Tamu na chungu ya safari yangu ya Agosti 24, 2023 Kutoka Kahama kwenda Dar es Salaam

Shukuru kufika angalau saa 11 alfajiri kuna wengi walilala palepale mpaka asubuhi.
 
Mbeya-Tanga 2018/2019 nilipanda chuma inaitwa Mbeya City. Tulisafiri siku mbili[emoji23] gari imejaza magunia kwenye corridor. Gear inatafutwa mara mbilimbili[emoji1430] kuna makampuni ya mabasi yanafanya majaribio kwenye roho za watu
 
Siku niliyolipanda Champion, nilishukia Chalinze. Yaani basi halina breki🙄
 
Bora nipande coster hizi private jion kuliko kupanda basi lisilieleweka,mara ya mwisho nimesafiri na Costa kutoka khm to Dar ,nimetoka 10 jion nimefika dar sa 3 asubuhi
 
Kwamba basi kama😂😂😂
 
Mkuu unachoongea ni kweli kabisa kwakuwa Mimi ilinitokea kwa mwaka Jana hapohapo kahama. Nilikata tickets kwa jina la bus jingine asubuhi naambiwa Hilo bus limeharibika kwa hiyo nimefaulishwa nipande dreamline.... Aseee kahama uhuni Mwingi Sana.
 
safari ya kulitafuta jiji la Mkuu wa Mkoa mwenye Maneno mengi, mropokaji na mcheshi ilianza.
Huyu sio mwingine bali ni Challamila sio Rehema Challamila Ray C ila ni Challamila hivyo hivyo yule mkuu wa Mkoa anaepambana na wadangaji jijini Dasalama
 
Hiyo Kampuni ya Dream line ni ya kipumbavu mno!

Ulicho eleza nami kilinikuta siku moja na hilo Bus la Dream liner!

Nikiwa nimefika hapo KAHAMA nikitokea Masumbwe nikakosa tiketi ya Frester na Satco akaja Kijana mmoja akamishawishi Kukata Bus la Dream Liner kwenda Dar!

Kesho yake asbh nilijuta nilipofika Bus Stand!
Bus lilipaswa kuondoka saa 12 asbh lakini tuliondoka karibia saa 3!

Traffic Police kumbe walishalijua Hilo Bus, ilipofika muda wa kuondoka Traffic Police akaja kwa ajili ya ukaguzi akasema matairi ya Hilo gari ni mabovu na gari ipelekwe kituo cha police!

Kwakweli siku hiyo tulisota na wafanyakazi wa Hilo gari hawajali, Kauli zao mbovu na gari ni chafu kupindukia!

Kwa ufupi Dream Liner siyo Kampuni ya Usafirishaji ya maana hata kidogo!
 
Wana ki-gereji chao bubu maeneo ya area c mbele ya town campus ya chuo cha hombolo, fika pale ujionee yanavyopigwa nyundo na mafundi mchundo, halafu cha ajabu wale mabwana kuanzia madereva, wahudumu wa mabasi,wakata tiketi mpaka hawa mafundi wote ni kabila moja WARANGI ukifika pale ni mwendo wa kutafuna mirungi na kuongea kilugha chao
 
Na huo ukabila pia umechangia pakubwa kuwa hivyo walivyo.
 
Huko kahama kuna majina mazuri ya magari ila mgari yenyewe yamechoka hadi hayastahili kuitwa majina hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…