Tamthilia ya Huba haiendani na jina lake. Kinachoendelea ni upotoshaji na uhuni

Garbage in, Garbage out.

Mtunzi hana akili, Muigizaji hana akili, mtazamaji hana akili. Wanatengeneza kitu hakina akili na wakifurahia wakiwa hawana akili katika mazingira yasiyo na akili.

Nchi Haina dira ya kimaadili, watu wake wapo wapu tuu. Tunapenda kuhype ujinga hatuna uwezo wa kusoma, kufikiri na kung'amua mafunzo katika visa rahisi kabisa.

Wenzetu ukiwapa watu watano kitabu cha Kusadikika Cha S. Robert wanaweza kuja na masomo matano tofauti ya namna walivyokielewa. Sisi na uvivu wa fikra tunataka tuelewe namna Moja watu wote utadhani maroboti. ukijaribu kuelewa tofauti unakuwa mbaya na utapakwa matope.

Ni mentality hii inayosababisha changamoto. Tukikuza elimu mtoa mada, tutapata vitu vingi vizuri halafu na nyongeza. Usitegemee waongozaji Hawa wa elimu duni walete badiliko. Rejea Binti filamu mujaaarabu kabisa ikiandaliwa na wasomi na kuchezwa na wenye elimu ila utashangaa wala haikupata hype wala kufuatiliwa kwa kiasi ambacho ungetarajia..

Sasa hebu fanya kurudi kwenye ujinga uone [emoji23][emoji23][emoji23]. Lazima uwapate kwa wingi kwenye territory yao. Na media zinafanya biashara zishajua watu wake vizuri na zinawapa wanachoconsume. Uchambuzi uchwara wa mipira 24/7 na kufanya maigizo ya mediocre 2d presentation.

Pole Mtu wa Mungu.
Safari bado ni ndefu sana.
 
Hii kazi yao haina mvuto hata misamiati ya sanaa (literary jargon) hakuna, maneno mengi ni kama ya form one B wa kule kwetu Marendego.
Mkuu Mtibeli Taikon hivi main Character ni nani kwenye hiyo huba?
 
Ukipoteza asili utakuwa mtu wa kutangatanga.

Hatuna mavazi ya asili
Hatuna mziki wa asili
Sasa hata lugha za asili zinapotea

Kesho tutakuwa hatujui hata sisi ni Akina nani. Na hakuna anguko baya kama anguko linaloanzia ndani.

Aliyetudanganya kwamba tukijifunza utamaduni wa kiswahili tutupe wa asili alitumaliza.

Uswahili ni kama makande. Upo tu kwa sababu Makabila mamia haya yalikuwepo kama ilivyo kwa maharagwe na mahindi ndani ya makande.

Kama.maharagwe na mahindi sio muhimu kwenye makande basi hata makande si muhimu. Na ukipoteza mahindi na maharagwe basi kwa hakika hakuna makande.

Tunajikaamga kwenye mafuta yetu sisi wenyewe. And we we'll find out soooooon
 
Niliwahi kupiga soga na kiongozi mmoja ndani ya BASATA nikamuuliza Je wao wana miongozo ipi kuhusu uendelezaji wa lugha kupitia sanaa? Alichonijibu nilijikuta nimeshiba wakati nilikuwa nipo naelekea mgahawani kupata chakula. Yaani unakutana na vitu unstructured balaa kwenye visa, utadhani hakuna script ama maandalizi! Mkuu ni heri hata watuletee Misukosuko pamoja na Nsyuka tu!
 

Hivi J plus na Seba wapo wapi?
 
Hii kazi yao haina mvuto hata misamiati ya sanaa (literary jargon) hakuna, maneno mengi ni kama ya form one B wa kule kwetu Marendego.
Mkuu Mtibeli Taikon hivi main Character ni nani kwenye hiyo huba?

Mpaka sasa haieleweki. Lakini nahisi ni JB.
Hatujui amebeba dhamira gani kuu mpaka sasa hivi
 

Tumekwisha kwa mna hiyo.

Umalaya
Umbeya
Udaku
Wanaume kujifanya wanawake.
Kupenda Kitonga
Ndio maudhui
 
Mpaka sasa haieleweki. Lakini nahisi ni JB.
Hatujui amebeba dhamira gani kuu mpaka sasa hivi
Yaani miaka mitatu muhusika mkuu hajulikani, mwanzoni pale nilihisi Devi na Tima lakini kadri siku zilivyosonga nikawa sielewi nikaona bora kuachia wengine waangalie.
Waige walau kwa Wahindi kazi zao safi na nyingi unaweza kukaa na watoto mkaangalia bila tabu.
 

Umesema vizuri sana mkuu.

Kwa sasa lengo la sanaa ni kuonyesha mitindo ya uvaaji, ususi na unyoaji wa nywele.
 
Ni heri nitazame Naagin au Baalveer lakini sio hizi tamthilia pasua kichwa 😀
 
Mtu na akili timamu,unayejielewa huwezi kukaa ukaangalia vipindi hivyo
Sijui matamthilia hayo

Ova
 

Devi na tima
Devi na Kibibi
Devi na Nelly
Umalaya mtupu.

JB na Tesa
JB na Tima
JB na Jenifer
Na sasa inaenda JB na MKE wa kashaulo.
Umalaya mtupu.

Tesa na JB
Tesa na mwanaye (Sijui anaitwa nani)
Umalaya mtupu

Kinyaiya na Tima
Kinyaiya na yule dada mwenye msambwanda,
Umalaya mtupu.

Kibibi na Devi
Kibibi na Chid
Kibibi na Badi boy
Umalaya mtupu.
 
Halafu kiingereza kingi na ni broken hatari! Unakutana na jitu linahubiri utamaduni wa mtu mwingine na kuacha wake. Badala hata ya kuonesha utamaduni wetu wao wapo busy kuonesha ni nani anavaa suti ya Gucci au Prada a kusuka Brazilian Hair....................... Na BASATA wapo sijui kazi yao ni nn tu?
 
Edward
View attachment 2843045
Miamba hawa wapo wanapiga ishu zao kitaa ila Seba amekonda sana sijui shida ni nn.
Jimmy Mponda yupo na Mzimuni Theatre Arts wanaendeleza mishe mishe

Filamu ya misukosuko ukiitazama hata kama imeigizwa kipindi kile bado inauzito na ubora wa kiwango cha juu.

Wanaweza kuirudia tena ile filamu kipindi hiki teknolojia ikiwa imekua.
Kama kuna maboresho wanaweza kuongeza ongeza au kupunguza baadhi ya ishu.

Hao wakiigiza hakunaga kulamba midomo au kutikisa tikisa makalio kama Wapuuzi.
 

BASATA hawajui nini wanatakiwa kufanya kwenye Jamii
 
Tumekwisha kwa mna hiyo.

Umalaya
Umbeya
Udaku
Wanaume kujifanya wanawake.
Kupenda Kitonga
Ndio maudhui
Ukitaka.kujua ujinga wao we muulize lengo kuu la yeye kufanya tamthilia zenye maudhuo haya ni nini!? Nakuhakikishia hajui kwenye hadhira yake anataka kufanikisha nini.

Kabla haujamuhukumu, waylize serikali na Viongozi wake wanapopitisha sera yoyote kama wameisoma na wameielewa na wanadhani italeta badiliko Gani ndani ya Mtanzania mmoja mmoja?! Hakutakuwa na jibu

Halafu nenda umuulize mwalimu anapofundisha Darasa... Anadhani anachofundisha alaenga kiwe na athari ipi chanya katika maisha ya mwanafunzi moja mmoja.. ukiachilia mbali yeye kufaulu mitihani?! Hawezi kuwa na jibu.

Toka nenda kamuulize mzazi..anapomfunza mtoto mafunzo aliyoyachagua..anatarajia yalete impact ipi kwa mtoto hapo baadae..katika mia labda wawili tu ndio watakupa maelezo ya kuridhisha.

Kwa kifupi maisha ya Watanzania wengi kwa ngazi zote ni maisha ya kubeti maisha ya kimachinga. Unapapasa papasa ukibahatika Alhamduliah. Ukikosa basi Insh'allah. Hakuna Nia ya dhati ya kupanga na kujitahidi kufuata njia.

Athari za mfumo huo unaziona kwenye elimu mtoto anapelekwa alikofaulu..wakati mmingine ni fluke tuu. Na inturn imetufanya hatujui tunataka kufanya nini mpaka tufeli..maana Hata ukitaka mwisho utakwenda ulipopangiwa tuu.

Tunajenga hovyo hovyo maana hatuna mpango thabiti. Tukibahatisha hapo hapo tunajenga .. mwendelezo wa kubeti. Ukiwatazama bodaboda barabarani na ujinga yao unaweza kudhani ni wao tuu ila mfumo wao na tabia zao barabarani ndizo tabia za Watanzania asilimia 98. Tunakwenda una upepo na upenyo.. ikitolea umefinywa.. umekufa na mengine kama hayo basi ni bahati mbaya.

Haya ya umbeya ujinga nk.. ni reflection ya kinachoendelea mitaani.. ila mtunzi hatujui lengo lake la kutuonesha ni nini.. tujifunze tuwe wambea ,wanafiki, wezi na mashoga? Au ayapinga haya?! Kwa kifupi sioni wanachotaka ku-achieve.. na Hadith isiyokuwa na lengo ni kelele tuu.

Hili ni la BASATA.. lakini ngoja Je BASATA wana kichujio cha maudhui?! Wanakitoa.wapi kama taifa halina dira ya Maadili?!

Mungu Aendelee kukulinda Mtoa Mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…