Tamko la Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunnah Tanzania (BASUTA) kuhusu mkataba baina ya Tanzania na DP World

Tamko la Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunnah Tanzania (BASUTA) kuhusu mkataba baina ya Tanzania na DP World

Huu waraka ndio unawakilisha brain halisi za waislam.

Bado kesho watashangaa na kuulizana kwa nini wenzetu upande wa pili wanachosema kinakuwa na nguvu!?
Kweli inashangaza sana, maaskofu hawakuwashutumu ansaar sunnar kwa kuunga mkono mkataba wa bandari, wao walizungumzia mapungufu ya mkataba na wakaukataa na kueleza sababu na wakataka marekebisho.
Sasa waislam wanaleta udini kwa vile aliyeuza bandari ni muislam na mnunuzi ni muislam.
Tuache udini kwenye tuzungumzie mkataba na siyo udini.
 
Hivi,wanapaswa kutoa mawazo yao kuhusu DP World au kushutumu wengine waliotoa maoni yao?Kwa nini hawataki kujifunza kukubaliana kutokukubaliana?Wakiambiwa maneno makali watajinunisha kwa akili hizo kweli?
Sa mkuu kama kusoma wanasoma lkn kuelewa context ni changamoto unategemea nn? Inabid tukosoe kile kilichoandikwa kwa lugha ya Taifa mkuu!!
 
Upumbavu huu.
Hili ni tamko juu ya mkataba wa DP world ama dhidi ya tamko la TEC?

Ni upumbavu kusema walifumbia macho mikataba ya zamani na kwa hiyo kwa vile walifumbia macho hata ikija mikataba ya hovyo wanyamaze!

Je ni kweli kwamba walifumbia?
Kwani kelele za mikataba mibovu hadi Magufuli kuikemea zilitoka wapi kama sio kwa watanzania hawa?
 
Sijamalizia kusoma nimesoma utangulizi tu nikapata picha halisi ya nini kilichoandikwa, hivi ukifanya makosa huko nyuma ndio tiketi ya kurudia makosa tena? Nadhani tunapaswa kujikita kwenye hoja sio kuwajadili waliopinga.

Wanaopinga wamepinga na wametoa sababu zao, na hasara ya huu mkataba, wanaokubali wao huwapinga na kuwashutumu bila kubainisha faida ya mkataba na kuwajibu kwa hoja.
 
Note: tunaamini uwezo wa akili wa viongozi wa answaar sunna ndio uwezo wenu nyie katika imani. Kama dp world atawekeza kweli basi hawatakubali kuwa na watu kama nyie kwenye operations zao Waalllah!
Pole sana
 
Tatizo hapa Tunatoka kwenye hoja na kuleta Undugu katika imani. Kilicho wakilishwa na TEC ni Hoja na sio Nani au Dini flani kupewa Tenda ya kuendesha Bandari yetu.

Tuki tetea dini zetu Au Mwenzetu katika imani kwenye maswala ya Rathilimali zetu Tutapotea kabisa Ndugu zetu.

Nchi hii isiposimamiwa Vizuri tutaendelea kuwa maskini na umaskini uo utakua umesababishwa na viongozi kutokua wazalendo na kusimamia mikataba kwa Uadilifu na Umakini.

Tuache dhana ya Udini kwenye jambo hili Embu SERIKALI ije na mkataba huu hadharani itoe Ufafanuzi kifungu kwa kifungu na sio kutoa manenotu bila Fact nadhani SERIKALI ikifanya hivyo ukweli utajulikana.
 
Waisalamu wenzangu hivi ni lini mtaachana na akili za TENDE HALUA? Baraza lilipaswa kujikita kwenye UHALALI na UBORA wa mkataba katika wasilisho la maoni yake. Badala yake wameonesha UPEO wao halisi wa masuala ya kitaifa namna ulivyo FINYU.

AIBU NIMEONA MIMI
View attachment 2728045
Wewe kiasi uone aibu maana uislamu haundeshwi kwa matamko kuna taratibu zake zimewekwa jinsi ya kukosoa na kuliendea jambo kuna njia pia ni jinsi gani kukosoa sii utaratibu wa kiislamu kumkosoa kiongozi hadharani wakati njia za kuonana nae hazijafungwa
 
Yani hii ndio inawakilisha brain ya kiislam miaka mitatu imepita tangu bandari ichimbwe mita 15 na tulitumia gharama kubwa na walikopa pesa kuiendeleza Leo hii wanataka mgeni aje anufaike chap, ni ujinga wa hali ya juu.
Tatizo sio kuweka pesa bandarini na blaa blaa kama hizo,swala ni productivity na uwezo wa kupanuka na kupata masoko.

Hata ungechimba daily kama huna Ufanisi na huwezi kushindana ni kazi Bure
 
Wamejibu kuhusu vipengele vyenye utata vya mkataba, au wanamtetea mwenzao katika imani hata kama hayupo sahihi?
Kama Mtu Hana HOJA Za Msingi, Unategemea Ajibu Nini Zaidi Ya KUJIFARIJI Kwa Mgongo Wa UDINI Huku akijua Kabisa Tatizo Liko Pale Pale !!
 
Lowasa alituambia kipaumbele chake ni elimu, elimu, elimu
Na hawa ni wasomi wa kiisramu!
Mnasema katiba imewapa uhuru wa kuongea, alafu hamtaki TEC aongee!
Na hivyo bipengere mbona hamja iongelea sasa?
Mnawatia aibu waisramu
 
Duh nanukuu..

"Hivyo basi, sisi BASUTA tusingependa kujikita kwenye mjadala wa vipengele mahususi wa Mkataba wenyewe wa bandari tukiamini mchakato unaenda vizuri na maslahi mapana ya taifa yatafikiwa"
Imani kwenye sheria!!? 😁
 
Back
Top Bottom