Tamthilia ya Huba haiendani na jina lake. Kinachoendelea ni upotoshaji na uhuni

Tamthilia ya Huba haiendani na jina lake. Kinachoendelea ni upotoshaji na uhuni

TAMTHILIA YA HUBA HAIENDANI NA JINA LAKE. KINACHOENDELEA NI UPOTOSHAJI NA UHUNI TUU.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Wanafilamu wengi walikuwa wakilalamika hakuna wawekezaji katika tasnia ya filamu ndio maana kazi zinazotoka ni mbofumbofu. Miaka ya hivi karibuni kumetokea mabadiliko kidogo yenye matumaini katika tasnia hii baada ya dunia kuhama kutoka analojia kwenda dijitali. Uwepo wa Dstv na makampuni mengine umekuwa kichocheo cha ukuaji wa tasnia ya uigizaji hapa nchi.

Wawekezaji haitakuwa kisingizio tena. Watanzania walitarajia kuona kazi nzuri zenye kupendeza, zenye kusisimua, utunzi wenye ubunifu wa kipekee, tamthilia zenye mipangilio ya visa, matukio na maneno ya kisanaa yenye kuleta akili mpya ndani ya jamii.
Lakini Taikon ninasikitika kuwa bado kuna ombwe kubwa katika Filamu zetu.

Ukiangalia uigizaji wa wasanii wetu hauna tofauti na ule uliokuwa unafanyika sekondari. Yaani ni kama watoto wadogo hivi ambao wanaigiza Kibabababa na kimamamama.

Ninaamini Waigizaji hawana makosa kwa sababu muigizaji anaigiza kulingana na mtunzi na muongozaji atavyotaka filamu ichezwe. Tatizo kubwa la Tasnia ya filamu hapa nchini ipo kwa Watunzi na waongozaji wa filamu.
Uwezo wa Watunzi upo chini sana. Mtunzi ndiye chanzo cha Filamu. Yeye ndiye anayeandaa kisa, matukio, wahusika, mandhari nzuri.k.
Muongozaji wa filamu ambaye pia anaweza kuwa mtunzi yeye kazi yake ni kuwa katika ulimwengu halisi na kuchagua wahusika na mandhari halisi inayoendana na simulizi ya mtunzi hata kama ni ya kubuni. Muongozaji wa filamu lazima amuelewe mtunzi alikuwa anapicha gani kichwani mwake katika stori yake. Ndio maana inashauriwa kama mtunzi yupo ni bora muongozaji wa filamu amshirikishe ili filamu itoke kama ilivyokusudiwa.

Tuachane na mambo hayo. Turudi kwenye mada.

1. Filamu za Bongo zinatatizo la misconceptions.
Nafikiri hii inatokana na watanzania wengi pia kuwa na tatizo hili.
Wabongo wengi tunatatizo la misconceptions katika baadhi ya ishu. Mfano wabongo wengi wanashindwa kutofautisha kati ya heshima na Woga.
Sio ajabu ukamsikia mtu akisema ukiwa na pesa unaheshimika wakati heshima inatokana na matendo yenye heshima, maadili mema. Badala ya kusema ukiwa na pesa unaogopeka.

Upendo Vs Tamaa.
Watanzania wengi wanashindwa kutofautisha kati ya upendo na tamaa. Na hiki ndicho kinachojitokeza kwenye filamu ya huna.
Huba kwa lugha nyingine huitwa upendo "mapenzi ya dhati" ambapo pakiwa na huba automatically hakuwezi kuwa usaliti.

Lakini ukitazama kwenye tamthilia ya huba kuna hiyo misconception ya kuchanganya huba na tamaa.
Mtunzi anafikiria kila mapenzi ni HUBA. Wakati mapenzi yasiyo ya dhati huitwa tamaa. Na mapenzi ya kweli ndio huitwa HUBA.

Ukifuatilia kinachoendelea kwenye tamthilia hiyo utagundua kinachoendelea ni umalaya, uhuni na tamaa mbaya. Na wala hakuna kitu kinachoitwa Huba kama jina la tamthilia lilivyo.

Umalaya, uchafu, na uasherati uliovuka mipaka ndicho kinachoendelea humo ambapo ni kinyume cha Huba. Kuchukuliana Mabwana, kuchukuliana Wake.
Mara Mama anatoka na Kijana wake wakiume.
Mara Baba "JB" anatoka na Mke wa Mkwe wake "Tima" yaani uchafu uchafu tuu. Filamu inanuka uchafu tuu. Hakuna huba hata sehemu moja.

2. Kuwajibika kisheria hakuna.
Mtu kafanya uhalifu kwa mfano kaua au kateka. Mtunzi hajaandaa kisa cha namna ya kushughulikia wahalifu katika simulizi yake.
Jambo hilo limejitokeza pia katika tamthilia ya wimbi. Tukio la utekaji limetokea, hiyo ni jinai ni lazima mtunzi angeandaa wahusika wengine wa kisheria kama polisi wakifuatilia tukio hilo.
Haya huku kwenye tamthilia ya Huba, Mke wa JB aliuawa, lakini ufuatiliaji wake hauridhishi ni kama kesi imetekelezwa hewani.

Angalau Pazia walijitahidi kwenye kipengele hiki.
Mnashindwa na Wakenya kama kwenye Semina, Kovu, n.k.
Mtunzi lazima ukishatunga kisa cha uhalifu lazima jicho lako na kalamu yako iwe kali mno kuhakikisha unaandaa tukio jingine mbele kumuadhibu mhalifu na kuleta madhara makubwa yatokanayo na huo uhalifu ili jamii ijifunze kuwa uhalifu sio mzuri. Watu waogope.

Lakini ninyi mnafundisha Watu umalaya, kudanga, kufanya uasherati. Yaani mawazo kama watoto wanaobalehe Balehe hivi muda wote kuwaza mapenzi tena katika namna nyepesi kabisa.

Ati huyu kamtongozo huyu kisha Kalala naye, kisha kumfuata tena Dadaake Kalala naye, mara Kalala na mama yake.
Mara mkwe na mkwe wanalalana tena. Mpaka unajiuliza hivi haya mambo yanafanywa na watu wenye akili timamu kweli.
Tena bila aibu yapo live nchi nzima Watu waone kuwa Watanzania ni wajinga kwa kiwango hiki.

Badilikeni bhana!

3. Ubunifu katika Visa hakuna.
Ubunifu wa migogoro hakuna hata unajiuliza hivi tamthilia maana yake nini. Yaani unakuta kipande kizima kinaenda Watu wanajizungusha zungusha tuu.

Alafu kuna ile kasumba mbaya ya kudhani kupiga piga kelele na kutupiana maneno makali ati ndio migogoro. Embu acheni hizo.

Kwa mfano kwenye filamu ya Huba mgogoro ambao ungevutia zaidi ni ule wa kuchunguza nani aliyemuua mke wa JB?
Mhusika mmoja anafuatilia kuhakikisha muuaji anapatikana mhusika mwingine anakazana kuficha.
Upande mwingine mgogoro mwingine wa kuchunguza mali za JB zinatokana na nini na sio iishie tuu kwenye mambo ya kishirikina, kusadikika ambayo hayana uhalisia.

Haya athari za baba na mama kuachana lazima mgogoro mwingine ungezuka kwa kuonyesha jinsi watoto wanavyopata tabu, na lazima watoto wapewe kipande wacheze.

Kwa vile jina la tamthilia ni HUBA, lazima kuna wahusika wawili ambao wangekuwa wanapendana sana kiasi kwamba nguvu ya mapenzi ingeonekana.
Wengine wanajaribu kuyasukasuka hayo mahusiano na kuyateteresha lakini wahusika hao ( love birds) wanapitia hizo changamoto lakini wanashinda majaribu.
Hivyo ndivyo mambo yanavyoenda.

Sasa ushasema Huba alafu muda huohuo unaonyesha nguvu ya Pesa kwamba pesa inaweza kuvunja Huba. Hii haipo hivyo. Labda kama huba yenye maana ya kudanga hapo sawa.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Garbage in, Garbage out.

Mtunzi hana akili, Muigizaji hana akili, mtazamaji hana akili. Wanatengeneza kitu hakina akili na wakifurahia wakiwa hawana akili katika mazingira yasiyo na akili.

Nchi Haina dira ya kimaadili, watu wake wapo wapu tuu. Tunapenda kuhype ujinga hatuna uwezo wa kusoma, kufikiri na kung'amua mafunzo katika visa rahisi kabisa.

Wenzetu ukiwapa watu watano kitabu cha Kusadikika Cha S. Robert wanaweza kuja na masomo matano tofauti ya namna walivyokielewa. Sisi na uvivu wa fikra tunataka tuelewe namna Moja watu wote utadhani maroboti. ukijaribu kuelewa tofauti unakuwa mbaya na utapakwa matope.

Ni mentality hii inayosababisha changamoto. Tukikuza elimu mtoa mada, tutapata vitu vingi vizuri halafu na nyongeza. Usitegemee waongozaji Hawa wa elimu duni walete badiliko. Rejea Binti filamu mujaaarabu kabisa ikiandaliwa na wasomi na kuchezwa na wenye elimu ila utashangaa wala haikupata hype wala kufuatiliwa kwa kiasi ambacho ungetarajia..

Sasa hebu fanya kurudi kwenye ujinga uone [emoji23][emoji23][emoji23]. Lazima uwapate kwa wingi kwenye territory yao. Na media zinafanya biashara zishajua watu wake vizuri na zinawapa wanachoconsume. Uchambuzi uchwara wa mipira 24/7 na kufanya maigizo ya mediocre 2d presentation.

Pole Mtu wa Mungu.
Safari bado ni ndefu sana.
 
Habarini Wakuu!
Naomba Nichangie mada kama ifuatavyo,
Maoni yangu yanaweza kumkera mtu ila mtanisamehe sana!

Filamu na tamthilia mbali tu na kutuburudisha zinatakiwa zitusaidie kujifunza zaidi na kuweka umakini kwenye mambo ya msingi kwa njia ambayo ni rahisi. Filamu na tamthilia zina dhima na lengo kubwa kwa jamii kwani zinaweza kuvunja mawazo magumu na kuyafanya yawe rahisi kwa watu kuelewa kwa muda mfupi.

Ukitazama fikra za waanzilishi wa mwanzo wa picha mjongeo kabsa, wafaransa hawa Louis Le Prince, Alice Guy-Blaché, pamoja na Georges Méliès miaka ya 1887 hivi ilikuwa ni kuonesha dunia picha ambazo zitatumika kuelimisha na kuonesha mabadiliko ndani ya jamii. Ukija kwa kina Aaron Sorkin, pamoja na Quentin Jerome Tarantino wanajua kuwa kuandika visa na Mikasa ya filamu na tamthilia ni sayansi na pia ni sanaa haswa.

Tamthilia kama ya Roots ama Exterminate All the Brutes ndo zina mafundisho, ingawa zimeuzwa sana duniani ila ndani yake kuna vitu vingi vya kujifunza. Kuna wakati nilikuwa nafuatilia sana tamthilia mbili za Azam, tamthilia ya Sultana pamoja na Ottoman.

Kwa Waturuki wanaitambua kama tamthilia ya Muhteşem Yüzyıl ama tamthilia ya Rise of Empires: Ottoman ambazo zote zinaonesha ushujaa wa watawala wa Ottoman nyakati hizo. Mehmed VI na ndugu zake waliopita kabla yake. Unadhani NBC pamoja na Sony Pictures Television walikuwa ni wapumbavu kutengeneza tamthilia ya Law & Order: Special Victims Unit au The Blacklist wala sio hivyo, walijua kuwa kupitia tamthilia hizi jamii itajifunza mengi, Jiulize kwanini tamthilia ya 24 yaani kituo kikubwa kama FOX ambacho kilikuwa kikuvuna 7515000000 pesa za madafu kwa dakika thelathini tu, kwanini Bwana Lachlan Murdoch alikubali kuachana na kutengeneza tamthilia ya 24. Uliza wakuu wakupe majibu!??

Sasa hivi Azam kuna tamthilia ya Barbaros: Sword of the Mediterranean kwa Bongo tunaiita kwa jina la Barbarossa tamthilia hii ina kisa cha kihistoria kutoka Uturuki, halafu huko huko Wabongo tuna tamthilia yetu ya Lolita pamoja na Siri, watu wanaishi maisha dhahania na visa vya kububa tu, aisee Tanzania yangu bhana! Hivi hata kama ni wewe utaangalia tamthilia ipi hapo??

Watafuteni hata Amil Shivji au Seko Shamte!

Ngoja tuache mvua inyeshe tuone wapi panavuja
Ukipoteza asili utakuwa mtu wa kutangatanga.

Hatuna mavazi ya asili
Hatuna mziki wa asili
Sasa hata lugha za asili zinapotea

Kesho tutakuwa hatujui hata sisi ni Akina nani. Na hakuna anguko baya kama anguko linaloanzia ndani.

Aliyetudanganya kwamba tukijifunza utamaduni wa kiswahili tutupe wa asili alitumaliza.

Uswahili ni kama makande. Upo tu kwa sababu Makabila mamia haya yalikuwepo kama ilivyo kwa maharagwe na mahindi ndani ya makande.

Kama.maharagwe na mahindi sio muhimu kwenye makande basi hata makande si muhimu. Na ukipoteza mahindi na maharagwe basi kwa hakika hakuna makande.

Tunajikaamga kwenye mafuta yetu sisi wenyewe. And we we'll find out soooooon
 
Niliwahi kupiga soga na kiongozi mmoja ndani ya BASATA nikamuuliza Je wao wana miongozo ipi kuhusu uendelezaji wa lugha kupitia sanaa? Alichonijibu nilijikuta nimeshiba wakati nilikuwa nipo naelekea mgahawani kupata chakula. Yaani unakutana na vitu unstructured balaa kwenye visa, utadhani hakuna script ama maandalizi! Mkuu ni heri hata watuletee Misukosuko pamoja na Nsyuka tu!
 
Hivi J plus na Seba wapo wapi?
 
Hii kazi yao haina mvuto hata misamiati ya sanaa (literary jargon) hakuna, maneno mengi ni kama ya form one B wa kule kwetu Marendego.
Mkuu Mtibeli Taikon hivi main Character ni nani kwenye hiyo huba?

Mpaka sasa haieleweki. Lakini nahisi ni JB.
Hatujui amebeba dhamira gani kuu mpaka sasa hivi
 
Garbage in, Garbage out.

Mtunzi hana akili, Muigizaji hana akili, mtazamaji hana akili. Wanatengeneza kitu hakina akili na wakifurahia wakiwa hawana akili katika mazingira yasiyo na akili.

Nchi Haina dira ya kimaadili, watu wake wapo wapu tuu. Tunapenda kuhype ujinga hatuna uwezo wa kusoma, kufikiri na kung'amua mafunzo katika visa rahisi kabisa.

Wenzetu ukiwapa watu watano kitabu cha Kusadikika Cha S. Robert wanaweza kuja na masomo matano tofauti ya namna walivyokielewa. Sisi na uvivu wa fikra tunataka tuelewe namna Moja watu wote utadhani maroboti. ukijaribu kuelewa tofauti unakuwa mbaya na utapakwa matope.

Ni mentality hii inayosababisha changamoto. Tukikuza elimu mtoa mada, tutapata vitu vingi vizuri halafu na nyongeza. Usitegemee waongozaji Hawa wa elimu duni walete badiliko. Rejea Binti filamu mujaaarabu kabisa ikiandaliwa na wasomi na kuchezwa na wenye elimu ila utashangaa wala haikupata hype wala kufuatiliwa kwa kiasi ambacho ungetarajia..

Sasa hebu fanya kurudi kwenye ujinga uone [emoji23][emoji23][emoji23]. Lazima uwapate kwa wingi kwenye territory yao. Na media zinafanya biashara zishajua watu wake vizuri na zinawapa wanachoconsume. Uchambuzi uchwara wa mipira 24/7 na kufanya maigizo ya mediocre 2d presentation.

Pole Mtu wa Mungu.
Safari bado ni ndefu sana.

Tumekwisha kwa mna hiyo.

Umalaya
Umbeya
Udaku
Wanaume kujifanya wanawake.
Kupenda Kitonga
Ndio maudhui
 
Mpaka sasa haieleweki. Lakini nahisi ni JB.
Hatujui amebeba dhamira gani kuu mpaka sasa hivi
Yaani miaka mitatu muhusika mkuu hajulikani, mwanzoni pale nilihisi Devi na Tima lakini kadri siku zilivyosonga nikawa sielewi nikaona bora kuachia wengine waangalie.
Waige walau kwa Wahindi kazi zao safi na nyingi unaweza kukaa na watoto mkaangalia bila tabu.
 
Habarini Wakuu!
Naomba Nichangie mada kama ifuatavyo,
Maoni yangu yanaweza kumkera mtu ila mtanisamehe sana!

Filamu na tamthilia mbali tu na kutuburudisha zinatakiwa zitusaidie kujifunza zaidi na kuweka umakini kwenye mambo ya msingi kwa njia ambayo ni rahisi. Filamu na tamthilia zina dhima na lengo kubwa kwa jamii kwani zinaweza kuvunja mawazo magumu na kuyafanya yawe rahisi kwa watu kuelewa kwa muda mfupi.

Ukitazama fikra za waanzilishi wa mwanzo wa picha mjongeo kabsa, wafaransa hawa Louis Le Prince, Alice Guy-Blaché, pamoja na Georges Méliès miaka ya 1887 hivi ilikuwa ni kuonesha dunia picha ambazo zitatumika kuelimisha na kuonesha mabadiliko ndani ya jamii. Ukija kwa kina Aaron Sorkin, pamoja na Quentin Jerome Tarantino wanajua kuwa kuandika visa na Mikasa ya filamu na tamthilia ni sayansi na pia ni sanaa haswa.

Tamthilia kama ya Roots ama Exterminate All the Brutes ndo zina mafundisho, ingawa zimeuzwa sana duniani ila ndani yake kuna vitu vingi vya kujifunza. Kuna wakati nilikuwa nafuatilia sana tamthilia mbili za Azam, tamthilia ya Sultana pamoja na Ottoman.

Kwa Waturuki wanaitambua kama tamthilia ya Muhteşem Yüzyıl ama tamthilia ya Rise of Empires: Ottoman ambazo zote zinaonesha ushujaa wa watawala wa Ottoman nyakati hizo. Mehmed VI na ndugu zake waliopita kabla yake. Unadhani NBC pamoja na Sony Pictures Television walikuwa ni wapumbavu kutengeneza tamthilia ya Law & Order: Special Victims Unit au The Blacklist wala sio hivyo, walijua kuwa kupitia tamthilia hizi jamii itajifunza mengi, Jiulize kwanini tamthilia ya 24 yaani kituo kikubwa kama FOX ambacho kilikuwa kikuvuna 7515000000 pesa za madafu kwa dakika thelathini tu, kwanini Bwana Lachlan Murdoch alikubali kuachana na kutengeneza tamthilia ya 24. Uliza wakuu wakupe majibu!??

Sasa hivi Azam kuna tamthilia ya Barbaros: Sword of the Mediterranean kwa Bongo tunaiita kwa jina la Barbarossa tamthilia hii ina kisa cha kihistoria kutoka Uturuki, halafu huko huko Wabongo tuna tamthilia yetu ya Lolita pamoja na Siri, watu wanaishi maisha dhahania na visa vya kububa tu, aisee Tanzania yangu bhana! Hivi hata kama ni wewe utaangalia tamthilia ipi hapo??

Watafuteni hata Amil Shivji au Seko Shamte!

Ngoja tuache mvua inyeshe tuone wapi panavuja

Umesema vizuri sana mkuu.

Kwa sasa lengo la sanaa ni kuonyesha mitindo ya uvaaji, ususi na unyoaji wa nywele.
 
Hivi J plus na Seba wapo wapi?

1702623306372.png

Miamba hawa wapo wanapiga ishu zao kitaa ila Seba amekonda sana sijui shida ni nn.
Jimmy Mponda yupo na Mzimuni Theatre Arts wanaendeleza mishe mishe
 
Yaani miaka mitatu muhusika mkuu hajulikani, mwanzoni pale nilihisi Devi na Tima lakini kadri siku zilivyosonga nikawa sielewi nikaona bora kuachia wengine waangalie.
Waige walau kwa Wahindi kazi zao safi na nyingi unaweza kukaa na watoto mkaangalia bila tabu.
Ni heri nitazame Naagin au Baalveer lakini sio hizi tamthilia pasua kichwa 😀
 
Ukipoteza asili utakuwa mtu wa kutangatanga.

Hatuna mavazi ya asili
Hatuna mziki wa asili
Sasa hata lugha za asili zinapotea

Kesho tutakuwa hatujui hata sisi ni Akina nani. Na hakuna anguko baya kama anguko linaloanzia ndani.

Aliyetudanganya kwamba tukijifunza utamaduni wa kiswahili tutupe wa asili alitumaliza.

Uswahili ni kama makande. Upo tu kwa sababu Makabila mamia haya yalikuwepo kama ilivyo kwa maharagwe na mahindi ndani ya makande.

Kama.maharagwe na mahindi sio muhimu kwenye makande basi hata makande si muhimu. Na ukipoteza mahindi na maharagwe basi kwa hakika hakuna makande.

Tunajikaamga kwenye mafuta yetu sisi wenyewe. And we we'll find out soooooon
Mtu na akili timamu,unayejielewa huwezi kukaa ukaangalia vipindi hivyo
Sijui matamthilia hayo

Ova
 
Yaani miaka mitatu muhusika mkuu hajulikani, mwanzoni pale nilihisi Devi na Tima lakini kadri siku zilivyosonga nikawa sielewi nikaona bora kuachia wengine waangalie.
Waige walau kwa Wahindi kazi zao safi na nyingi unaweza kukaa na watoto mkaangalia bila tabu.

Devi na tima
Devi na Kibibi
Devi na Nelly
Umalaya mtupu.

JB na Tesa
JB na Tima
JB na Jenifer
Na sasa inaenda JB na MKE wa kashaulo.
Umalaya mtupu.

Tesa na JB
Tesa na mwanaye (Sijui anaitwa nani)
Umalaya mtupu

Kinyaiya na Tima
Kinyaiya na yule dada mwenye msambwanda,
Umalaya mtupu.

Kibibi na Devi
Kibibi na Chid
Kibibi na Badi boy

Halafu kiingereza kingi na ni broken hatari! Unakutana na jitu linahubiri utamaduni wa mtu mwingine na kuacha wake. Badala hata ya kuonesha utamaduni wetu wao wapo busy kuonesha ni nani anavaa suti ya Gucci au Prada a kusuka Brazilian Hair....................... Na BASATA wapo sijui kazi yao ni nn tu?
 
Edward
View attachment 2843045
Miamba hawa wapo wanapiga ishu zao kitaa ila Seba amekonda sana sijui shida ni nn.
Jimmy Mponda yupo na Mzimuni Theatre Arts wanaendeleza mishe mishe

Filamu ya misukosuko ukiitazama hata kama imeigizwa kipindi kile bado inauzito na ubora wa kiwango cha juu.

Wanaweza kuirudia tena ile filamu kipindi hiki teknolojia ikiwa imekua.
Kama kuna maboresho wanaweza kuongeza ongeza au kupunguza baadhi ya ishu.

Hao wakiigiza hakunaga kulamba midomo au kutikisa tikisa makalio kama Wapuuzi.
 
Halafu kiingereza kingi na ni broken hatari! Unakutana na jitu linahubiri utamaduni wa mtu mwingine na kuacha wake. Badala hata ya kuonesha utamaduni wetu wao wapo busy kuonesha ni nani anavaa suti ya Gucci au Prada a kusuka Brazilian Hair....................... Na BASATA wapo sijui kazi yao ni nn tu?

BASATA hawajui nini wanatakiwa kufanya kwenye Jamii
 
Tumekwisha kwa mna hiyo.

Umalaya
Umbeya
Udaku
Wanaume kujifanya wanawake.
Kupenda Kitonga
Ndio maudhui
Ukitaka.kujua ujinga wao we muulize lengo kuu la yeye kufanya tamthilia zenye maudhuo haya ni nini!? Nakuhakikishia hajui kwenye hadhira yake anataka kufanikisha nini.

Kabla haujamuhukumu, waylize serikali na Viongozi wake wanapopitisha sera yoyote kama wameisoma na wameielewa na wanadhani italeta badiliko Gani ndani ya Mtanzania mmoja mmoja?! Hakutakuwa na jibu

Halafu nenda umuulize mwalimu anapofundisha Darasa... Anadhani anachofundisha alaenga kiwe na athari ipi chanya katika maisha ya mwanafunzi moja mmoja.. ukiachilia mbali yeye kufaulu mitihani?! Hawezi kuwa na jibu.

Toka nenda kamuulize mzazi..anapomfunza mtoto mafunzo aliyoyachagua..anatarajia yalete impact ipi kwa mtoto hapo baadae..katika mia labda wawili tu ndio watakupa maelezo ya kuridhisha.

Kwa kifupi maisha ya Watanzania wengi kwa ngazi zote ni maisha ya kubeti maisha ya kimachinga. Unapapasa papasa ukibahatika Alhamduliah. Ukikosa basi Insh'allah. Hakuna Nia ya dhati ya kupanga na kujitahidi kufuata njia.

Athari za mfumo huo unaziona kwenye elimu mtoto anapelekwa alikofaulu..wakati mmingine ni fluke tuu. Na inturn imetufanya hatujui tunataka kufanya nini mpaka tufeli..maana Hata ukitaka mwisho utakwenda ulipopangiwa tuu.

Tunajenga hovyo hovyo maana hatuna mpango thabiti. Tukibahatisha hapo hapo tunajenga .. mwendelezo wa kubeti. Ukiwatazama bodaboda barabarani na ujinga yao unaweza kudhani ni wao tuu ila mfumo wao na tabia zao barabarani ndizo tabia za Watanzania asilimia 98. Tunakwenda una upepo na upenyo.. ikitolea umefinywa.. umekufa na mengine kama hayo basi ni bahati mbaya.

Haya ya umbeya ujinga nk.. ni reflection ya kinachoendelea mitaani.. ila mtunzi hatujui lengo lake la kutuonesha ni nini.. tujifunze tuwe wambea ,wanafiki, wezi na mashoga? Au ayapinga haya?! Kwa kifupi sioni wanachotaka ku-achieve.. na Hadith isiyokuwa na lengo ni kelele tuu.

Hili ni la BASATA.. lakini ngoja Je BASATA wana kichujio cha maudhui?! Wanakitoa.wapi kama taifa halina dira ya Maadili?!

Mungu Aendelee kukulinda Mtoa Mada.
 
Back
Top Bottom