wa Chadema Taifa.
Tundu Lisu akijibiwa azma yake hiyo na chairman Freeman Mbowe, atakua amefanikiwa kumuingiza mbowe mtegoni, na ndipo sasa mambo na madudu mengine mazito zaidi na muhimu sana dhidi ya chairman Mbowe yataibuliwa na kuwekwa hadharini.
Na hilo ndilo lengo hasa la Tundu Lisu. Na huo ndio utakua mwanzo wa safari ya kujiengua chadema na kuelekea kwingineko kula maisha au kupata nafasi na fursa ya kugombea urasi uchaguzi mkuu ujao Oct 2025, endapo hoja na tuhuma zake dhidi ya chairman Mbowe zitapanguliwa kwa ufasaha.
Nadhani Tundu Lisu ana mambo mengi mno moyoni dhidi ya uongozi wa chadema Taifa, hata hivyo, mpaka kufikia uamuzi wa kutaka awe mwenyekiti wa Chadema Taifa. Tundu Antipas Mughwai Lisu, anahitaji mambo mawili tu kwenye vita hii. Ni awe mwenyekiti wa Chadema Taifa, au kujiengua chadema na kutafuta fursa za kisiasa kwenye vyama vingine vya siasa nchini.
Na hili linaweza kua ni shinikizo kutoka nje ya nchi, hasa kutoka kwa wale wanao wanaombackup yeye na familia yake huko ughaibuni. Ni dhahiri awali alionekana hayupo serious.
Kukaa kimya kwa Freeman Aikaeli Mbowe, kutampasua kichwa na kutamdhoofisha sana Tundu Lisu anaetamani majibizano, na hapo mbowe atakua ameupiga mwingi zaidi, akiendelea na harakati zake za kutetea kiti chake cha uenyekiti wa Chadema Taifa, kadiri ya mipango mikakati yake na ratiba zake, bila kumzungumzia Lisu hata kidogo.
Kwa kufanya hivi, Freeman Mbowe atakua amemkwaza Lisu, na kumlazimisha amchokonoe zaidi zaidi au kujaribu kupaint uongozi wa Mbowe kama kitu ambacho kiliidumaza chadema na kwamba uongozi wake uligubikwa na sintofahamu nyingi sana.
Na Mbowe akiendelea kukaa kimya zaidi bila kujibu chochote, atakua amemchanganya zaidi Lisu na kumjaza hofu ambayo itamfanya atathmini upya mpango na mtego wake huu wa kumchefua chairman Mbowe ili eti yeye aonekane bora zaidi.
Kiufupi,
katika mpambano na mgawanyiko huu ndani ya chadema, kama wadau wa bobevu, tunajifunza na tutabaini wazi nani miongoni mwa mafahali hawa wawili ndani ya chadema, anatumia sayansi ya siasa kufanya siasa na nani anatumia mihemko, chuki na kukurupuka katika kutafuta uongozi wa kisiasa ndani ya chadema.
Unadhani ni nani aliemshinikiza Lisu kuachana na kugombea umakamu mwenyekiti wa Chadema Taifa, na kuamua kumendea uenyekiti wa Chadema Taifa?
Je, ni shinikizo kutoka ndani ya nchi au nje ya nchi?🐒
Mungu Ibariki Tanzania.