Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I agree kwa sababu miundombinu yake imechakaa na am sure umeme mwingi sana inapotea njiani. Hili shirika ili liwe na ufanisi ni lazima livunjwe into three sub companies : 1.Uzalishaji - Hawa kazi yao ni kuhangaika na mabwawa ya kuzalisha umeme pamoja na vinu vya gesi basi. 2.Usafirishaji wa umeme kutoka kwenye source - hawa kazi yao ni kuhangaika na yale ma laini makubwa ya kusafirisha umeme toka kwenye source mpaka kwenye vituo vya kupooza na kusambaza umeme majumbani. 3.Usambazaji wa umeme kwa watumiaji.Kuna meneja mmoja wa tanesco nilikua naongea nae akaniambia shirika linaenda kufa...coz cost of production n kubwa kuliko mapato.
Mbona songesha mnakopa? Tatizo mnaogopa kwamba huku huwezi kukimbia na kuhamia mtandao mwingine.Kukopa kopa sio kuzuri bora ibaki hivi.
Kuna siku atakuoa uwe mke wake wa pili... [emoji23] [emoji23]Tundu Lissu atabisha mpaka wazo hili
Acheni mawazo ya kizee nyie... Kwanza huu mfumo lengo lake kuu ni kusaidia pale umeme ikikata usiku au ghafla na mtu kwa muda huo hana alternative. Hivyo ni suala tuu la kuweka kiwango kidogo cha kukopa mfano umeme usiozidi elfu 10. Pia wanaweza kuwa na starting point ya umeme say wa elfu mbili, ambapo pale utakapokuwa umejipanga kununua umeme wa elfu 20 ujue wataanza kukata deni lao kwanza. Sasa kwa mfumo huo there is no way eti deni lita accumulate hadi lifikie laki mpaka mtu ahame nyumba, no way. Haiwezekani ukope umeme wa elfu 5 halafu ukae mwezi mzima bila kununua tena maana hata ukiingiza elfu 2 itakuwa inakata deni kwanza. Ni kama Songesha tuu...Kwann mnapenda sana mkopo? Hii system ya TANESCO kutokopesha ni nzuri. Kuna nyumba za kupanga au fremu za biashara.
Mtu anakopa umeme wa laki moja ukiisha anahama. Mzigo unamwangukia mwingine
Naona waweke tu mfumo,ukinunua umeme kwa mfano wa 5000 unajijaza wenyewe. Hakuna kwenda kujaza kwenye mita
Songesha unaweza kukopa laki moja?? Tuliza akili jombaa... Lazima kuwe na limit isiyozidi kiwango fulani kwa sababu unakopeshwa kiasi kidogo ili baadae au kesho ukanunue umeme wako. Kwani mitandao ya simu salio likikata wanaweza kukukopesha muda wa maongezi wa elfu 5?? Unaambulia mia 5 au at most buku... So it's the same thing...Kweli ww ni mataga wa kiwango cha PHD.
mita ni mali ya TANESCO na huwezi kuhama nayo.
Mm nimepanga fremu, kumbuka mita iliyofungwa, imefungwa na kusajiliwa jina jingine.
Nimekuja kwako na nimepanga fremu ya duka. Umeme unajitegemea. Siku nakaribia kuondoa nakopa umeme wa laki moja. Muda ukiisha naondoka. Hilo deni nani analipa?
Watanzania ni wagumu sana kulipa madeni. Kuna watu wanadaiwa na voda, tigo, airtel, branch na tala lkn hawajalipa mpaka leo.
Lissu hawezi kuwa na akili za kijinga kama hizi za kwako
Kawaulize wale JKT 850 [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Soja jiunge CCM nikupe shavu uache kuendesha Taxi bubu
Yaani hizo board ndo wale 60 % aliosema Prof Assad mkuu.. Kwanza they don't want changes maana wamejiwekea mifumo yao ya kizamani ya kupiga pesa...Kuna jamaa yangu ni mtaalamu wa Computer Engineering na Uchumi, katika maongezi yetu siku moja akanigusia hilo la kutengeneza mfumo huo wa kumkopesha mteja na akaenda kuuwasilisha kwenye board ya mameneja wa makao makuu akaambiwa asubiri ataitwa mpaka leo hola.
Nb. Sio hao tu Tanesco, niliwahi kuwaambia Dawasco wanifungie maji ofisini kwangu sababu biashara ninayoifanya haifanyiki bila maji tena ya kutosha, nikapewa fundi akaja walipofika fundi akaanza kuchimba ili aniunganishie maji ofisini, kidogo faza hausi akaja kumbe na yeye alikuwa ameomba aletewe ya Dawasco ikabidi kwangu huduma isitishwe kuunganishiwa akaunganishiwa mwenye nyumba mimi wa biashara nikaachwa. Kichekesho kinakuja kwenye bill, mwenye nyumba huwa bill yake haizidi elfu 3 kwa mwezi.
Kuna mchangiaji hapo juu amesema aliwahi kuitwa na bodi yenu na akawakilisha hili wazo, mwisho akaishia kuambiwa ataitwa ndiyo ntolee mpaka leo.Tumepokea ushauri tunashukuru sana mpendwa mteja wetu
TANESCO , Makao Makuu
Wewe ndiye unaona siyo rahisi but hapa duniani nothing is impossible...Umeangalia kwa mtazamo mmoja. Kwa wenye nyumba tu lakn haujaangalia kwa wapangaji. Mtu amepanga fremu au nyumba nzima. Siku anakaribia kuondoka anakopa umeme wa 20,000. Na halipi deni.
Hiyo hela atalipa nani? Siyo rahisi kama unavyofikiria ndiyo maana hauajatoa maelezo yaliyojitosheleza na njia zake ndiyo maana umekimbilia kukopesha.
Hii italeta migogoro sana, na siafiki suala hili la kukopa umeme hata kwa 100%
Nani a kukopeshe umeme wa elfu 40? Mbona salio la simu hawawezi kukukopesha hata elfu 2? Sana sana ni 500 au buku....Kukopesha umeme ni suala gumu ndiyo maana hata ww haujatoa ni njia gani watatumia kukopesha unit ila umeandika wawe wanakopesha.
Ni ngumu na italeta migogoro sana. Fikiria umepangishwa nyumba halafu kuna deni la 40,000 halijalipwa. Hiyo hela anatoa nani?
Ukiangalia thread yako haijajitosheleza. Ni njia gani TANESCO watatumia kukopesha umeme? Kuna nyumba zinapangishwa nzima.
Acha kuchanganya watanzania wote kwenye kapu moja. Wakati wewe unawaza hivyo wenzio wanachukua mikopo daily kwenye mabenki, SACCOS na Vikoba wanaendesha maisha yao. Wewe unayekimbia na kutupa laini ya simu kwa kukopa Songesha elfu 20 endelea...Ukopeshe watanzania hawa hawa waliofanya TALA akabeba virago vyake, Africa mambo ya postpaid bado sana sisi hata matundu ya vyoo shida
Kaka mkubwa JMF hii yako pia ni idea nzuri saaaana mkuu. HongeraBora ungesema waunganishie watu umeme bure(namaabisha bure kabisa bila gharama za saveyor, sijui, mchoro, nguzo, waya etc). Kisha hizo gharama zote waziingize kwenye LUKU kila unaponunua umeme ukatwe pesa ya ziada hadi zitakapotimia. Mfano kama unit unanunua kwa 300tsh, basi mwenye deni anunue kwa 400. Kwakufanya hivyo watu wengi wangeweka umeme kwani kuna watu wanashindwa kulipia hata ule wa REA
Hii mada ya zamani sanaKhee kukopa tena mkuu
Nilidhani utakuja na idea ya kuunganisha meter za Luku na mobile phone.
Ukinunua umeme unaingia moja kwa moja kwenye mita
Voda wakikopesha faida ni ya voda, lakini ukikopeshwa na TANESCO faida inaenda serikalini inawasaidia watanzania katika kujikwamua kiuchumi. Huu ndio uzalendo.Khee kukopa tena mkuu
Nilidhani utakuja na idea ya kuunganisha meter za Luku na mobile phone.
Ukinunua umeme unaingia moja kwa moja kwenye mita
Hio ya kukopeshana hata vida wanaweza wakakukopesha ununur umeme
Voda wakikopesha 5,000/= baada ya siku nne mtu anakopa tena Tigo 2,000/= atahama huko na kukopa tena Airtel au Halotel.Hio ya kukopeshana hata vida wanaweza wakakukopesha ununur umeme
Jamaa anadhani kama yeye sio muaminifu basi watanzania wote wapo hivyo hivyoAcha kuchanganya watanzania wote kwenye kapu moja. Wakati wewe unawaza hivyo wenzio wanachukua mikopo daily kwenye mabenki, SACCOS na Vikoba wanaendesha maisha yao. Wewe unayekimbia na kutupa laini ya simu kwa kukopa Songesha elfu 20 endelea...
Naona umekuwa smart911 ghafla