TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

Aiseeee wee jamaa ni genius kweli, anzisha consultancy firm. Hili ni wazo zuri mnooo sema tuu Tanesco inaendeshwa kizamani na wana mambo ya kizee/anology....
 
Kuna meneja mmoja wa tanesco nilikua naongea nae akaniambia shirika linaenda kufa...coz cost of production n kubwa kuliko mapato.
I agree kwa sababu miundombinu yake imechakaa na am sure umeme mwingi sana inapotea njiani. Hili shirika ili liwe na ufanisi ni lazima livunjwe into three sub companies : 1.Uzalishaji - Hawa kazi yao ni kuhangaika na mabwawa ya kuzalisha umeme pamoja na vinu vya gesi basi. 2.Usafirishaji wa umeme kutoka kwenye source - hawa kazi yao ni kuhangaika na yale ma laini makubwa ya kusafirisha umeme toka kwenye source mpaka kwenye vituo vya kupooza na kusambaza umeme majumbani. 3.Usambazaji wa umeme kwa watumiaji.
 
Acheni mawazo ya kizee nyie... Kwanza huu mfumo lengo lake kuu ni kusaidia pale umeme ikikata usiku au ghafla na mtu kwa muda huo hana alternative. Hivyo ni suala tuu la kuweka kiwango kidogo cha kukopa mfano umeme usiozidi elfu 10. Pia wanaweza kuwa na starting point ya umeme say wa elfu mbili, ambapo pale utakapokuwa umejipanga kununua umeme wa elfu 20 ujue wataanza kukata deni lao kwanza. Sasa kwa mfumo huo there is no way eti deni lita accumulate hadi lifikie laki mpaka mtu ahame nyumba, no way. Haiwezekani ukope umeme wa elfu 5 halafu ukae mwezi mzima bila kununua tena maana hata ukiingiza elfu 2 itakuwa inakata deni kwanza. Ni kama Songesha tuu...
 
Songesha unaweza kukopa laki moja?? Tuliza akili jombaa... Lazima kuwe na limit isiyozidi kiwango fulani kwa sababu unakopeshwa kiasi kidogo ili baadae au kesho ukanunue umeme wako. Kwani mitandao ya simu salio likikata wanaweza kukukopesha muda wa maongezi wa elfu 5?? Unaambulia mia 5 au at most buku... So it's the same thing...
 
Yaani hizo board ndo wale 60 % aliosema Prof Assad mkuu.. Kwanza they don't want changes maana wamejiwekea mifumo yao ya kizamani ya kupiga pesa...
 
Tumepokea ushauri tunashukuru sana mpendwa mteja wetu

TANESCO , Makao Makuu
Kuna mchangiaji hapo juu amesema aliwahi kuitwa na bodi yenu na akawakilisha hili wazo, mwisho akaishia kuambiwa ataitwa ndiyo ntolee mpaka leo.
 
Wewe ndiye unaona siyo rahisi but hapa duniani nothing is impossible...
 
Nani a kukopeshe umeme wa elfu 40? Mbona salio la simu hawawezi kukukopesha hata elfu 2? Sana sana ni 500 au buku....
 
Ukopeshe watanzania hawa hawa waliofanya TALA akabeba virago vyake, Africa mambo ya postpaid bado sana sisi hata matundu ya vyoo shida
Acha kuchanganya watanzania wote kwenye kapu moja. Wakati wewe unawaza hivyo wenzio wanachukua mikopo daily kwenye mabenki, SACCOS na Vikoba wanaendesha maisha yao. Wewe unayekimbia na kutupa laini ya simu kwa kukopa Songesha elfu 20 endelea...
 
Bora ungesema waunganishie watu umeme bure(namaanisha bure kabisa bila gharama za saveyor, sijui, mchoro, nguzo, waya etc). Kisha hizo gharama zote waziingize kwenye LUKU kila unaponunua umeme ukatwe pesa ya ziada hadi zitakapotimia. Mfano kama unit unanunua kwa 300tsh, basi mwenye deni anunue kwa 400. Kwakufanya hivyo watu wengi wangeweka umeme kwani kuna watu wanashindwa kulipia hata ule wa REA
 
Kaka mkubwa JMF hii yako pia ni idea nzuri saaaana mkuu. Hongera

 
Khee kukopa tena mkuu
Nilidhani utakuja na idea ya kuunganisha meter za Luku na mobile phone.
Ukinunua umeme unaingia moja kwa moja kwenye mita

Hio ya kukopeshana hata vida wanaweza wakakukopesha ununur umeme
 
Khee kukopa tena mkuu
Nilidhani utakuja na idea ya kuunganisha meter za Luku na mobile phone.
Ukinunua umeme unaingia moja kwa moja kwenye mita
Hii mada ya zamani sana
=====
 
Khee kukopa tena mkuu
Nilidhani utakuja na idea ya kuunganisha meter za Luku na mobile phone.
Ukinunua umeme unaingia moja kwa moja kwenye mita

Hio ya kukopeshana hata vida wanaweza wakakukopesha ununur umeme
Voda wakikopesha faida ni ya voda, lakini ukikopeshwa na TANESCO faida inaenda serikalini inawasaidia watanzania katika kujikwamua kiuchumi. Huu ndio uzalendo.
 
Acha kuchanganya watanzania wote kwenye kapu moja. Wakati wewe unawaza hivyo wenzio wanachukua mikopo daily kwenye mabenki, SACCOS na Vikoba wanaendesha maisha yao. Wewe unayekimbia na kutupa laini ya simu kwa kukopa Songesha elfu 20 endelea...
Jamaa anadhani kama yeye sio muaminifu basi watanzania wote wapo hivyo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…