Kama atakua anahamahama mitandao kwaajili ya kukopa atakua na option 4 - 5 tu, lakini pia kwa hapo baadae hutoweza kusajili Sim card mpya kwenye mtandao mwingine kama una deni katika huduma za kifedha katika mtandao mwingine (Hili limeshafanyika kwenye huduma ya Mobile Number Portability), Pia ukiamua Usajili Sim card nyingine katika huo huo mtandao uliokopa, hutoweza kukopa kwenye Sim card yako mpya, Pia ikumbukwe mkopo unaopewa unaakisi matumizi yako katika hizo huduma za kifedha na mkopo unaopewa wanauhakika kwa asilimia zaidi ya 80 utakuwa na uwezo wa Kuulipa kulingana na historia yako ya Matumizi, bahati mbaya wa TZ wengi huwa wakikopeshwa katika hizi huduma za Kifedha hata kama wanauwezo wa Kulipa wengi huwa hawalipi na wanaona ni kama Sifa vile.