TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

Vp sasa baada ya kukopa akihama kutoka Vodacom kisha akakopa na Tigo pamoja na Airtel, mtawezaje kumdhibiti
Kama atakua anahamahama mitandao kwaajili ya kukopa atakua na option 4 - 5 tu, lakini pia kwa hapo baadae hutoweza kusajili Sim card mpya kwenye mtandao mwingine kama una deni katika huduma za kifedha katika mtandao mwingine (Hili limeshafanyika kwenye huduma ya Mobile Number Portability), Pia ukiamua Usajili Sim card nyingine katika huo huo mtandao uliokopa, hutoweza kukopa kwenye Sim card yako mpya, Pia ikumbukwe mkopo unaopewa unaakisi matumizi yako katika hizo huduma za kifedha na mkopo unaopewa wanauhakika kwa asilimia zaidi ya 80 utakuwa na uwezo wa Kuulipa kulingana na historia yako ya Matumizi, bahati mbaya wa TZ wengi huwa wakikopeshwa katika hizi huduma za Kifedha hata kama wanauwezo wa Kulipa wengi huwa hawalipi na wanaona ni kama Sifa vile.
 
Tanesco itaanza kupoteza rasilimali watu/teknolojia kuanza ku deal na wadaiwa Sugu wa umeme wa elfu mbili mbili, Hii itakua ni sawa na Kuua Mende Kwa Nyundo.
Mkuu, wewe unaweza ukaishi sehemu ya giza kwa mwezi mmoja eti kwa kuwa TANESCO wanakudai 3,000?
 
Hakuna hoja yoyote ya maana humu
 
Nakuona manager wa TANESCO unavyopinga hoja kwa manufaa yako teh teh teh teh
 
Baba umeandika msaafu mzima bila nukta hata moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…