Tambiko la Wanyaturu kwa gari la Lissu, wahusika bora wajitokeze

Nina mpango wa kumuona huyu nabii anaejiita kiboko ya wachawi ili anitabirie kuhusu kifo cha JPM, kama kuna mkono wa mtu, wapukutike mmoja baada ya nwingine.
 
W
Wengi sana tutashuhudia wakipagawa wao na familia zao.
Waliohusika na shambulio lile ni makomandoo waliokuwa wanaitwa task force hawa wanawalinda viongozi kwakuwa hawana kazi za kufanya huko jeshini baada ya mafunzo. wanachukuliwa kama slaha tu. watu hawa ni hatari kwakuwa hutembea na silaha zadi ya moja kwa wakati mmoja
 
Mtu mzima na akili zake haandiki upuuzi kama huo, hata kuita kijana nimemkweza ningeita mtoto tuu.
Jiheshimu kama ninavyo kuheshimu
Siwezi kukuambia maneno ya kukuudhi hata uniambie nini
Sio wewe bali kila mmoja humu
Have a lovely day
Respect
 
Ohoooooo!!
 
Huu ni uongo. Wangekua na nia wasingesubiri gari lirudi.

Miaka ya 90 kijijini kwetu vijana walimpiga na kumkatili uhai kijana wa kijiji kingine aliyekua anakatiza kijijini kwetu usiku. Kipindi hicho umeme hakuna, wale vijana walimhisi yule ni mwizi wa mifugo.

Asubuhi yake Baba yake kijana akafika kijijini akaenda kwa mwenyekiti akatoa tangazo kwamba aliyeshiriki ajitokeze amuombe msamaha. Watu wakapiga kimya.

Mchana baba mtu akaenda pale mwili wa mtoto ulipokutwa akachota mchanga akaondoka. Jioni yake matunda tukayaona.

Alichofanya anajua yeye huko kwao ila ile show mnaicheza ukoo mzima. Yaani aliyeshiriki mauti inamuanzia yeye na ukoo unafuata.

Misiba double double kijijini usiku huo huo mwenyekiti, wazazi wa vijana na vijana waliobaki wakaenda hicho kijiji kwenda kumuomba msamaha yule mzee. Wakatengeneza pombe wakarudi kuimwaga pale ulipokutwa mwili hakuna aliyekufa tena ila binamu yangu hawezi kuzalisha mpaka leo na wanahusisha hiyo ishu na hilo tukio.
 
Huo unaozungumzia ni uchawi. Sisi tunazungumzia tambiko. Jaribu kuelewa na kama ni ngumu basi omba msaada wa jirani akueleweshe
 
Kwa jicho la ujasusi nasubiria utekezaji uanze. Hakuna bahati mbaya kwenye ulingo wa siasa.
 
Tambiko? Excuse me!
Kama "utaalam" huo upo, why not!

Kwanza ndio tutashuhudia ambayo husimuliwa tu.

Watu wamepewa nafasi ya kutosha kujutia, wakakaza shingo, nini tena kifanyike?

Hata kama ni mbwembwe tu za kijadi, acha wahusika wapate moto matumboni mwao.
Kila wakiguswa na unyasi sasa watafikiri wamegongwa na nyoka! Maisha ya namna hiyo usifikiri ni ya raha.
 
Pakupeleka mashtaka ni kwa Mungu tu ,sio kwa wazee wala wajukuu wa wazee wa mi
 
Kweli lile tukio ni la kinyama ila kama haki imeshindikana kupatikana kupitia vyombo vya dola tunyooshe mikono basi, haya mambo mengine sio.

Tambiko? Excuse me!
Nice Tumwachie Mungu tu aisee.
 
Umesema kweli kabisa. Zaidi hiyo ni vita ya kisaikolojia, wasidhani wale wanao muita Pengo na Mwamposa ofisi wawaombee wanateseka na nini zaidi ya fikra hizohizo kuwa kuna hatari yaja.
Hakuna mateso mabaya kama hayo ya kila ukiguswa na unyasi unataharuki kuwa nyoka kakugonga.

guswa na unyasi ukadha
 
Hata hivyo hao wanyaturu wamshukuru Mungu aliyemwokoa mtu wao
 
Kwa Kweli zile Dua za kimila huwa hazina mchezo kwa mtu aliyedhulumiwa πŸ‘πŸ˜±
 
Exposure Therapy ya Tundu Laigwanan Lissu, sasa imekuwa ni tambiko!

Mbula.
 
Mauchawi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…