Nguzo na vifaa vyote vya kuunganisha umeme ni mali ya TANESCO, katika hali halisi,huduma ya kuwekewa umeme ilipaswa kutolewa bure,mteja ulipie matumizi ya umeme.
Kwa miaka mingi walipa kodi wa Tanzania, kupitia serikali yao wamekuwa wanatoa ruzuku ya uendeshaji wa Shirika la Umeme Tanzania.
Miaka 5 iliyopita watumiaji wa umeme wamekuwa wakichangia au kulipia asilimia 3 kwenye mfuko wa REA,(kwa maana nyingine watumiaji wa umeme wamechangia mabillioni ya fedha kwenye mfuko wa REA).
Ninadhani,ni kwa muktadha huu serikali imeamua wananchi kulipia shs27,000 (kwa Waombaji wapya),hii siyo fadhila,ni wajibu wa serikali kwa wananchi wake na ni haki ya wananchi kupata huduma ya umeme kwa gharama nafuu.
Ushauri
(1). TANESCO kitengo Cha huduma kwa wateja badala ya kuwataka wateja kujaza taarifa zilizoainishwa, kwenye fomu zao,waagize kila kituo waweke utaratibu wa kuwasilisha taarifa ya pending applications za wateja wapya (TANESCO Mkoa/Kanda/Makao Makuu ) kila siku/week/mwezi/quarter/mwaka na hatua mbalimbali zilizofikiwa na changamoto.
(2). Aidha kitengo Cha huduma kwa wateja wanaweza kuingia kwenye mitandao wakaona (kwa mfano kituo Cha Nyakato au Chanika) Kuna pending applications ngapi.
(3).Kwa kuwa asilimia 3 ya REA inakusanywa na TANESCO,na kupelekwa kwenye mfuko au taasisi husika.
-Ni vema jukumu la usambazaji umeme(transmission-nguzo na vifaa vya umeme),likahamishiwa REA,na
-TANESCO,ikabakiwa na jukumu la uzalishaji (Generation-Vyanzo vya umeme) na utoaji huduma kwa wateja (ukusanyaji maduhuli nk).