Nimekuwa nikisoma hayo maneno bila kuelewa!
Hebu nisaidie mnakuwa na maana gani kusema watafute fedha linapokuja swala la wanawake?
PESA ndiyo sabuni ya roho.
Pesa ni kichocheo cha furaha.
Ukiwa na pesa unajiamimi.
Unaweza kufanya unalotaka kandri ya uwezo wako.
Ndiyo maana wengi wanadiriki kusema tafuta pesa ili uwe kama mfalme.
Wanaosema pesa ndiyo kila kitu tuna hoja za msingi .
Pesa inaweza kukufanya umfurahishe mpenzi wako kwa kumnunulia zawadi.
Kumnunulia mapambo ambayo yatamfanya awe na amani kwa wakati husika.
Yawezekana kuna vazi alikuwa akilipenda, unapomnunulia, anafurahi.
Unapokuwa hauna kitu ni rahisi kukimbiwa. Ni rahisi mwenzako kukuona huna msaada.
Anashuhudia wenzake wanavyofanyiwa na wapenzi wao, anaona yeye ni kama anaishi dunia ya pili. Siyo dunia hii ambayo wenzake wanafurahia mapenzi.
Mapenzi ya kweli yanaweza kupotezwa na pesa kama mtu asipokuwa makini. Pesa ina nguvu. Inaleta uhasama.
Inapoteza uaminifu, mtu anaposhawishiwa na pesa, katika mazingira ambayo kwake yeye ni magumu ni rahisi kutumbukia kwenye kishawishi.
Kama mtu anaishi kwenye mazingira ambayo hajui hatima yake, hajui kesho atakula au kuvaa nini ni tatizo. Hapendezi kama wenzake, anaishi kwa masimango.
Akitokea mtu mwenye pesa, akahitaji penzi lake, huyo bila kipingamizi anaanzisha uhusiano pasipo kuangalia ana mpenzi wake au la.
Tanasha anatambua vyema kwamba Diamond Bado yupo na Zarina lakini na yeye Bado yupo humo humo nguvu yapesa inatumika hapo Land cruiser V8 ndio imeenda kumpokea Airport Kuna Nini Tena hapo?