Tamko la Padre Kitima na changamoto ya Korona dhidi ya Usalama wa Nchi: Tunakwenda wapi baada ya hapa?

Tamko la Padre Kitima na changamoto ya Korona dhidi ya Usalama wa Nchi: Tunakwenda wapi baada ya hapa?

Najibu kwa ufupi. Andiko langu linalenga hadhira pana. Kwa hiyo, ni sahihi kuwa somehow academic, lakini sio too academic kama unavyosema. Kuhusu superiority na inferiority complex sina shida navyo, ila mie naamini katika argumentation supremacy. Nafundisha shule ya Msingi kwa vile ndio size yangu, nina Diploma ya Ualimu. Naishi vizuri na walimu wa UPE. Hapa Simbawanga ni pazuri, kuna amani, upendo, na kuchukuliana kwa upole. Karibu!
Unajua nimetokea kukupenda bure. Katika Kiswahili nadhani kuna shida ya maneno like na love! Kwa la kwanza your command of the language and your presentation. Kuhusu content we differ. But I'm sure you can always make my day. And our meeting won't be boring!

La pili you're lovable. Who doesn't wish a beautiful and intelligent daughter like you? I'm a senior citizen. Hakuna kizuri kikakosa kasoro. Diploma kwako ni kasoro. Utanielewa. Nikiwa bado shule, somo fulani nilipata 95%. Tunafanya masahihisho. Mwalimu alianzia nyuma.

Nilikuwa nakaa mbele. Akamsifia mwanafunzi fulani aliyepata 45%.Akisema amejitahidi sana na aongeze bidii. Nikajua nitanyeshewa sifa. Mwalimu alipofika kwangu akaanza kunigombeza. Akidai nilikuwa na uwezo wa kupata 100! Uwezo wako nikuwa na shahada ya uzamivu!

Kuna jambo silipendi kwako. Mabandiko yako kuhusu wabunge covid-19 na kuhusu Bagonza yalinichefua kuzidi maelezo. You stooped too low. And this's my worst worry: treading sycophantic intellectualism path. Jinamizi lililoivamia Tz bila huruma!
 
Tayari manung'uniko yako hayo nimeyajibu hapa:

Asante kwa kusoma. Japo ni nje ya mada, umeongelea upinzani wako dhidi yangu juu ya "kule kwenye wale wadada covid19." Unaniambia kwamba "Kule... ulichemka."

Naona hukuweza kuelewa maandiko yangu juu ya Timu Mdee (covid19) dhidi ya Timu Mbowe (covid19+).

Kwa vile wewe hukuelewa, nadhani hata wengine wengi hawakuelewa. Ufafanuzi mfupi unatolewa juu ya hilo kama ifuatavyo.

Kwanza ni kuhusu kanuni za jumla:

1. Mimi ni miongoni mwa wanaopinga ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi ndani ya chama na nje ya chama.
2. Mimi ni miongoni mwa wanaopinga itikadi ya samaki mmoja akioza basi wote wameoza.
3. Mimi ni miongoni mwa wanaopinga itikadi ya utapiahabari (disinformation) inayofanywa na wakubwa kwa sababu tu kwamba wao ni wakubwa.

Kwa sababu ya pointi hizi tatu, sasa nakufahamisha hoja zifuatazo, na ambazo ndio zinafafanua mabandiko yangu juu ya kina Mdee:

1. Tukio la ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi ndani ya chama unaorandana na sakata la kina Mdee ni moja kati ya matukio zaidi ya manne ninayoyafahamu. Mwaka 2010, nyaraka za uteuzi wa madiwani wa viti maalumkatika Ofisi ya Katibu Mkuu zilichakachuliwa na binti aitwaye Juliet Lushuli akapachikwa na kuteuliwa na Tume kuwa Diwani. Mwaka 2015, nyaraka za uteuzi wa madiwani wa viti maalumkatika Ofisi ya Katibu Mkuu zilichakachuliwa na binti aitwaye Annet Bagonza akapachikwa na kuteuliwa na Tume kuwa Diwani. Na mwaka 2015 yaraka za uteuzi wa wabunge wa viti maalum katika Ofisi ya Katibu Mkuu zilichakachuliwa na wanawake watano ambao walikuwa wanachama wa CCM wakapachikwa na kuteuliwa na Tume kuwa Wabunge. Kwa sababu ya matukio haya, kama tukio la kina Mdee limezalisha Covid19 basi matukio baki matatu yaliyosimamiwa na Mbowe yalizalisha Covid19+. Kwa hiyo, kuwaadhibu Covid19 na kuwaacha Covid19+ wakitembea kifua mbele hakutatui tatizo lililoko ndani ya Chama.

2. Katika uchaguzi mkuu uliopita, kuna vurugu zimefanywa ndani ya chama katika hatua zifuatazo: kuchukua fomu za uteuzi, kurudisha fomu za uteuzi, kupiga kura za maoni, kusikiliza rufaa za watia nia kabla Kamati Kuu haijapitisha wagombea. Kuna watu walinyimwa fomu, wapo walipewa fomu na kunyimwa nafasi ya kuzirudisha, wapo ambao majina yao yaliondolewa kinyemela kwenye karatasi za kura za maoni, wapo watia nia ambao waliongezewa kura zisizo zao, wapo watia niawaliokata rufaa na kufika kwenye ukumbi wa vikao vya rufaa lakini wakatelekezwa nje ya ukumbi huo kwa masaa 48 bila kusikilizwa hadi wakaondoka bila kusikilizwa wala kuambiwa sababu ya kutosikilizwa, wapo watia nia waliogawa rushwa kwa wajumbe waliokuja kupiga kura za maoni, na madudu mengine. Katika uchaguzi wa nje ya chama, uwezekano mkubwa ni kwamba, kuna vurugu pia zilifanyika katika hatua zote. Lakini, uwezekano mkubwa ni kwamba, hakuna vurugu iliyofanywa katika uchaguzi wa nje ya chama na ambayo haikufanyika katika uchaguzi wa ndani ya chama, isipokuwa matukio ya pre-marked illegal ballots. Ndani ya Chama vurugu hisi zimesimamiwa na Timu Mbowe (covid19+). Kwa hiyo, kuwaadhibu Covid19 na kuwaacha Covid19+ wakitembea kifua mbele hakutatui tatizo lililoko ndani ya Chama.

3. Wakati Mbowe anatangaza adhabu dhidi ya kina Mdee alitumia kanuni ya disinformation. Sio kweli kwamba, wabunge wote 19 walikula njama ya kutenda makosa waliyosomewa. Mbowe anaujua ukweli huu. Lakini alichofanya ni kama mwalimu wa darasa akute wanafunzi kadhaa wanapiga kelele, halafu alicharaze viboko darasa zima. Samaki mmoja akioza sio kweli kwamba wote wameoza. Kwa hiyo, kuwaadhibu Covid19 na kuwaacha Covid19+ wakitembea kifua mbele hakutatui tatizo lililoko ndani ya Chama.

4. Hitimisho: Kutokana na yote hayo hapo juu, kufikiri kuwa endapo Timu Mbowe watafanikiwa kuwaadhibu Timu Mdee, basi Chama kitakuwa kimesafishika ni ndoto za mchana. Kunahitajika tiba mbadala. Hiyo ndiyo pointi yangu juu ya sakata la kina Mdee Vs kina Mbowe. Ninafahamu kuwa kina Mdee sasa ni wabunge kwa sababu wanakingiwa kifua na mfumo tawala na sio vinginevyo. Najua kuwa msimamo huu ni kinyume cha Katiba ya nchi na sheria husika. Lakini, kipi kianze na kwa nini: Kutafuta heshima kwa Katiba ya Chama au kutafuta heshima kwa Katiba ya nchi? Ukitumia panga kwenye ugomvi wakati hujawahi kujifunza kungfu na unapigana na mtu mwenye ujuzi wa kutumia panga katika mapigano ya kungfu unaumia. Kusalama pia naona shida. Chadema imeishia kwenye Kanda, na toka Kanda hadi vitongojini ni kama inatengeneza merger na makanisa kadhaa. Such a symbiosis is a threat to national secutity. Kuna giza kubwa mbele ya Chadema ya leo. Yaani, naona mtanziko ambao unaashiria siku mbaya sana kwa Chadema huko mbeleni....

5. Msisitizo: Narudia tena kusema kwamba: napinga uchakachuaji wa utaratibu wa uchaguzi ndani ya chama uliowingiza majina ya wanaoitwa covid19 kwenye ofisi za NEC; kwamba napinga udhabu holela iliyotolewa kwa covid19 wote bila kuzingatia ushahidi uliokuwa mbele ya meza ya Kamati Kuu ukionyesha nani alifanya nini na yupi hakufanya nini; na kwamba ninapinga covid19+ kubeba mamlaka ya kuwaadhibu covi19 wakati covid19+ ni wachafu zaidi.
 
Hakuna kizuri kikakosa kasoro. Diploma kwako ni kasoro. Utanielewa. Nikiwa bado shule, somo fulani nilipata 95%. Tunafanya masahihisho. Mwalimu alianzia nyuma. Nilikuwa nakaa mbele. Akamsifia mwanafunzi fulani aliyepata 45%.Akisema amejitahidi sana na aongeze bidii. Nikajua nitanyeshewa sifa. Mwalimu alipofika kwangu akaanza kunigombeza. Akidai nilikuwa na uwezo wa kupata 100! Uwezo wako nikuwa na shahada ya uzamivu!
Mawazo yako ni ya kweli.
Nami nataka kupanda daraja.
Ndoto yangu kusoma mpaka hadi kupata Masters in Development Studies.
Nasikia kozi hiyo ipo huko kwenu Dar.
Huku 'Simbawanga' kozi kama hizo hazipo.
Kozi kama hiyo ni bei gani?
Nani anaweza kufadhili kozi kama hiyo?
Huwa najiuliza maswali haya kila mara.
Huwa nawauliza marafiki kila mara.
Wote hunambia kozi hizo ni za watoto wa vigogo tu kwani sio chini ya milioni 30.
Tangu nianze kazi miaka 10+ iliyopita cumulative salary yangu haijafika hata milioni 5.
Ni shida kweli!
Wewe unawajua wafadhili?
Kama ndiyo, nipe anwani zao leo!
 
View attachment 1720670
Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Athuman Diwani (Kushoto) akiwa amesimama na Rais John Magufuli (Kulia)

Wiki iliyopita, akiwa anatekeleza majukumu yake kama Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki la Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima, aliitisha mkutano wa maripota kutoka vyomba kadhaa vya upashanaji habari hapa Tanzania na kutoa tamko muhimu, ambalo kimantiki linaweza kufupishwa katika hoja yenye muundo ufuatao:

1. Matokeo yanayofanana huwa na sababu zinazofanana.

2. Kati ya Desemba 2020 na Februari 2021 makuhani tumeshuhudia vifo vingi vilivyotokana na changamoto za upumuaji ambazo huko nyuma tuliona kuwa zilikuwa ni dalili za ugonjwa wa virusi vya korona, yaani UVIKO;

3. Kwa hiyo, huenda vifo hivyo vimetokana na UVIKO;

4. Njia ya uhakika zaidi ya kutuwezesha kujua ukweli juu ya chanzo cha vifo vinavyotokea sasa hivi ni kufanya upimaji wa kisayansi.

5. Na tayari tunavyo vifaa vya kisayansi kwa ajili ya kutambua maambukizi ya UVIKO, lakini serikali inatuzuia kufanya vipimo hivyo;

6. Hakuna sababu nzuri ya serikali kuendelea kuzuia vituo vyetu vya afya kuchukua vipimo vya UVIKO;

7. Kwa hiyo, kwa niaba ya TEC, na kupitia kwenu waandishi wa habari, natoa wito kwa serikali kuruhusu wataalam wa tiba kutekeleza kwa vitendo mchakato wa vipimo vya kisayansi kuhusisna na tatizo la UVIKO.

Kupitia tamko lake Padre Kitima aliufahamisha umma kwamba Kanisa Katoliki linamiliki na kuendesha vituo vya afya zaidi ya 500 ambavyo mapaka sasa vimezuiwa na serikali kufanya kazi ya kupima uwepo wa virusi vya ugonjwa wa korona, jambo ambalo ni sawa na kulizuia Kanisa kufanya kazi yake ya kitume kupitia huduma ya tiba za kisayansi.

Padre Kitima alisema kuwa, katika mazingira haya, tayari mapadre 25 na watawa 60 wamekufa kwa sababu ya changamoto za upumuaji, changamoto ambazo huwasumbua sana waathirika wa virusi vya korona.

Hivyo, Padre Kitimaalitoa wito wa kulikumbusha Taifa la Tanzania juu ya umuhimu, uharaka na ulazima wa kuienzi Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi kupitia huduma ya tiba za kisayansi.

Kwa ujumla, tamko la Padre Kitima liliongelea nafasi ya Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi katika kutatua matatizo ya jumuiya ambayo ni pamoja na ujinga, maradhi kama vile Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO), umaskini, rushwa na unyonyaji.

Hata hivyo, wito wa Padre Kitima haujapokelewa vema na baadhi ya Watanzania. Kuna waliokejeli hoja yake, wapo waliomkejeli yeye mleta hoja, na wapo waliojaribu kuhamisha mawazo ya wasikilizaji kutoka kwenye hoja iliyo mezani na kuwapeleka kwenye hoja mwanasesere, hasa hoja zenye kuamsha hisia na kudhoofisha urazini.

Naona kuwa zote hizi ni mbinu za makusudi kwa ajili ya kupotosha ukweli uletao uhuru dhidi ya ujinga.

Ni upotoshaji unaofanywa kwa ajili ya kutafuta maslahi ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kidini au kutafuta maslahi mengine, yaani utapiahabari (disinformation).

Katika miaka kadhaa iliyopita, na hasa tangu enzi za kashfa kubwa kubwa, tatizo la “disinformation” limekuwa ni miongoni mwa maadui wakubwa wa maendeleo ya Taifa maadui wengine wakiwa ni ujinga, maradhi, umaskini, rushwa na unyonyaji.

Yaani, ukitaka kuelewa KIRAHISI maana ya utapiahabari (disinformation) kumbuka namna taarifa juu ya matukio yafuatazo zilizofanyiwa menejimenti: Escrow, Lugumi, Epa, Nida, Richmond, Kiwira, Meremeta, Tangold, Kagoda, Buzwagi, Uuzwaji Nyumba za Serikali, Ununuzi wa Majengo Pacha ya Bot, Loliondo Gate, Chavda na Mashamba ya Mkonge, Pembe za Ndovu Kwenye Ndege ya Rais Wa China, Uuzwaji Nyumba za Serikali, Uuzwaji wa Fukwe, Ununuzi wa Nyumba ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Italy, ununuzi wa BAE Radar, Deep Green Finance Company Limited, BoT Twin Towers, Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Buzwagi contract, Mchuchuma mine, Loliondo Hunting Blocks, Mwananchi Gold, Mafuta House, Meremeta Limited, Quality Plaza, Tangold Limited, Mwananchi Trust Co. Ltd, NA Tanzania International Container Terminal Services (TICTS).

Sasa tatizo hilo limehamia kwenye ugonjwa wa virusi vya korona (UVIKO). Lakini, tatizo hili la utapiahabari katika kipengele cha UVIKO lisingekuwa kubwa zaidi kama serikali ingekuwa inaelewa na kuheshimu tofauti zilizopo kati ya sayansi na ushirikina.

Ushirikina ni tabia ya kuamini na kuaminisha watu baki katika matukio yanayotokana na sababu za miujiza bandia wakati sababu halisi zipo.

Na kwa mujibu wa
Aristotle "sayansi ni maarifa ya hakika na dhahiri yanayopatikana kutokana na uthibitisho wa kirazini." Yaani, "science is the sure and evident knowledge obtained from demonstration."

Naye
Mt. Aquinas anakubaliana na fasili hii anaposema kuwa "sayansi ni ujuzi wa vitu unaoanzia katika sababu zake za kweli." Yaani, "science is the knowledge of things from their true causes."

Hii maana yake ni kuwa mitaala yote ya chuo kikuu ni sayansi zinazotofautiana, sio kwa aina, bali kwa viwango tu.

Kwa kuzingatia ukweli huu juu ya sayansi, hapa chini, napendekeza kufafanua umuhimu, uharaka na ulazima wa wito wa Padre Kitima katika kutatua matatizo haya kwa kuonyesha tofauti kati ya ushirikina na sayansi.

Napendekeza kwamba kuna tofauti kubwa sita kati ya mtu ambaye ni mwanasayansi na mtu ambaye sio mwanasayansi. Na njia bora ya kuonyesha tofauti hizo ni kujadili hatua kuu saba zilizomo katika Mchakato wa utafiti wa Kisayansi. Yaani, mchakato wa “Kuona, Kuhoji, Kutuhumu, Kutafiti, Kutahini, Kuhukumu na Kutenda.”

Hivyo, kwa sababu hii, Kanuni ya utafiti wa Kisayansi tunaweza kuiita “Kanuni ya 7K,” kama mchoro ufuatao unavyoonyesha:

View attachment 1722615
Mchoro wenye kuonyesha Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi

Kwa mujibu wa mchoro huu, hatua ya kwanza katika Mchakato wa Utafiti wa Kisayansi ni “kuona.” Na neno “kuona” (observation) linamaanisha kitendo chochote cha mtu kutumia mlango wowote wa fahamu, yaani macho, masikio, ngozi, ulimi au pua, ili kubaini mabadiliko yanayotokea katika mazingira yake na kutunza kumbukumbu ya mabadiliko hayo kichwani mwake.

Kila mtu mwenye akili timamu anaweza kupokea taarifa na kutunza kumbukumbu ya matukio yanayoendelea katika mazingira yake.

Tofauti ya kwanza kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kuona utata na hivyo kubaini tatizo kwa “kuhoji” sababu ya utata huo (problem definition).

Ukweli ni kwamba, sio kila mtu anayeweza “kuona” atachukua hatua ya pili ya “kuhoji.” Kimsingi, kuhoji ni hatua ya kujiuliza swali la “kwa nini jambo hili linatokea namna hii na sio vinginevyo?

Kwa mfano, Mwanasayansi Isaac Newton (1642-1727) alipokuwa ameketi chini ya mti na kuona tunda linadondoka kuelea kwenye uso wa dunia, na sio kupaa angani, alijiuliza swali, “kwa nini?

Watu wengi kabla yake walikuwa wanaona tukio hilo lakini ni wachache waliwahi kujiuliza swali hili.

Hivyo, tofauti ya kwanza kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kubaini tatizo kwa “kuhoji” (problem definition).

View attachment 1721758

Mwanasayansi Sir Isaac Newton (1642-1727)
Tofauti ya pili kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kubuni tuhuma inayojaribu kujibu swali lilijitokeza hapo awali. Sio kila mtu anayejiuliza “kwa nini?” anasonga mabele na kujaribu kupendekeza jawabu kwa swali hilo.

Kwa mfano, baada ya Isaac Newton kujiuliza swali la “kwa nini tunda linadondoka kuelekea kwenye uso wa dunia na sio kinyume chake?” alipendekeza kwamba huenda kuna nguvu ya uvutano kati ya dunia na tunda, ambapo ukubwa wa nguvu hiyo unategemea uzito wa dunia, uzito wa tunda na umbali kati ya tunda na dunia.

Watu wengi kabla ya Newton walikuwa wanaona tukio la kudondoka kwa matunda na kujiuliza swali kama yeye, lakini ni wachache waliowahi kujaribu kupendekeza jawabu la makisio kama alivyofanya Newton.

Hivyo, tofauti ya pili kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa “kubuni tuhuma” (hypothesis formulation) ambayo ni jawabu la makisio tu.

Tofauti ya tatu kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kuandaa jaribio kwa ajili ya kukusanya ushahidi (evidence collection) unaoweza kutumika katika hatua ya kutahini ukweli wa tuhuma (hypothesis testing) iliyobuniwa hapo awali kama jawabu la makisio,.

Kwa mfano, baada ya Newton kupendekeza kwamba huenda kuna nguvu ya uvutano kati ya dunia na tunda, ambapo ukubwa wa nguvu hiyo unategemea uzito wa dunia, uzito wa tunda na umbali kati ya tunda na dunia, aliandaa jaribio la kimaabara na kukusanya taarifa muhimu kwa ajili ya kuthibitisha tuhuma hii.

Watu wengi kabla ya Newton walikuwa wanaona matukio ya kudondoka kwa matunda, kujiuliza swali kama yeye, na kujaribu kupendekeza jawabu la makisio kama alivyofanya Newton. Lakini, ni wachache waliwahi kuchukua hatua ya ziada ya kubuni jaribio kwa ajili ya kukusanya taarifa zinazoweza kutumika katika kutahini ukweli wa tuhuma husika.

Hivyo, uwezo wa kukusanya ushahidi (data collection) kwa ajili ya kutuwezesha “kutahini ukweli wa tuhuma” (hypothesis testing) ndio tofauti ya tatu kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi.

Maandalizi ya jaribio kwa ajili ya kukusanya taarifa zitakazotumika kutahini ukweli wa tuhuma hutegemea sekta ya sayansi inayohusika. Kuna sayansi asilia, sayansi za jamii, sayansi za kihistoria, sayansi za kifalsafa, na sayansi za kiteolojia.

Kila sekta ina upekee wake. Hapa nitatumia mfano wa sekta ya sayansi asilia ambako ukusanyaji wa ushahidi hutegemea milango mitano ya fahamu.

Kwa ufupi, wanasayansi asilia hutumia majaribio pacha kukusanya ushahidi. Jaribio la kwanza huwa ni kwa ajili ya kutahini ukweli wa tuhuma chanya (positive hypothesis), na jaribio la pili ni kwa ajili ya kutahini ukweli wa tuhuma hasi (null hypothesis).

Tofauti ya nne kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kutumia ushahidi uliokusanywa “kutahini ukweli wa tuhuma” (hypothesis testing) iliyo mezani.

Yaani, kama ilivyo katika mtihani wowote, kazi ya kutahini ukweli wa tuhuma inatoa fursa kwa mtahiniwa (yaani mleta tuhuma) ama kufauli au kufeli. Hii ni hatua ya kujiuliza: Je ushahidi uliokusanywa unakubaliana na tuhuma au unapishana na tuhuma? KInachofanyika ni sawa na kazi ya mwalimu kusahihisha karatasi za mtihani kwa kutumia skimu ya uhakiki.

Kama majibu ya mwanafunzi yanakubaliana na majibu yaliyo katika skimu ya uhakiki, basi mwanafunzi anapewa alama, vinginevyo anapigwa mkasi. Vivyo hivyo, kama ushahidi uliokusanywa ukithibitisha tuhuma, basi mtahiniwa anakuwa amefaulu. Na kama ushahidi uliokusanywa ukishindwa kuthibitisha tuhuma, basi mtahiniwa anakuwa amefeli.

Tofauti ya tano kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kufanya hukumu (theory formulation) sahihi baada ya kukusanya na kutafsiri ushahidi wa kitafiti.

Kwa mfano, kama tunataka kujua kama dawa ya kwinini inatibu ugonjwa wa malaria, tutaandaa makundi mawili ya watu wenye vimelea vya malaria. Kundi la kwanza watapewa dozi ya kwinini na kundi la pili hawapewi dozi hiyo.

Baada ya muda vipimo vya damu vitachukuliwa kutoka kila kundi. Kama kundi lililopewa dozi ya kwinini litapona na kundi la pili kuendelea kuumwa malaria, tutahitimisha kuwa dawa ya kwinini inaweza kutibu malaria, ikiwa masharti kadhaa yatazingatiwa.

Hitimisho hili litakuwa ni hukumu ya mtafiti dhidi ya mtu aliyeleta tuhuma kwamba "huenda dawa ya kwinini inatibu ugonjwa wa malaria kama vidonge viwili viwili vikimezwa kwa siku tatu mfululizo."

Na hivyo, uwezo wa “kuhukumu” kwa usahihi, yaani uwezo wa kutafsiri taarifa za kitafiti kwa kuandika nadharia sahihi unatupa tofauti ya tano kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi.

Na tofauti ya sita, na ya mwisho, kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kuweka nadharia katika vitendo.

Kwa mfano, kama nadharia ya kutibu malaria kwa kutumia kwinini inasema kuwa mgonjwa ameze vidonge viwili kila siku asubuhi, kwa siku tatu mfululizo, basi uwezo wa kusimamia utaratibu huu wa matibabu pia utamtofautisha mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi.

Hivyo, tofauti ya sita kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa “kutekeleza nadharia” kwa usahihi (theory application).

Tulipokuwa wanafunzi wa shule ya sekondari mwalimu wetu wa sayansi alitufundisha kukumbuka Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi, kwa msaada wa neno OPHETTA.

Neno OPHETTA ni kifupi cha maneno haya: “Observation Making, Problem Definition, Hypothesis Formulation, Evidence Collection,Hypothesis Testing, Theory Formulation, Theory Application.

Yaani, kwa Kiswahili tunaweza kusema kwamba, Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi ni kanuni inayotuhimiza “Kuona, Kuhoji, Kutuhumu, Kutafiti, Kutahini, Kuhukumu na Kutenda.” Ndio maana nimeiita “Kanuni ya 7K.

Kanuni hii inayo matumizi mapana katika sekta zote za sayansi, zikiwemo sayansi asilia, sayansi za jamii, sayansi za kihistoria, sayansi za kifalsafa, na sayansi za kiteolojia. Sayansi hizi zinatofautishwa na jinsi hatua za "kukusanya ushahidi (evidence collection) na “kutahini ukweli wa tuhuma” (hypothesis testing) zinavyofanyika.

Kwa mujibu wa Papa Yonae Paul II, kanuni ya OPHETTA ni kanuni inayomtofautisha mwanasayansi na mshirikina. Alipoandika waraka wake uiwato "Faith and Reason (1998)," yaani “Fides et Ratio (1998),” alikuwa anataka kuwakumbusha makuhani katoliki juu ya umuhimu wa kutumia kanuni ya OPHETTA katika uinjilishaji. Papa anaandika:

"Scripture, therefore, is not the Church's sole point of reference. The 'supreme rule of her faith' derives from the unity which the Spirit has created between Sacred Tradition, Sacred Scripture and the [scientific and philosophical reason of the] Magisterium of the Church in a reciprocity which means that none of the three can survive without the others." (ib. 55).

Hapa, Papa anawahimiza makuhani kubalansi hoja zao kwa kutumia ushahidi uliokusanywa kutokana na Mapokeo, Misahafu, na Urazini wa Majisteria ya Kanisa. Urazini huo unarejea maarifa ya Sayansi na Filosofia kama yanavyotafsiriwa na Majisteria ya Kanisa, baada ya kushauriana na
Taasisi zipatazo 10 za Kisayansi na Kifalsafa zinazoongozwa na Papa.

Taasisi hizo ni pamoja na: Pontifical Academy of Sciences;
Pontifical Academy of Social Sciences; Pontifical Academy for Life; Pontifical Academy of St Thomas Aquinas; Pontifical Theological Academy; Pontifical International Marian Academy; Pontifical Academy of Fine Arts and Letters of the Virtuosi at the Pantheon; Pontifical Roman Academy of Archaeology; Pontifical Academy Cultorum Martyrum; Pontifical Ecclesiastical Academy; na Pontifical Academy for Latin.

Baada ya kusikiliza tamko lake, ni hitimisho langu kwamba, Kuhani Charles Kitima ametekeleza vizuri agizo hilo.

View attachment 1721706

Padre Charles Kitima, Katibu Mkuu wa TEC, akiwa amebeba kitabu chenye jina la "Ibada ya Misa Takatifu"

Baada ya kusema haya, napenda kumalizia andiko langu kwa kusema mambo manne.

Kwanza, nawaalika wanazuoni wote wa Tanzania kuienzi kanuni ya OPHETTA kwa kuifanya kaulimbiu yao ya kila siku.

Ni kanuni inayowahusu wanasiasa, wachumi, wanasosiolojia, watumishi wa umma, wanasheria, wanateolojia, na waandishi wa habari.

Pili, na kwa namna ya pekee, nawaalika Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa kuienzi kanuni ya OPHETTA kila wakati, kila mahali na kwa kila mtendaji.

Nimewahi kuambiwa kwamba, taarifa kadhaa zinazoandaliwa na baadhi ya Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa zinakiuka kanuni ya OPHETTA, na hasa katika hatua ya kukusanya ushahidi kwa ajili ya kutahini ukweli wa tuhuma (hypothesis testing).

Hivyo, kama tatizo hili bado lipo, namwaalika Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athuman, kuchukua hatua stahiki za kuwajengea uwezo maafisa wake wanaopwaya.

Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa asiyejua tofauti kati ya tuhuma na hukumu atakuwa anakiuka kanuni ya OPHETTA kila siku, na hivyo kuhatarisha Usalama wa Taifa anaopaswa kuulinda.

Na ninaona kuwa huenda kina Cyprian Musiba ni miongoni mwa watu wa aina hii.

Wito wangu ni kuwa Idara ya Usalama wa Taifa inapaswa kulisaidia Taifa kusogea karibu na sayansi na kuwa mbali na ushirikina ambao ni moja ya vitisho vikubwa dhidi ya usalama wa nchi.

Na tatu, Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi inayo nafasi kubwa katika Maendeleo ya Taifa letu, na hasa katika kukabiliana na ushirikina unaoambatana na changamoto za upumuaji zilizoligubika Taifa.

Sayansi imekuwa na mchango mkubwa sana katika jamii. Kwanza, imekuwa kimiminika cha kuyeyusha punje za ushirikina. Imetusaidia kuachana na kasumba ya kauli ya bosi ni ukweli siku zote.

Na mengine mengi, kama Bertrand Russel anavyotuarifu katika kitabu chake kiitwacho THE IMPACT OF SCIENCE IN SOCIETY (New York: AMS Press, 1968). Katika kitabu hiki kinachopatikana bure mtandaoni tunasoma yafuatayo:

“Out of the work of the great men of the seventeenth century a new outlook on the world was developed, and it was this outlook, not specific arguments, which brought about the decay of the belief in portents, witchcraft, demoniacal possession, and so forth. I think there were three ingredients in the scientific outlook of the eighteenth century that were specially important: (I) Statements of fact should be based on observation, not on unsupported authority. (2) The inanimate world is a self-acting, self-perpetuating system, in which all changes conform to natural laws. (3) The earth is not the center of the universe…” (Russel 1968: 6)

Kwa sababu hizi zote, ni maoni yangu kuwa, tunakopaswa kwenda baada ya hapa ni kwenye maabara zinazotumia kanuni ya OPHETTA.

Taarifa kwamba kuna vituo vya afya zaidi ya 500 vinavyomilikiwa na Kanisa Katoliki ambavyo vimezuiwa kupima ugonjwa wa virusi vya korona ni kashfa inayoliweka Taifa letu karibu na ukweli wa kishirikina na kulisogeza mbali na ukweli wa kisayansi.

Ushirikina ni moja ya vitisho vikuu dhidi ya usalama wa nchi sehemu zote duniani.

Hivyo, serikali yetu inapaswa kubadilisha mtazamo wake kuanzia sasa kwa kuruhusu upimaji wa kisayansi katika vituo vyote vya afya vilivyopo nchini.

Na nne, siku zote tusisahau mahusiano ya kietiolojia (etiological connections) yafuatayo yaliyopo kati ya maadui wakubwa dhidi ya usalama wa nchi:

Ushirikina na utapiahabari (disinformation) huleta ujinga, ujinga huleta magonjwa, magonjwa huleta umaskini, umaskini huleta unyonge, unyonge huleta vifo, vifo humomonyoa nguvukazi ya Taifa, mmomonyoko wa nguvukazi ya Taifa huleta kifo cha Taifa.

KIla mtu anaalikwa kulinda Usalama wa Taifa letu kwa kuukata huu mnyororo wa kietiolojia ili kuliweka huru Taifa letu dhidi ya kifo.

Naomba kuwasilisha hoja, na wote karibuni "Simbawanga" Primary School ninakofundisha.

View attachment 1721725

Padre Charles Kitima, Rais Magufuli, Askofu Nyaisonga na Askofu mwingine mmoja wakiwa wanajadiliana juu ya Maendeleo ya Taifa la Tanzania
Kanisa liko sahihi
 
Mawazo yako ni ya kweli.
Nami nataka kupanda daraja.
Ndoto yangu kusoma mpaka hadi kupata Masters in Development Studies.
Nasikia kozi hiyo ipo huko kwenu Dar.
Huku 'Simbawanga' kozi kama hizo hazipo.
Kozi kama hiyo ni bei gani?
Nani anaweza kufadhili kozi kama hiyo?
Huwa najiuliza maswali haya kila mara.
Huwa nawauliza marafiki kila mara.
Wote hunambia kozi hizo ni za watoto wa vigogo tu kwani sio chini ya milioni 30.
Tangu nianze kazi miaka 10+ iliyopita cumulative salary yangu haijafika hata milioni 5.
Ni shida kweli!
Wewe unawajua wafadhili?
Kama ndiyo, nipe anwani zao leo!
Tutawasiliana na kuona jinsi ya kufanikisha hiyo shauku yako!
 
Uhai wako ni mali yako, sio maslahi ya Roma, Over!
Kiuweledi hakupaswa kuongelea hali ya UVIKO, angezungumzia hali ya kiroho ya Tanzania ambayo 'kimsingi' ndio wajibu wa padre Kitima.
 
Nilitaka kuandika jambo juu ya huyo uliyomjibu ila nikafuta.
Ukweli ni kwamba andiko lako limeshiba, limejaa maswali pamoja na majibu ndani yake. Ndio maana hao wapotoshaji wanashindwa kunukuu aya Yoyote ya bandiko hili na kisha kulitolea makanushao yao.

Tunashukuru kwa elimu uliyoitoa
Ni heri ulifuta ulichoandika. Hakikuwa sahihi. Huelewi. Huyo sio mpotoshaji. Hajashindwa kunukuu. Amenukuu kikubwa na kukanusha. Yatosha tu kusema kuwa wewe ni mwanafunzi anayemtetea aliyetoa elimu katika andiko lililoshiba. Na mwenye mwandiko huu ni mkufunzi mwelekezi kwa mwalimuyo na sio mpotoshaji aslani.
 
Kiuweledi hakupaswa kuongelea hali ya UVIKO, angezungumzia hali ya kiroho ya Tanzania ambayo 'kimsingi' ndio wajibu wa padre Kitima.

Ukuta unaotenganisha mwili na roho ni mkubwa na impermeable kiasi gani?
 
Na tano, ni wito kwa wanateolojia kuhusu mafundisho ya kidini yanayohamasisha ushirikina miongoni mwa waumini wake. Nitatumia mfano wa mvutano kati ya Rais Magufuli na baadhi ya viongozi wa dini.

Tamko la Padre Kitima lenye kuilalamikia uamuzi wa serikali wa kulikataza Kanisa kuchukua vipimo vya ugonjwa wa virusi vya korona kupitia vituo vyake vya afya, limekuja wakati ambapo Rais Magufuli anawatuhumu baadhi ya vioongozi wa dini kufanya maamuzi yanayopingana na imani wanayomfundisha yeye kama muumini wao.

Rais John Magufuli ni muumini wa Kanisa Katoliki. Anasema kuwa, viongozi wake wa dini wamekuwa wanafundisha kwamba, wakati wa mageuzi, mkate na divai hugeuka mwili na damu ya Yesu kiuhalisia; kwamba Yesu ni Mungu; na kwamba Mungu anaweza kufanya kila kitu.

Kwa hiyo, kwa mtazamo wa Rais Magufuli, kila muumini anayekula mwili na kunywa damu ya Yesu, hapaswi kuogopa ugonjwa wa virusi vya korona, kwani ndani ya maumbo ya mkate na divai kunapaswa kuwepo na kinga ya kimungu inayoweza kuua virusi vya korona. Hii maana yake ni kwamba, hakuna haja ya waumini wenye maisha mazuri ya kisakramenti kuvaa barakoa wala kutumia sanitaiza.

Lakini, kilichomshangaza Rais Magufuli ni kwamba, changamoto ya ugonjwa wa virusi vya korona imesababisha waumini wengi wenye maisha mazuri ya sakramenti kufa na kuwasukuma baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki kufunga makanisa yao kwa muda.

Kwa hiyo, kuna mambi mawili yanawezekana. Ama wakati wa mageuzi (consecration) Yesu haingii katika maumbo ya mkate na divai tofauti na viongozi wa dini wanavyofundisha. Au wakati wa mageuzi (consecration) Yesu huingia katika maumbo ya mkate na divai kama viongozi wa dini wanavyofundisha, lakini huyo Yesu hana nguvu ya kufanya kila kitu kama viongozi wa dini wanavyofundisha. Ndio kusema kwamba, Yesu anayeingia katika maumbo ya mkate na divai anazo nguvu dhaifu kuliko nguvu za virusi vya korona.

Mpaka Padre Kitima anatoa tamko lake, bado Rais Magufuli alikuwa anaendelea kusisitiza kwamba, kuvaa barakoa ni dalili ya imani haba juu ya Mungu anayeweza kufanya kila kitu. Bila shaka, hii ndiyo sababu iliyomsukuma kuzuia vituo vya afya nchini kuchukua virusi vya korona.

Lakini, Padre Kitima anasema hapana. Hata kama viongozi wa dini wanafundisha kwamba Mungu anaweza kufanya kila kitu, bado kuna haja ya kuchukua vipimo vya kisayansi. Hili ndilo chimbuko la mgogoro kati ya Kanisa Katoliki na serikali inayoongozwa na Rais Magufuli.

Hivyo, natoa wito kwa wanateolojia. Kuna kila dalili kwamba, baadhi ya mafundisho ya kidini yanachochea ushirikina. Kwa mfano, katika kila altare ya Kanisa Katoliki kuna mifupa ya watakatifu inawekwa. Nilimsikia Askofu aliyehubiri siku ya kuhamisha mwili wa Kardinali Rugambwa kuupeleka Kanisa alikozikwa akijigamba, "hata sisi huo ndio uchawi wetu."

Kuna maji ya mabaraka, chumvi ya baraka, kupunga pepo, sala ya mageuzi (consecration) ambako tunafundishwa kwamba Yesu anaingia katika maumbo ya mkate na divai kifiziolojia, na mambo kama haya.

Ni kwa sababu hizi, na sababu zinazofanana na hizi, baadhi ya waumini kama vile Rais Magufuli wanasema kwamba hostia takatifu na maombi ni silaha tosha dhidi ya korona. Wanateolojia wetu wanasemaje kuhusu changamoto hii, na wanatoa mwogozo gani kwa watu hawa?
Hoja hii imekaa vizuri.
Wanateolojia wetu mko wapi?
Leteni nondo zenu hapa tuelimike.
 
Ukuta unaotenganisha mwili na roho ni mkubwa na impermeable kiasi gani?
Ukuta haupo kabisa. Hata ufa tu ni balaa kubwa. Hivyo anayetunza kimojawapo hana budi kutunza na kingine pia. Mwili hauwezi kuwepo bila roho. Hiyo ni maiti. Roho bila mwili ni mzimu au mzuka. Kifo ni kutengana kwa mwili na roho. Padri hahudumii mizimu. Wote wanaokariri kuwa kazi ya watumishi wa Mungu ni ya kiroho tu ni misikule.
 
View attachment 1720670
Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Athuman Diwani (Kushoto) akiwa amesimama na Rais John Magufuli (Kulia)

Usuli

Tarehe 03 Machi 2021, akiwa anatekeleza majukumu yake kama Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki la Tanzania (TEC), Padre Charles Kitima, aliitisha mkutano wa maripota kutoka vyomba kadhaa vya upashanaji habari hapa Tanzania na kutoa
tamko muhimu, ambalo lilibeba hoja kadhaa, hoja yake mojawapo ikiwa inaweza kufupishwa katika muundo wa kimantiki ufuatao:

1. Matokeo yanayofanana huwa na sababu zinazofanana.
2. Kati ya Desemba 2020 na Februari 2021 makuhani tumeshuhudia vifo vingi vilivyotokana na changamoto za upumuaji ambazo huko nyuma tuliona kuwa zilikuwa ni dalili za ugonjwa wa virusi vya korona, yaani UVIKO;
3. Kwa hiyo, huenda vifo hivyo vimetokana na UVIKO;
4. Njia ya uhakika zaidi ya kutuwezesha kujua ukweli juu ya chanzo cha vifo vinavyotokea sasa hivi ni kufanya upimaji wa kisayansi.
5. Na tayari tunavyo vifaa vya kisayansi kwa ajili ya kutambua maambukizi ya UVIKO, lakini serikali inatuzuia kufanya vipimo hivyo;
6. Hakuna sababu nzuri ya serikali kuendelea kuzuia vituo vyetu vya afya kuchukua vipimo vya UVIKO;
7. Kwa hiyo, kwa niaba ya TEC, na kupitia kwenu waandishi wa habari, natoa wito kwa serikali kuruhusu wataalam wa tiba kutekeleza kwa vitendo mchakato wa vipimo vya kisayansi kuhusisna na tatizo la UVIKO.

Kupitia tamko lake Padre Kitima aliufahamisha umma kwamba Kanisa Katoliki linamiliki na kuendesha vituo vya afya zaidi ya 500 ambavyo mapaka sasa vimezuiwa na serikali kufanya kazi ya kupima uwepo wa virusi vya ugonjwa wa korona, jambo ambalo ni sawa na kulizuia Kanisa kufanya kazi yake ya kitume kupitia huduma ya tiba za kisayansi.

Naandika kama raia ili kutoa maoni yangu juu ya tamko hili kwa kuonyesha sababu zenye kueleza kwa nini wito wa Padre Kitima haupaswi kupuuziwa na serikali.

Utangulizi

Tangu Machi 2020, ugonjwa wa virusi vya korona (UVIKO) ulipozuka, mjadala wa siku nyingi juu ya mahusiano yaliyopo kati ya sayansi na dini umefufuka upya.

Kihistoria, zimekuwepo kambi kuu nne. Kuna kambi ya watu wanaosema kuwa dini na sayansi ni maadui wasioweza kusalimiana. Hawa wanadai kwamba, kauli za upande mmoja zinapinga kauli za upande wa pili, kama ambavyo tofauti kati ya nadharia ya uumbaji wa viumbe hai na nadharia ya mvuvumko wa viumbe hai zinavyothibitisha. Hii ni nadharia inayosisitiza uhasama kati ya sayansi na dini.

Kuna kambi ya watu wanaosema kuwa dini na sayansi ni majirani wasio na mahusiano ya urafiki wala uadui. Hawa wanadai kwamba, kila kambi ni himaya inayojitegemea ambako mwingine hawezi na hapaswi kukanyaga, kama ambavyo tofauti zilizopo kati ya data zinazoonekana kwa njia ya milango mitano yafahamu na tunu za kimaadili zisizoonekana wala kugusika zinavyothibitisha. Hii ni nadharia inayosisitiza uhuru wa sayansi na dini, yaani kila kambi kujitegemea.

Kuna kambi ya watu wanaosema kuwa dini na sayansi ni majirani wanaokamilishana. Hawa wanadai kwamba, kila kambi ni himaya ambako jirani wa upande wa pili anaweza na anapaswa kukanyaga kwa ajili kubadilishana mawazo na mwenzake ili kutafuta mwafaka juu ya masuala muhimu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hii ni nadharia inayosisitiza majadiliano endelevu kati ya dini na sayansi.

Na kuna kambi ya watu wanaosema kuwa dini na sayansi ni marafiki wanaweza kusalimiana. Hawa wanadai kwamba, kuna kauli za upande mmoja zinazosikilizana na kauli za upande wa pili. Hii ni nadharia inayosisitiza kuendeleza mwafaka uliopo kati ya sayansi na dini.

Mjadala bado unaendelea juu ya nafasi ya nadharia hizi nne katika jamii. Lakini, kwa hapa Tanzania, ujio wa uviko umeligawanya Taifa katika kambi kuu mbili. Kuna kambi ya kina Rais Magufuli inayosema kuwa sala, maombi na sakramenti ya kumunio ni mazindiko tosha dhidi ya maambukizi ya UVIKO. Hivyo, kwa sababu hii, serikali ilipiga marufuku vipimo vyote vya kisayansi katika maabara za serikali na sekta binafsi.

Na kwa upande mwingine, kuna kambi ya kina Padre Kitima wanaosema kuwa dini na sayansi ni majirani wanaokamilishana. Hawa wamekuwa wanahimiza wananchi kusali na kuzingatia maagizo yote ya wanasayansi. Pia wamekuwa wanahimiza serikali kuruhusu vipimo vya kisayansi kufanyika katika maabara zote nchini.

Kwa mujibu wa tamko la Padre Kitima, tangu Desemba 2020 hadi Machi 2021, tayari mapadre 25 na watawa 60 wamekufa kwa sababu ya changamoto za upumuaji, changamoto ambazo zilikuwa zinawasumbua sana waathirika wa virusi vya korona katika miezi ya Machi 2020.

Hivyo, Padre Kitimaalitoa wito wa kulikumbusha Taifa la Tanzania juu ya umuhimu, uharaka na ulazima wa kuienzi Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi kupitia huduma ya tiba za kisayansi.

Kwa ujumla, tamko la Padre Kitima liliongelea nafasi ya Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi katika kutatua matatizo ya jumuiya ambayo ni pamoja na ujinga, maradhi kama vile Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO), umaskini, rushwa na unyonyaji.

Hata hivyo, wito wa Padre Kitima haujapokelewa vema na baadhi ya Watanzania. Kuna waliokejeli hoja yake, wapo waliomkejeli yeye mleta hoja, na wapo waliojaribu kuhamisha mawazo ya wasikilizaji kutoka kwenye hoja iliyo mezani na kuwapeleka kwenye hoja mwanasesere, hasa hoja zenye kuamsha hisia na kudhoofisha urazini.

Naona kuwa zote hizi ni mbinu za makusudi kwa ajili ya kupotosha ukweli uletao uhuru dhidi ya ujinga. Ni upotoshaji wa ukweli unaofanywa kimakusudi kwa ajili ya kutafuta maslahi fulani ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kidini au vinginevyo, yaani, kwa neno moja, utapiahabari (disinformation).

Na kama tunavyojua, utapiahabari huleta ujinga, ujinga huleta magonjwa, magonjwa huleta umaskini, umaskini huleta unyonge, unyonge huleta vifo, vifo huleta mmomonyoko wa nguvukazi ya Taifa, mmomonyoko wa nguvukazi ya Taifa huleta kifo cha Taifa.

Kwa hiyo, utaona kuwa, katika miaka kadhaa iliyopita, na hasa tangu enzi za kashfa kubwa kubwa, tatizo la utapiahabari limekuwa tatizo lililoongezeka katika orodha ya maadui wakubwa wa maendeleo ya Taifa letu.

Yaani, ukitaka kuelewa kirahisi maana na ukubwa wa tatizo la utapiahabari hapa nchini kumbuka namna taarifa juu ya matukio yafuatazo zilivyochakachuliwa: Escrow, Lugumi, Epa, Nida, Richmond, Kiwira, Kagoda, Mkataba wa Buzwagi, Uuzwaji Nyumba za Serikali, Ununuzi wa Majengo Pacha ya Bot, Kashfa ya Loliondo, Chavda na Mashamba ya Mkonge, Pembe za Ndovu Kwenye Ndege ya Rais Wa China, Uuzwaji wa Fukwe za Bahari ya Hindi, Ununuzi wa Nyumba ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Italia, ununuzi wa BAE Radar, Deep Green Finance Company Limited, Ujenzi wa Maghorofa Pacha ya BoT, Mradi wa IPTL, Mgodi wa Mchuchuma, Vitalu vya Uwindaji, Kampuni ya Mwananchi Gold Ltd, Kampuni ya Meremeta Ltd, Mradi wa Quality Plaza, Kampuni ya Tangold Ltd, Kampuni ya Mwananchi Trust Co. Ltd, na Kampuni ya TICTS ya kule Bandarini Dar.

Sasa hivi tatizo hilo la utapiahabari limehamia kwenye sekta ya uhai wa binadamu kupitia ugonjwa wa virusi vya korona (UVIKO). Lakini, haki ya kuishi ni kikonyo cha haki zingine zote. Yaani, haki za binadamu ni haki za binadamu hai. Mwili wa marehemu ni mabaki ya mwili wa binadamu.

Kwa hiyo, tunapaswa kusanifu na kusambaza hoja za kukataa na kukataza itikadi ya utapiahabari kuhamishiwa kwenye sekta ya uhai wa bindamu. Hoja katika bandiko hili ni hoja mojawapo kati ya hoja nyingi zinazoweza kusanifiwa na watetezi wa uhai wa binadamu na uhai wa Taifa.

Tofauti kati ya sayansi na ushirikina

Lakini, ni maoni yangu kwamba, tatizo hili la utapiahabari katika kipengele cha UVIKO lisingekuwa kubwa zaidi kama serikali ingekuwa inaelewa na kuheshimu tofauti zilizopo kati ya sayansi na ushirikina.

Ninavyoelewa mimi, "
ushirikina ni tabia ya kuamini na kuaminisha watu baki kwamba tukio moja ni chimbuko la tukio jingine wakati ukweli ni kwamba hakuna uhusiano wa sababu na matokeo kati ya matukio hayo mawili."

Ndio kusema kuwa, mtu ambaye akili yake inaongozwa na imani ya kishirikina ni kama mtu aliyevaa miwani ya rangi nyekundu ambayo humfanya kuona kwamba kila kitu kilicho mbele yake kina rangi nyekundu wakati ukweli halisi hauko hivyo. Anakuwa amekumbwa na tatizo la
akili yake kuona maruweruwe kila anapojaribu kutambua sababu za vitu mbalimbali.

Yaani, ushirikina ni ulemavu wa akili kama ambavyo
tatizo la upofu wa kushindwa kuona baadhi ya rangi ni ulemavu wa macho unaomfanya mhusika kushindwa kabisa kutambua rangi kadhaa kwa kutumia macho.

Na kwa upande mwingine, naelewa kwamba, "
sayansi ni maarifa ya hakika juu ya vitu na sababu zake za kweli yaliyopatikana kutokana na uthibitisho dhahiri wa kirazini."

Kwa hiyo, mwanasyansi ni mtu ambaye anamini na kuaminisha watu baki kwamba tukio moja ni chimbuko la tukio jingine kwa sababu ukweli ni kwamba kuna uhusiano wa sababu na matokeo kati ya matukio hayo mawili, ambapo tukio la kwanza ni sababu ya tukio la pili.

Matukio mawili yanayoletana huwa na mahusiano ya sababu na matokeo na husemekana kuwa na mahusiano ya kietiolojia, kwa kuwa "etiolojia" ni sayansi inayochunguza mahusiano kati ya sababu na matokeo yake.

Katika mahusiano haya ya kietiolojia, tukio la kwanza huitwa sababu, chanzo, kiini, asili au chimbuko la tukio la pili. Na tukio la pili huitwa matokeo, hatima, tamati au fainali ya tukio la kwanza.

Na kwa ujumla, endapo tukio A na tukio B ni matukio mawili tofauti yanayowezekana, basi, matukio haya yanaletana endapo, na endapo tu, ikiwa tukio A linatokea ni lazima tukio B lifuate, na ikiwa tukio A halitokei ni lazima kwamba tukio B halitafuata.

Kwa ujumla, fasili hizi za maneno "sayansi," "sababu" na "matokeo" zinamaanisha kuwa mitaala yote ya chuo kikuu ni sayansi zinazotofautiana, sio kwa aina, bali kwa viwango tu.

Sayansi imekuwa na mchango mkubwa sana katika jamii. Kwanza, imekuwa kimiminika cha kuyeyusha punje za ushirikina. Imetusaidia kuachana na kasumba ya kauli ya bosi ni ukweli siku zote.

Kuna manufaa mengine mengi sana ya sayansi. Kwa ufupi, kutokana na kazi ya watu mashuhuri wa karne ya kumi na saba mtazamo mpya juu ya ulimwengu ulibuniwa, na ilikuwa mtazamo huu, sio hoja maalum, ambao ulisababisha kupuuzwa kwa imani kwamba kuna juju, uchawi, watu wanaopagawa kwa sababu ya mapepo, na kadhalika.

Kimsingi, kulikuwa na viambata vikuu vitatu katika mtazamo wa kisayansi wa karne ya kumi na nane ambavyo vilikuwa muhimu sana.

Kwanza, ni madai kwamba, taarifa za ukweli zinapaswa kutegemea uchunguzi, na kusikiliza sio kutoka kwa mamlaka isiyo na ushahidi thabiti mikononi.

Pili ni madai kwamba, ulimwengu wa vitu vinavyoonekana na kushikika ni mfumo wenye kujisimamia na kujiendesha binafsi, na ambamo mabadiliko yote huongozwa na kanuni za maumbile.

Na tatu ni madai kwamba, dunia sio kitovu cha ulimwengu wa sayari zote tunazozifahamu.

Mchakato wa tafiti zinazofanyika kisayansi

Tangu enzi za kina Isaac Newton, mchakato wa utafiti wa Kisayansi umevuvumka na kuhusisha hatua saba zifuatazo: “Kuona, Kuhoji, Kutuhumu, Kutafiti, Kutahini, Kuhukumu na Kutenda.” Kwa sababu hii, Kanuni ya utafiti wa Kisayansi tunaweza kuiita “Kanuni ya 7K.

View attachment 1721758
Mwanasayansi Sir Isaac Newton (1642-1727)

Hatua saba za utafiti wa kisayansi ni: (1) Kutambua tukio (kuona) kwa msaada wa hisia za macho, masikio, mdomo, pua au ngozi; (2) Kuhoji sababu ya pengo linalojitokeza kati ya matarajio yako na uhalisia wa kitu ulichokiona; (3) Kutuhumu sababu ya ulichokiona kwa kupendekeza jawabu la awali; (4) Kukusanya taarifa za kiushahidi kwa ajili ya kuthibitisha au kukanusha tuhuma; (5) Kutahini ushahidi ulioukusanya kwa kupima kama unathibitisha au kukanusha tuhuma; (6) Kama tuhuma inathibitika, kufanya hukumu kwa kuandaa hitimisho la kinadharia kwa msingi wa ushahidi uliokusanywa na kutahiniwa; na (7) Kutangaza nadharia na kuiweka katika vitendo.

Mchoro ufuatao unaonyesha vizuri hatua zinazotumika kwenye mchakato wa utafiti unaofuata ustaarabu wa kisayansi:

View attachment 1727086
Mchoro wenye kuonyesha Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi

Hebu sasa tutumie mfano wa kawaida kabisa kuonyesha jinsi ustaarabu wa kufanya utafiti wa kisayansi unavyofanyika.

Kwa sababu ya kutumia milango mitano ya fahamu, ni wazi kuwa, watu wengi tunatumia ustaarabu wa tafiti za kisayansi kila siku tunapotumia milango mitano ya fahamu, hata kama hatujui kwamba tunafanya hivyo. Kwa mfano, fikiria kuwa, unataka kuchaji simu yako.

KUONA: Umechomeka chaja kwente simu na kwenye soketi ya umeme ukutani. Matarajio yako ni kwamba utaona kioo cha simu kinapiga kope kuashiria kuwa simu inapokea moto. Lakini ukiangalia kioo hicho unaona kuwa hakuna dalili zozote zenye kuonyesha kwamba simu hiyo inapokea moto. Hapa kuna pengo kati ya matarajio na uhalisia, na pengo hili linahitaji maelezo.

KUHOJI: Hapa utajiuliza, kwa nini kioo cha simu ninayotaka kuichaji hakipigi kope kama ambavyo huwa kinafanya siku nyingine huko nyuma?

KUTUHUMU: Baada ya kujiuliza swali la "kwa nini" hatua inayofuata ni kujaribu kutabiri au kuotea sababu zake. Huenda TANESCO wamekata umeme; huenda umeme katika meta yako ya LUKU umekwisha; huenda soketi ya umeme ukutani imeharibika; huenda kitako cha simu unayojaribu kuchaji kimeharibika; au huenda simu yote imeharibika. Zote hizi ni tuhuma zinazowezekana, na kunahitajika namna ya kuzipangua moja baada ya nyingine ili hatimaye simu ipate chaji.

KUKUSANYA USHAHIDI: Unaweza kuchunguza kama nyumba ya jirani imeunganishwa kwenye umeme na kama TV yake inaongea ili kujua kama TANESCO wamekata umeme au hapana; unaweza kuchungulia kwenye LUKU ili kuona kama bado kuna yuniti za umeme au zimekwisha ili uweze kuongeza umeme; unaweza kudadidisi sebule kusudi uone kama kuna soketi ya pili, ili uweze kuhamishia chaja kwenye soketi nyingine na kuona kama simu itawaka; na unaweza kuona kama kuna mtu mwenye simu nyingine jirani yako kusudi uweze kuchomeka chaja ile ile kwenye simu nyingine na kuona kama simu hiyo itawaka.

KUTAHINI USHAHIDI: Katika hatua hii, kama umegundua kuwa nyumba ya jirani imeunganishwa kwenye umeme WA tanesco na kama TV yake inaongea ina maana TANESCO hawajakata umeme; kama LUKU haina yuniti za umeme unaweza kuongeza umeme ili upate kuchaji simu yako baada ya hapo; kama sebuleni kuna soketi ya pili unaweza kuhamishia chaja kwenye soketi nyingine na kuona kama simu itawaka; na kama kuna mtu mtu mwenye simu nyingine jirani yako unaweza kumwomba na kuchomeka chaja ile ile kwenye simu yake ili kuona kama simu hiyo itawaka.

KUHUKUMU: Katika hatua hii, kama TANESCO hawajakata umeme utahitimisha kuwa umeme wa TANESCO unafika kwenye nyumba yako ; kama LUKU ina yuniti za umeme utahitimisha kuwa umeme wa TANESCO unafika kwenye soketi ya ukutani; kama soketi ya pili haikuiwezesha simu kuwaka utahitimisha kwamba kitako cha simu kimeharibika; na kama simu nyingine ya jirani yako itawaka utahitimisha kuwa kitako cha simu kimeharibika. KIla hitimisho ni hukumu, kwa maana ya nadharia inayoelezea sababu ya pengo ulilolibaini kati ya matarajio na uhalisia wa kitu ulichokiona.

KUTENDA: Kila hitimisho lililofikiwa katika hatua inayofuata linamaanisha hatua fulani ichukuliwe. Kwa mfano, kama TANESCO hawajakata umeme na LUKU yako ina yuniti za umeme zero inataamua kuchaji simu yako kwa jirani. Na kama utahitimisha kuwa umeme wa TANESCO unafika kwenye soketi ya ukutani na simu nyingine ya jirani yako haiwaki kwa kutumia chaja ile ile utaamua kubadilisha chaja ili kuchaji simu yako.

Muhtasari wa hatua saba katika mchakato wa kutafiti kisayansi

Tulipokuwa wanafunzi wa shule ya sekondari mwalimu wetu wa sayansi alitufundisha kukumbuka Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi, kwa msaada wa neno OPHETTA.

Neno OPHETTA ni kifupi cha maneno haya: “Observation Making, Problem Definition, Hypothesis Formulation, Evidence Collection, Hypothesis Testing, Theory Formulation, Theory Application.

Yaani, kwa Kiswahili tunaweza kusema kwamba, Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi ni kanuni inayotuhimiza “Kuona, Kuhoji, Kutuhumu, Kutafiti, Kutahini, Kuhukumu na Kutenda.” Ndio maana nimeiita “Kanuni ya 7K.

Kanuni hii inayo matumizi mapana katika sekta zote za sayansi, zikiwemo sayansi asilia, sayansi za jamii, sayansi za kihistoria, sayansi za kifalsafa, na sayansi za kiteolojia. Sayansi hizi zinatofautishwa na jinsi hatua za "kukusanya ushahidi (evidence collection) na “kutahini ukweli wa tuhuma” (hypothesis testing) zinavyofanyika.

Tofauti kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayani

Kwa kutumia Kanuni za 7K iliyojadiliwa hapo juu, sasa tunaweza kutofautisha kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi. Tunajua kuwa, kila mshirikina sio mwanasayansi, lakini sio kila mtu asiye mwanasayansi ni mshirikina.

Hapa nataka kutofautisha kati ya watu ambao sio mwanasayansi na sio washirikina, kwa upande mmoja, na watu ambao sio mwanasayansi na ni washirikina, kwa upande mwingine, ili kwa njia hiyo, tuweze kuweka mikakati miwili.

Mosi ni mkakati wa kuwatoa maofisini watu ambao sio mwanasayansi na ni washirikina. Na pili ni mkakati wa kuwarudisha kwenye mstari watu ambao sio mwanasayansi na sio washirikina.

Napendekeza kwamba kuna tofauti kubwa sita kati ya mtu ambaye ni mwanasayansi na mtu ambaye sio mwanasayansi. Hatua saba (7) za mchakato wa utafiti wa kisayansi zinatoa mwanga muhimu hapa.

Kila mtu mwenye akili timamu anaweza kupokea taarifa na kutunza kumbukumbu ya matukio yanayoendelea katika mazingira yake. Kwa hiyo, katika hatua ya kwanza hakuna tofauti kati ya mtu ambaye ni mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi.

Kwa maneno mengine, tofauti ya kwanza kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi inajitokeza kwenye hatua ya pili, yaani uwezo wa kuona utata na hivyo kubaini tatizo kwa “kuhoji” sababu ya utata huo (problem definition).

Ukweli ni kwamba, sio kila mtu anayeweza “kuona” atachukua hatua ya pili ya “kuhoji.” Kimsingi, kuhoji ni hatua ya kujiuliza swali la “kwa nini jambo hili linatokea namna hii na sio vinginevyo?

Kwa mfano, Mwanasayansi Isaac Newton (1642-1727) alipokuwa ameketi chini ya mti na kuona tunda linadondoka kuelea kwenye uso wa dunia, na sio kupaa angani, alijiuliza swali, “kwa nini?

Watu wengi kabla yake walikuwa wanaona tukio hilo lakini ni wachache waliwahi kujiuliza swali hili.

Hivyo, tofauti ya kwanza kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kubaini tatizo kwa “kuhoji” (problem definition).

Tofauti ya pili kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kubuni tuhuma inayojaribu kujibu swali lilijitokeza hapo awali. Sio kila mtu anayejiuliza “kwa nini?” anasonga mabele na kujaribu kupendekeza jawabu kwa swali hilo.

Kwa mfano, baada ya Isaac Newton kujiuliza swali la “kwa nini tunda linadondoka kuelekea kwenye uso wa dunia na sio kinyume chake?” alipendekeza kwamba huenda kuna nguvu ya uvutano kati ya dunia na tunda, ambapo ukubwa wa nguvu hiyo unategemea uzito wa dunia, uzito wa tunda na umbali kati ya tunda na dunia.

Watu wengi kabla ya Newton walikuwa wanaona tukio la kudondoka kwa matunda na kujiuliza swali kama yeye, lakini ni wachache waliowahi kujaribu kupendekeza jawabu la makisio kama alivyofanya Newton.

Hivyo, tofauti ya pili kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa “kubuni tuhuma” (hypothesis formulation) ambayo ni jawabu la makisio tu.

Tofauti ya tatu kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kuandaa jaribio kwa ajili ya kukusanya ushahidi (evidence collection) unaoweza kutumika katika hatua ya kutahini ukweli wa tuhuma (hypothesis testing) iliyobuniwa hapo awali kama jawabu la makisio,.

Kwa mfano, baada ya Newton kupendekeza kwamba huenda kuna nguvu ya uvutano kati ya dunia na tunda, ambapo ukubwa wa nguvu hiyo unategemea uzito wa dunia, uzito wa tunda na umbali kati ya tunda na dunia, aliandaa jaribio la kimaabara na kukusanya taarifa muhimu kwa ajili ya kuthibitisha tuhuma hii.

Watu wengi kabla ya Newton walikuwa wanaona matukio ya kudondoka kwa matunda, kujiuliza swali kama yeye, na kujaribu kupendekeza jawabu la makisio kama alivyofanya Newton. Lakini, ni wachache waliwahi kuchukua hatua ya ziada ya kubuni jaribio kwa ajili ya kukusanya taarifa zinazoweza kutumika katika kutahini ukweli wa tuhuma husika.

Hivyo, uwezo wa "kukusanya ushahidi kitafiti" (data collection) kwa ajili ya kutuwezesha “kutahini ukweli wa tuhuma” (hypothesis testing) ndio tofauti ya tatu kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi.

Maandalizi ya jaribio la kitafiti kwa ajili ya kukusanya taarifa zitakazotumika kutahini ukweli wa tuhuma hutegemea sekta ya sayansi inayohusika. Kuna sayansi asilia, sayansi za jamii, sayansi za kihistoria, sayansi za kifalsafa, na sayansi za kiteolojia.

Kwa mfano, wataalam wa sayansi asilia na sayansi za jamii hutumia majaribio pacha kukusanya ushahidi. Jaribio la kwanza huwa ni kwa ajili ya kutahini ukweli wa tuhuma chanya (positive hypothesis), na jaribio la pili ni kwa ajili ya kutahini ukweli wa tuhuma hasi (null hypothesis). Wanafalsafa na wanateolojia wanazo mbinu zao za ziada.

Tofauti ya nne kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kutumia ushahidi uliokusanywa “kutahini ukweli wa tuhuma” (hypothesis testing) iliyo mezani.

Yaani, kama ilivyo katika mtihani wowote, kazi ya kutahini ukweli wa tuhuma inatoa fursa kwa mtahiniwa (yaani mleta tuhuma) ama kufauli au kufeli. Hii ni hatua ya kujiuliza: Je ushahidi uliokusanywa unakubaliana na tuhuma au unapishana na tuhuma? KInachofanyika ni sawa na kazi ya mwalimu kusahihisha karatasi za mtihani kwa kutumia skimu ya uhakiki.

Kama majibu ya mwanafunzi yanakubaliana na majibu yaliyo katika skimu ya uhakiki, basi mwanafunzi anapewa alama, vinginevyo anapigwa mkasi. Vivyo hivyo, kama ushahidi uliokusanywa ukithibitisha tuhuma, basi mtahiniwa anakuwa amefaulu. Na kama ushahidi uliokusanywa ukishindwa kuthibitisha tuhuma, basi mtahiniwa anakuwa amefeli.

Tofauti ya tano kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kutoa hukumu (theory formulation) sahihi baada ya kukusanya na kutafsiri ushahidi wa kitafiti.

Kwa mfano, kama tunataka kujua kama dawa ya kwinini inatibu ugonjwa wa malaria, tutaandaa makundi mawili ya watu wenye vimelea vya malaria. Kundi la kwanza watapewa dozi ya kwinini na kundi la pili hawapewi dozi hiyo.

Baada ya muda vipimo vya damu vitachukuliwa kutoka kila kundi. Kama kundi lililopewa dozi ya kwinini litapona na kundi la pili kuendelea kuumwa malaria, tutahitimisha kuwa dawa ya kwinini inaweza kutibu malaria, ikiwa masharti kadhaa yatazingatiwa.

Hitimisho hili litakuwa ni hukumu ya mtafiti dhidi ya mtu aliyeleta tuhuma kwamba "huenda dawa ya kwinini inatibu ugonjwa wa malaria kama vidonge viwili viwili vikimezwa kwa siku tatu mfululizo."

Na hivyo, uwezo wa “kuhukumu” kwa usahihi, yaani uwezo wa kutafsiri taarifa za kitafiti kwa kuandika nadharia sahihi unatupa tofauti ya tano kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi.

Kuna tofauti ndogo sana kati ya kutahini ukweli wa tuhuma (hypothesis testing) na hatua ya kutoa kuhukumu (theory formulation). Njia rahisi ya kueleza ni kurejea walimu wanachofundishwa katika somo liitwalo "Measurement and Evaluation," maneno ambayo hapa nayatafsiri kama "Kutahini na Kuhukumu Maendeleo Mwanafunzi."

Kutahini uwezo wa mwanafunzi ni kutafuta alama za mwanafunzi katika jaribio fulani. Na kuhukumu uwezo wa mwanafunzi ni kutafsiri maana ya alama hizo ili kumweka katika kundi mojawapo la wanafunzi wenye uwezo unaofanana. Ni viyvom hivyo katika kutahini na kuhukumu ukweli wa tuhuma ya kisayansi (scientific hypothesis).

Ufafanuzi huu unaturuhusu kuona tofauti ya sita kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi. Tofauti ya sita, na ya mwisho, kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa kuweka nadharia katika vitendo (theory application).

Kwa mfano, kama nadharia ya kutibu malaria kwa kutumia kwinini inasema kuwa mgonjwa ameze vidonge viwili kila siku asubuhi, kwa siku tatu mfululizo, basi uwezo wa kusimamia utaratibu huu wa matibabu pia utamtofautisha mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi.

Hivyo, tofauti ya sita kati ya mwanasayansi na mtu asiye mwanasayansi ni uwezo wa “kutekeleza nadharia” kwa usahihi (theory application).

Mtazamo wa Kanisa Katoliki Kuhusu Sayansi

Tangu enzi za Galileo Galilei (1564–1642), Baba wa Taifa la Wanasayansi, Kanisa Katoliki limeendelea kuboresha mtazamo wake juu ya uhusiano kati ya Sayansi na Dini. Nitaeleza kwa ufupi.

View attachment 1721706

Padre Charles Kitima, Katibu Mkuu wa TEC, akiwa amebeba kitabu chenye jina la "Ibada ya Misa Takatifu"

Kwa mfano, Papa Yonae Paul II, katika "
Waraka juu ya Makutano ya Imani na Urazini (1998)," anasema kuwa kanuni ya OPHETTA ni kanuni inayomtofautisha mwanasayansi na mshirikina.

Alipoandika alikuwa waraka huu anataka kuwakumbusha makuhani katoliki juu ya umuhimu wa kutumia kanuni ya OPHETTA katika uinjilishaji.

Papa alisema kwamba, Misahafu sio marejeo pekee ya Kanisa, kwani, Kanuni ya imani yake inatokana na umoja uliopo katika vyanzo vikuu vitatu, yaani, Mapokeo , Misahafu na Urazini wa kisayansi na kifalsafa uliothbitishwa na vyombo vya kitafiti vinavyomilikiwa na Mamlaka Kuu ya Kanisa.

Alifafanua kwamba, vyanzo hivi vitati vina hadhi sawa, kwa maana kwamba hakuna hata chanzo kimoja kati yake, kinachoweza kujitosheleza bila kukamilishwa na vyanzo vingine viwili (ibara ya 55).

Kwa njia hii, Papa aliwahimiza makuhani kubalansi hoja zao kwa kutumia ushahidi uliokusanywa kutokana na Mapokeo, Misahafu, na Urazini wa Majisteria ya Kanisa. Urazini huo unarejea maarifa ya Sayansi na Filosofia kama yanavyotafsiriwa na Majisteria ya Kanisa, baada ya kushauriana na
Taasisi zipatazo 10 za Kisayansi na Kifalsafa zinazoongozwa na Papa.

Taasisi hizo za Kipapa ni pamoja na: Akademia ya Sayansi Asilia; Akademia ya Sayansi za Jamii; Akademia ya Uhai; Akademia ya Mt. Thomas Aquinas; na Akademia ya Teolojia ya Kipapa.

Baada ya kusikiliza tamko la Kuhani Charles Kitima, ni hitimisho langu kwamba, yeye ni mwanafunzi mzuri wa Papa Yohanne Paul II na mtu mwenye uelewa mkubwa kuhusu nafasi ya Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi katika maisha ya watu.

Pia ni mwanafunzi mzuri wa kina Galileo Galilei, JOhannes Kepler, Isaac Newton na Albert Eistein. Kauli yake ifuatayo ni ushahidi tosha:

''Ukweli huwaweka watu huru, kama mafundisho ya Biblia yanavyosema, lakini Tanzania tunaambiwa (na serikali kwamba) utaleta hofu. (Kanisa Katoliki linasisitiza kwamba) ukweli utapatikana kwa njia ya tafiti huru (za kisayansi)."

Padre Kitima pia alisisitiza kwamba kutegemea sala pekee hakuwezi kuondosha tatizo la ugonjwa wa korona nchini.

''Mungu si hirizi. Anataka binadamu tuwajibike. Korona ipo. Unaambiwa chukua tahadhari unasema umekwisha sali... Mungu wetu anataka tuwajibike. Yaani tutende majukumu yetu kwa karama na utashi tuliopewa," anafafanua Padre Kitima.

Ni kwa sababu ya imani hii thabiti katika ustaaarabu wa tafiti za kisayansi, hatimaye Padre Kitima aliwaalika wataalam wa tiba, watafiti na wanasayansi kufanya utafiti ili kubaini chanzo cha vifo vya watu wanaokufa kwa sababu changamoto za upumuaji.

View attachment 1726202

Baba wa Taifa la Wanasayansi, Galileo Galilei
Hitimisho na mapendekezo muhimu

Tumeona tofauti kati ya sayansi na ushirikina kwa kusisitiza kwamba sayansi ni zaidi ya sayansi asilia, na kwamba sayansi ni maarifa yaliyothibitishwa kirazini kwa kutumia njia mahsusi kulingana na sekta ya sayansi inayohusika. Baada ya kusema haya, napenda kumalizia andiko langu kwa kupendekeza mambo matano.

View attachment 1721725

Padre Charles Kitima, Rais Magufuli, Askofu Nyaisonga na Askofu mwingine mmoja wakiwa wanajadiliana juu ya Maendeleo ya Taifa la Tanzania

Kwanza, nawaalika wanazuoni wote wa Tanzania kuienzi kanuni ya OPHETTA kwa kuifanya kaulimbiu yao ya kila siku.

Ni kanuni inayowahusu wanasiasa, wachumi, wanasosiolojia, watumishi wa umma, wanasheria, wanateolojia, na waandishi wa habari.

Pili, na kwa namna ya pekee, nawaalika Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa kuienzi kanuni ya OPHETTA kila wakati, kila mahali na kwa kila mtendaji.

Nimewahi kuambiwa kwamba, taarifa kadhaa zinazoandaliwa na baadhi ya Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa zinakiuka kanuni ya OPHETTA, na hasa katika hatua ya kukusanya ushahidi kwa ajili ya kutahini ukweli wa tuhuma (hypothesis testing).

Hivyo, kama tatizo hili bado lipo, namwaalika Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athuman, kuchukua hatua stahiki za kuwajengea uwezo maafisa wake wanaopwaya.

Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa asiyejua tofauti kati ya tuhuma na hukumu atakuwa anakiuka kanuni ya OPHETTA kila siku, na hivyo kuhatarisha Usalama wa Taifa anaopaswa kuulinda.

Na ninaona kuwa huenda kina Cyprian Musiba ni miongoni mwa watu wa aina hii.

Wito wangu ni kwamba, Idara ya Usalama wa Taifa inapaswa kulisaidia Taifa kusogea karibu na sayansi na kuwa mbali na ushirikina ambao ni moja ya vitisho vikubwa dhidi ya usalama wa nchi.

Naamini kuwa, Kanuni ya Utafiti wa Kisayansi inayo nafasi kubwa katika Maendeleo ya Taifa letu, na hasa katika kukabiliana na ushirikina unaoambatana na changamoto za upumuaji zilizoligubika Taifa.

Tatu, kwa sababu hizi zote, ni maoni yangu kuwa, tunakopaswa kwenda baada ya hapa ni kwenye maabara zinazotumia kanuni ya OPHETTA. Wataalam wa tiba tulio nao wapewe nafasi ya kuamsha vipaji vyao.

Taarifa kwamba kuna vituo vya afya zaidi ya 500 vinavyomilikiwa na Kanisa Katoliki ambavyo vimezuiwa kupima ugonjwa wa virusi vya korona ni kashfa inayoliweka Taifa letu karibu na ukweli wa kishirikina na kulisogeza mbali na ukweli wa kisayansi.

Nasisitiza kuwa, ushirikina ni moja ya vitisho vikuu dhidi ya usalama wa nchi sehemu zote duniani. Hivyo, serikali yetu inapaswa kubadilisha mtazamo wake kuanzia sasa kwa kuruhusu upimaji wa kisayansi katika vituo vyote vya afya vilivyopo nchini.

Nne, napendekeza kwamba, siku zote tukumbuke kuwa tunalo jukumu la kukata mnyororo wa sababu na matokeo (etiological connections) unaotengenezwa na muungano wa maadui wakubwa dhidi ya usalama wa nchi yetu.

Mnyororo huo ni kama ifuatavyo: Ushirikina na utapiahabari (disinformation) huleta ujinga, ujinga huleta magonjwa, magonjwa huleta umaskini, umaskini huleta unyonge, unyonge huleta vifo, vifo huleta mmomonyoko wa nguvukazi ya Taifa, mmomonyoko wa nguvukazi ya Taifa huleta kifo cha Taifa.

Hivyo, kila mtanzania anaalikwa kulinda Usalama wa Taifa letu kwa kuukata huu mnyororo wa kietiolojia ili kuliweka huru Taifa letu dhidi ya kifo. Njia nzuri ya kuua nyoka ni kugonga kichwa. Na kichwa cha mnyororo huu wa kietiolojia ni "Ushirikina na utapiahabari."

Tuanzie hapo na yeyote atakayejaribu kukwamisha kazi hii anapaswa kuwekwa pembeni kistaarabu. nchi yoyote dunia, na Tanzan ia ikiwemo, ni kubwa kuliko serikali yake. Aidha, nchi yoyote dunia, na Tanzan ia ikiwemo, ni kubwa kuliko mkuu wake wa nchi.

Na tano, ni wito kwa wanateolojia kuhusu mafundisho ya kidini yanayohamasisha ushirikina miongoni mwa waumini wake. Nitatumia mfano wa mvutano kati ya Rais Magufuli na baadhi ya viongozi wa dini.

Tamko la Padre Kitima lenye kuilalamikia uamuzi wa serikali wa kulikataza Kanisa kuchukua vipimo vya ugonjwa wa virusi vya korona kupitia vituo vyake vya afya, limekuja wakati ambapo Rais Magufuli anawatuhumu baadhi ya vioongozi wa dini kufanya maamuzi yanayopingana na imani wanayomfundisha yeye kama muumini wao.

Rais John Magufuli ni muumini wa Kanisa Katoliki. Anasema kuwa, viongozi wake wa dini wamekuwa wanafundisha kwamba, wakati wa mageuzi, mkate na divai hugeuka mwili na damu ya Yesu kiuhalisia; kwamba Yesu ni Mungu; na kwamba Mungu anaweza kufanya kila kitu.

Kwa hiyo, kwa mtazamo wa Rais Magufuli, kila muumini anayekula mwili na kunywa damu ya Yesu, hapaswi kuogopa ugonjwa wa virusi vya korona, kwani ndani ya maumbo ya mkate na divai kunapaswa kuwepo na kinga ya kimungu inayoweza kuua virusi vya korona. Hii maana yake ni kwamba, hakuna haja ya waumini wenye maisha mazuri ya kisakramenti kuvaa barakoa wala kutumia sanitaiza.

Lakini, kilichomshangaza Rais Magufuli ni kwamba, changamoto ya ugonjwa wa virusi vya korona imesababisha waumini wengi wenye maisha mazuri ya sakramenti kufa na kuwasukuma baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki kufunga makanisa yao kwa muda.

Kwa hiyo, kuna mambi mawili yanawezekana. Ama wakati wa mageuzi (consecration) Yesu haingii katika maumbo ya mkate na divai tofauti na viongozi wa dini wanavyofundisha. Au wakati wa mageuzi (consecration) Yesu huingia katika maumbo ya mkate na divai kama viongozi wa dini wanavyofundisha, lakini huyo Yesu hana nguvu ya kufanya kila kitu kama viongozi wa dini wanavyofundisha. Ndio kusema kwamba, Yesu anayeingia katika maumbo ya mkate na divai anazo nguvu dhaifu kuliko nguvu za virusi vya korona.

Mpaka Padre Kitima anatoa tamko lake, bado Rais Magufuli alikuwa anaendelea kusisitiza kwamba, kuvaa barakoa ni dalili ya imani haba juu ya Mungu anayeweza kufanya kila kitu. Bila shaka, hii ndiyo sababu iliyomsukuma kuzuia vituo vya afya nchini kuchukua virusi vya korona.

Lakini, Padre Kitima anasema hapana. Hata kama viongozi wa dini wanafundisha kwamba Mungu anaweza kufanya kila kitu, bado kuna haja ya kuchukua vipimo vya kisayansi. Hili ndilo chimbuko la mgogoro kati ya Kanisa Katoliki na serikali inayoongozwa na Rais Magufuli.

Hivyo, natoa wito kwa wanateolojia. Kuna kila dalili kwamba, baadhi ya mafundisho ya kidini yanachochea ushirikina ambao unamfanya hata mkuu wa nchi kugeuka kituko. Kwa mfano, wakati wa ujenzi wa Kanisa kila altare ya Kanisa Katoliki inawekewa mifupa ya watakatifu. Nilimsikia Askofu aliyehubiri siku ya kuhamisha mwili wa Kardinali Rugambwa kuupeleka Kanisani alikozikwa akijigamba, "hata sisi huo ndio uchawi wetu."

Kuna maji ya mabaraka, chumvi ya baraka, kupunga pepo, sala ya mageuzi (consecration) ambako tunafundishwa kwamba Yesu anaingia katika maumbo ya mkate na divai kifiziolojia, na mambo kama haya.

Ni kwa sababu hizi, na sababu zinazofanana na hizi, baadhi ya waumini kama vile Rais Magufuli wanasema kwamba hostia takatifu na maombi ni silaha tosha dhidi ya korona. Wanateolojia wetu wanasemaje kuhusu changamoto hii, na wanatoa mwogozo gani kwa watu walioathiriwa na mafundisho ya Kanisa kwa kiwango hiki?

Naomba kuwasilisha hoja, na wote karibuni "Simbawanga" Primary School ninakofundisha.

MAREJEO MUHIMU YALIYOTUMIKA

  1. Bertrand Russel, The Impact of Science in Society (New York: AMS Press, 1968
  2. Helena Matute, et al, Scientific thinking and Illusions of causality: How they bias our everyday thinking and how they could be reduced, Journal of Frontiers in Psychology 2015, vol. 6 (July), p. 1-14.7.
  3. John Hagen, "Science and the Church." The Catholic Encyclopedia. Vol. 13. New York: Robert Appleton Company, 1912. (Accessed on 09 Mar. 2021).
  4. Pope John Paul II, Fides et Ratio (1998)
  5. Wikipedia, Magical thinking (Accessed on 09 March 2021).
  6. Wikipedia, Color blindness (Accessed on 09 Marh 2021).
  7. J. Dmitri Gallow (2017), Seminar Notes for Causality (Accessed on 09 March 2021).
  8. Ian G. Barbour, Religion in Age of Science (Harper Collins e-Books, 1991). (ATTACHED BELOW)
  9. Keith Ward, God, Faith and the New Millennium: Christian Belief in an Age of Science (Oxford: One World Publications, 2002). (ATTACHED BELOW)
  10. Caleb W. Lack, Jacques Rousseau, Critical Thinking, Science, and Pseudoscience: Why We Can’t Trust Our Brains (Springer Publishing Company, 2016). (ATTACHED BELOW)

    Mama Amon,
    Shule ya Msingi 'Simbawanga',
    Mkoa wa 'Simbawanga',
    Andiko la: 09 March 2021.
    Maboresho ya hivi karibuni: 14 March 2021.

Huyu Padri alikuwa wapi wakati kanisa linakataa matumizi ya kondomu? Wataalamu walisema tutumie kondomu kujikinga, serikali ikasema hivyo pia, kanisa likasema hapana! Alikuwa wapi? Leo hii Corona ndo amejua maana ya wataalamu.
 
Kondomu inaashiria uzinifu asilimia 100% lakini barakoa ni kujikinga na vumbi na hewa chafu.
 
Kondomu inaashiria uzinifu asilimia 100% lakini barakoa ni kujikinga na vumbi na hewa chafu.
Kondomu anavaliwa nani? Mkeo? Kwa lengo gani? Kama ni kwa kuzuia mimba, poa. Hata hivyo zipo njia nyingine lukuki kwa lengo hilo. Kondomu si njia sahihi ya kujikinga na ukimwi. Njia sahihi ni A na B tu!
 
Padre alikiuka muongozo wa nchi kuhusu itifaki ya utoaji taarifa kuhusu ugonjwa wa UVIKO. Tiini mamlaka za nchi kwa maana nazo zimetoka kwa MUNGU WA MBINGUNI
Nakuunga mkono! Padre hana dhamana ya kutoa taarifa za ugonjwa wa corona na anajua hivyo. Huu ulikuwa ni UASI wa wazi kwa mamlaka ya nchi.
Kuasi mamlaka ya nchi ni kumwasi Mungu!! Wasome Biblia!
 
Nakuunga mkono! Padre hana dhamana ya kutoa taarifa za ugonjwa wa corona na anajua hivyo. Huu ulikuwa ni UASI wa wazi kwa mamlaka ya nchi.
Kuasi mamlaka ya nchi ni kumwasi Mungu!! Wasome Biblia!
mmmh
 
Kondomu inaashiria uzinifu asilimia 100% lakini barakoa ni kujikinga na vumbi na hewa chafu.
So what? Does it defeat science? what is the difference between uzinifu and vumbi na hewa in the hands of the laboratory? Another rubbish supporter.
 
Back
Top Bottom