Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni lazima mtu ambaye ana mapato alipe kodi iliyo sahihi aliye na kidogo alipe kidogo na aliye na kikubwa alipe kidogo, masikini kubeba mzigo mkubwa ni kutengeneza pengo kubwa kati ya waliyonacho na wasiyonachoWizara ya Fedha imetoa ufafanuzi kuhusu tozo ya miamala ya simu na benki Septemba Mosi, 2022 ikiwa ni siku kadhaa tangu kuibuka kwa malalamiko kutoka kwa wadau kuhusu gharama za huduma hizo za kifedha.
Waziri wa Fedha na Mipango - Mwigulu Nchemba
Chimbuko la tozo ilikuwa ni kwaajili ya kuunganisha nguvu kama watanzania ili tuweze kutekeleza baadhi ya mahitaji ya lazima kama madarasa, nyumba za walimu, ujenzi wa vituo vya afya, ununuzi wa vifaa tiba na ujenzi wa miundo mbinu ambayo yamekuwa yakekosa fedha kutokana na ufinyu wa bajeti.
Ufinyu wa bajeti umetokana na kuongezeka na majukumu ya msingi inayofanywa na serikari. Majukumu hayo ni kama miradi mikubwa kama bwawa la Mwalimu Nyerere, reli ya kisasa na maeneo mengine ni barabara, afya, elimu bure, mikopo elimu ya juu na umeme vijijini.
Kiwango cha tozo kilipunguzwa kutoka Tsh. 10,000/- mpaka Tsh. 7,000/- baada ya kupata maoni kutoka kwa watanzania kwamba tozo zimekubalika lakini zimeanzia kwa gharama ya juu sana. Lakini hii pia ikapunguzwa tena (na kwenye maeneo mengine) kutoka Tsh. 7,000/- mpaka Tsh, 4,000/- ili kuongeza wigo wa ushiriki ambapo ndiyo ilikuwa chimbuko la kwenda kwenye tozo za benki.
Nchi hii ni yetu na kila mtu yuko huru kutoa maoni akiona mambo hayaendi vizuri. Serikali imepokea maoni na itafanyia kazi swala la kutozwa mara mbili kwa fedha zinazo kuwa benki na swala la mpangaji kukusanya kodi ya jengo na kuipeleka kwenye mamlaka ya mapato badala ya mmiliki wa jengo.
Ni lazima mtu ambaye ana mapato alipe kodi iliyo sahihi aliye na kidogo alipe kidogo na aliye na kikubwa alipe kidogo, masikini kubeba mzigo mkubwa ni kutengeneza pengo kubwa kati ya waliyonacho na wasiyonacho.
Serikali inaendele kufanya uhakiki ili iweze kuongeza wigo wa tozo na kodi ambazo zitasaidia kupunguza mzigo kwa mtu mmoja mmoja.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Innocent Bashungwa
Tozo zimesaidia kuboresha sekta ya afya, elimu na barabara kwa kujenga vituo vya afya, madarasa na barabara vijijini na mijini, lakini pia kuongeza vifaa na watumishi.
Maswali na Majibu
Swali mwandishi DW: Miaka ya nyuma watanzania waliaminishwa kuwa Tanzania ni tajiri na inaweza kujiendesha yeneywe bila kutegemea tozo kutoka kwa wananchi je, utajiri huu wa Tanzania uliofanya Tanzania kujiendesha yenyewe umepotelea wapi?
Jibu Mwigulu Nchemba: Utajiri wa rasilimali usipozivuna utaendelea kuwa masikini, unakuwa na utajiri ila wewe ni masikini. Bila kuwekeza kwenye shughuli za uzalishaji tutaendelea kuwa masikini.
Tozo kuongezeka ni sababu mambo yanabadilika na mahitaji yanaongezeka, ambapo na bajeti pia lazima iongekezeke. Tozo ni moja ya chanzo kinachofanikisha kufikiwa kwa mahitaji hayo ya kibajeti.
Swali mwandishi Azam Tv: Mpango wa serikali kubana matumizi umefikia wapi? Gharama za maisha kupanda licha ya serikali kutoa ruzuku kwa maadhi ya maeneo tatizo ni nini?
Jibu Mwigulu Nchemba: Jitihata zinafanyika hapa ndani kuhakikisha inapunguza ukali wa maisha lakini chanzo kama Uviko-19 na vita bado vipo hivyo gharama zitaendelea kupanda mbali na jitihada zinazofanyika.
Hatua mbalimbali za kubana matumizi zimechukuliwa na ufafanuzi utatolewa kadri nafasi itakavyopatikana.
Wanatuchosha mnatuchoshaWizara ya Fedha imetoa ufafanuzi kuhusu tozo ya miamala ya simu na benki Septemba Mosi, 2022 ikiwa ni siku kadhaa tangu kuibuka kwa malalamiko kutoka kwa wadau kuhusu gharama za huduma hizo za kifedha.

Nikwasababu hakuna namna huwezi kukosa kununua sabuni ,unga au mkate kwa kuogopa vat utaishi vipiMbona kila bidhaa imewekewa vat na tunalipa?
Aliniacha hoi pale aliposema madeni ya taifa hayawahusu wananchi.Huyu ambaye anataka kuwa rais ni kama haelewi dunia inapoenda. IPO siku hizo tozo zitamuadhibu sana na atajuta. Anadhani anakomoa kumbe anajikomoa.
Sijui atawaambia nini watu huyu Rais wa mawe siku atataka kura.
Hatuna chombo mathubuti cha kusimamia kodi zetu ndio maana malalamiko ni mengi.Miradi ya maendeleo ni muhimu zaidi kuliko tutozo. Jamani tulipe kwa amani na upendo. Lakini tuwe wakali kwa watumishi wanaofuja pesa zetu na tupinge magari ya anasa V8. Ukiona V8 usisifie bali onesha kukerwa, ukiona mtumishi mwizi usimsifie bali muogope kama wezi wengine.
Yaani hapo kwenye kodi ya nyumba ndio niliona wamekusudia kabsa kumwangamiza mfanyabiashara mpangaji, kwani isingekuwa rahisi kuwapata wapangaji wasio na biashara rasmi yaani sio rahisi kumpata mpangaji alipe hiyo kodi kama hana tin na leseni, vilevile mwenye nyumba atakwambia nataka hela yangu kamili hautaki hamisha biashara yako, ni maumivu kwa wafanyabiashara na ninadhani jina la kubatiza hiyo tozo ili mfanyabiashara alipe bila kumgusa mwenye nyumba hilo jina limekosa.Tozo ziondoloewe! Watafute vyanzo vingine vya mapato. Hiyo miradi ya umeme na Standard gauge ijengwe kwa vyanzo vya mapato vilivyotumika tangu ilipoannzishwa. Hata ikichukua muda mrefu let's say 2025 - 2030 ni sawa tu. Wawaache wananchi waitumikiea serikali huku wakifanya maendeleo yao binafsi. Tuchukulie mfano watumishi wa serikali, mshahara unaingia benki tayari serikali imekata kodi, ukitoa unakatwa (ukibakiza hela uje utoe siku nyingine unakatwa tena), unalimpia pango unakatwa, unalipia umeme unakatwa, ukiwatumia wazazi kule kijjini unakatwa, benki nayo inakukata, mitandao ya simu nayo inakukata, ukienda kununua mahitaji ya nyumbani unakatwa kodi. Hata hii kodi ya nyumba waliweka vise versa ili kuwachanganya wananchi wakubali kuwepo kwa kodi hiyo ila iwepo kwa mwenye nyumba
Ni maneno tu ila kimsingi zote ni kodi.Tofautisha tozo na Kodi. Tax and levy. Kinachobishaniwa na wananchi Ni kwamba huwezi kuwa na Kodi na tozo at the same time.
Kwa nini asilalamike? Hujielewi. Aliyekuambia wanachama chochote lazima wakubaliane kila kitu ni nani?Halafu utakutana na mwana CCM kindaki ndaki nae yupo bize kulalamikia tozo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Msingi ulitaka ujengwe na mtu mwenye umri gani? Mnakera sanaHiyo misingi mnaijenga lini?.
Ukute wewe saa hizi una miaka 50+,halafu unaahidi ujenge misingi....
As if kondoo wewe utakuwa sparedNashauri tozo ziongezwe ndio njia pekee ya kuwaamsha makondoo yaliyolala fofofo kazi kugombea jezi za Simba na Yangu, wapuuzi kabisa.
Mwigulu kamatia hapohapo mpaka mazezeta yajitambuwe.
Unalalamika nini wakati viongozi 90% wanatokana na ccm? Huko kusema jambo la kitaifa ni kujifanya uko nao lkn mkikutana kwenye vikao vya chama mnakubaliana pamoja,Kwa nini asilalamike? Hujielewi. Aliyekuambia wanachama chochote lazima wakubaliane kila kitu ni nani?
Lonapokuja suala la kitaifa acheni upuuzi wa kuleta mambo ya uccm na uchadema.
Hapo sasamtoa ufafanuzi ni nani na anatokea wapi??? unawezaje kujikosoa au kujitolea ufafanuzi kwa uamzi wako mwenyewe