TANESCO achana na Solar Energy, ni wizi na hasara kwa Taifa

Haya ni mahubiri ya wema wa Mungu au ndio njia ya kutetea solar energy? Sikuelewi kabisa!!! Andika kinachojadiliwa. Acha kuleta habari ya Mwenyezi Mungu hapa. Mungu ndo anakuongoza hadi upate umeme wa solar? Umeulizwa; wapi Duniani solar ni alternative energy ya kutumainiwa? Sema!!!! Unaleta uliyokaririr darasani ili kujibu mtihani hapa! Fooool!
 
Watu wasiosoma Electricity, Electronics au Computer Eng hawawezi kuelewa Hili Sio Solar tu any DC power ni ghali per unit price kuliko AC, watu huwa haelewi kuwa hata kwenye Simu zetu za mkononi Battery ni one of most expensive component.


Solar Energy ni ghali sana
 
Siku zote Sola si umeme wa uhakika.
Kwa nini?kumbuka nchi nyingi waafrika solar energy inapatikana si chini ya masaa 12 tena asilia 99 mwaka mzima nini kigumu hapo mpaka usiwe umeme wa uhakika?
 
Solar ni umeme Bora na rahisi sana kuliko unavyopotosha!!!... Nimetumia solar hapa Gezaulole Kigamboni Dar es salaam miaka 6 sikuona Wala kupata shida ya aina yeyote!!!... Tofauti yake uwekezaji wake unahitaji fedha na utaalamu wa uhakika
Tena kwa nchi yetu yenye guarantee ya jua kali 12 hrs a day hususani mikoa ya pwan na kati
 
Kwa nini?kumbuka nchi nyingi waafrika solar energy inapatikana si chini ya masaa 12 tena asilia 99 mwaka mzima nini kigumu hapo mpaka usiwe umeme wa uhakika?
Nahisi una elimu ndogo au uelewa ni mdogo sana! Huo umeme wa masaa 12 ni kiasi gani na unaweza kufanya nini ktk maisha yako? Lengo ni kutumia umeme siyo tu kuzalisha umeme.
 
Sijui kwa nini TANESCO imejaza mainjinia lakini wana uelwa mdogo kiasi hiki. Lakini nahisi ni makusudi. Ni shirika lililozoea kuiba pesa miaka yote.
 
Kuna mikoa ina jua hatari ikiongozwa na dar es salaam pwan tanga dodoma pia kwa wastan nchi nzima ina pata 12hrs ya jua kwa siku shida iko.wapi hapo?
 
Bwana linajengwa kubwaaa la nini? Solar wizi mtupu
 
Kuna mikoa ina jua hatari ikiongozwa na dar es salaam pwan tanga dodoma pia kwa wastan nchi nzima ina pata 12hrs ya jua kwa siku shida iko.wapi hapo?
Jua kazi yake ni kucharge Battery, Hizo Battery ni Ghali sana... also Transmission ya DC ni gharama zaidi..

Hivi hujui
 
Kuna mikoa ina jua hatari ikiongozwa na dar es salaam pwan tanga dodoma pia kwa wastan nchi nzima ina pata 12hrs ya jua kwa siku shida iko.wapi hapo?
Hizo battery unajua zinauzwa bei gani, operating costs, miundombinu ya kufanikisha, kufunga vifaa upya kila baada ya muda mfupi, mvua ikinyesha na mwanga ukawa hautoshi. Usiku giza likiingia umeme unakosa then wanaoutumia huo wanafanyaje au utataka nao wanunue betri za kuhifadhi, kama sivyo basi betri za kuhifadhi kituoni ziwe nyingi kuwezesha hata usiku kutoa umeme.

Tangu wafunge mitambo ya HEP hujawahi sikia marekebisho ya gharama au muda mwingi.
 
Una maradhi kichwani wewe, kwa hiyo kwako jambo lolote zuri lazima kuwepo na reference mahali kama lina faida au la...wewe huwezi anzisha ya kwako mazuri na wengine waje kujifunza kwako, akili ya maskini mjinga wa mwisho...soma hapa uongeze ujinga ulionao Noor Ouarzazate Solar Complex, Morocco
 
Muda si mrefu naachana na hawa Tanesco,nitakuwa na umeme jua wangu natumbukiza kama 10M halafu ndio Tanesco watakuwa historia kwangu , hata uje umeme wa bwawa la Nyerere nimeamua kuwapa kisogo hawa Tanesco,hawaeleweki mara umeme unakatwa siku nzima,mara mtumiaji mkubwa ananunua umeme tofauti na anayetumia kidogo,badala ya kumjali anayetumia zaidi umeme wao wanamjali asiyetumia umeme, sasa kwa heri Tanesco nitakuwa off grid kwa kila kitu hadi maji.
 
Wewe ni mwongo,hujui unazungumza nini.
Acha kupotosha umma.Solar power ni nguvu ya juwa isio na mshindani.
Huko Kenya power and lighting company kama Tanesco inapumulia mashine, baada ya wananchi kuwekeza solar power kwa nyumba zao.
Wananchi walinyanyaswa sana kwa kukatika umeme mara kwa mara gharama kubwa ya umeme,lakini solar power ni UPS yaani un enterupted power supply. Tanesco hawezi hilo,hana sifa hiyo is days are numbered.
Pili solar panels una uwakika wa kupata umeme kati ya miaka 15 hadi 25.bila shida .
Shida kubwa tekinologia ni mpya kwa nchini kwetu na kuna watu wasiokuwa na sifa ndio wanatoa huduma mbovu na kupotosha nishati hiyo.
Nchi kama Ujerumani isio kuwa na mwanga wa jua kama nchi za tropic imeweza kuwa na ufanisi mkubwa wa nishati hiyo na kuuza akiba kwa mfumo wa conventional power kama Tanesco.
Tatizo si solar,tatizo ni upeo.
Miaka 5 ijayo kuna uwezekano mkubwa wa Tanesco akabakia kutoa huduma kwenye viwanda.
Twende na tekinologia.

 
We kajinga kweli kweli! Tunazungumzia umeme wewe unaleta mifano ya Kenya na wananchi wanaoweka solar, unaijua sababu ni nini? Usilete mifano usiyoijua mende we! Ndo ubaya wa JF. Mtu unabishana hata na ka mtu kenye elimu haba. Tunataka umeme wa kusaga nafaka, tunautaka tuendeshe mitambo ya kuranda mbao, vijana waweke barbaershops, nk. huko kenya wanafanya hayo kwa solar? Foool!

Hata tunayo REA unajua sababu kwa nini Kenya hawawezi kufanya rural electrification? hawawezi, na njia pekee ni watu binafsi kujiwekea Solar. Sisi tunaweza kwa sababu ya social settings na land ownership tuliyonayo. Kenya umeme uko Nairobi na kurudi kusini tu basi! Ukiingia miji na vijiji vya kaskazini mwa Nairobi huwezi. Sasa kama uko Tanesco na unaamua kwa kufuata yaliyotokea Kenya kwa ufahamu mdogo huu, ndo hiyo hatari tunayozungumzia kwamba Tanesco ina watu vihiyo.
 
Hongera! If you have 10 M to dispose of for home DC energy consumption then, you have good business paying back at a rate of 60% such that, in the next 4 years, you will be able to refurbish your system with new storage batteries. Uko kwenye Ndoto, boss!
 
Watu wengi hawajui electricity wala physics in general ndio maana wanazani Umeme wa solar ni cheap kisa unatoka kwenye Jua...

Hawajui kuzalisha Volt 1 ya DC ni ghali sana Kuliko Volt 1 ya AC. Yaani kwa matumizi ya Kawaida ya nyumbani gharama ya solar ni hata mara 10000

Hawa watu wangejifunza challenge wanayopata Magari ya Tesla kwenye Kucharge Hizo Battery and costfull the process is
 
Solar Ni DC power ni ina high cost per unit price from production to maintenance
Kwa taarifa yako tu ni kuwa kadri siku zinavyoongezeka kupungua kwa gharama za vifaa vinavyotumika kuzalisha umeme jua inazidi kupungua siku hadi siku kutokana na uboreshaji wa teknolojia. Mfano, miaka ya tisini solar panel bei yake ilikuwa karibu shilingi TZS 10,000/ Wp lakini kwa sasa inakaribia shilingi TZS 1,300/Wp. Na inazidi kushuka. Hii hali inaenda hata kwa vifaa kama batteries, charge controller, inverters, nakadhalika.

Kwa msingi huo, ni makosa kupiga kampeni dhidi ya matumizi ya umeme wa solar kwa sababu ya eti gharama kubwa za umeme huo wakati trends zinaonyesha bei ya umeme huo inashuka kadri siku zinavyosonga.
 

Katika umeme ambao siupendi ni wa SOLAR ,gharama za kuwekeza kubwa halafu mwanga hafifu hauna uhakika wa kulast 24hrs.......Ni wizi bora wainvest kwenye Nuclear Reactor.
 
Ni kweli gharama za kuzalisha umeme wa jua ziko juu kidogo kulinganisha na umeme huo wa AC.

Lakini kwa taarifa yako kusafirisha umeme wa DC ni bei ndogo zaidi kuliko kusafirisha AC. Na hapa ndipo panatia hasara maana loss njiani ni kubwa kwa AC. Suala la gharama za umeme si uzalishaji tu hata usambazaji. Pia gharama za uendeshaji za umeme wa solar ni ndogo kuliko za huo umeme unaopigia kampeni ya kufa na kupona!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…