TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

TANESCO inaweza ikatengeneza faida kubwa sana endapo wataanza kukopesha units za LUKU. Hii ni ngumu kwa mteja kukwepa marejesho

Tatu,kwa kufanya hivyo inabidi Tanesco walipe kodi ya mapato yatakayotokana na mikopo ya umeme kwa muda fulani kitu hivyo hicho unachowaza kwamba ni "faida kubwa" haitakuwepo pesa nyingi italipa kodi (VAT na nyinginezo) na gharama za uendeshaji.
Kwani mapato ya sasa ya TANESCO yanalipiwa VAT (kodi za serikali au hapana)? Hiyo mitandao ya simu inayokopesha wanawezaje kupata faida kwa huduma hiyo? Kwani wao hawalipi kodi za serikali (VAT)?
 
Pili, Tanesco ili akopeshe umeme lazima awekeze hela ya kununua umeme toka kwa mzalishaji kwa minajiri ya mkopo tuu.
Nne,timing ya kumlipa mzalishaji itakuwa disrupted na mikopo ya umeme.
Unaona sasa ambavyo unajichanganya wewe mwenyewe. Point yako ya pili na ya nne zinakinzana pakubwa sana. Time ya kumlipa mzalishaji itakuwa interupted vipi wakati tayari umeshauri TANESCO lazima aweke hele ya kununua umeme kutoka kwa mzalishaji.
 
Fuatilia uendeshaji wa hili shirika ndio utajua kwanini selikali ime-monopolize huduma ya umeme. Kwanini hakuna soko huria la umeme. Yani kila mti azalishe na asambaze.
Serikali ime-monopolize huduma ya umeme kwa sababu ya miundombinu ya usambazaji kuwa migumu.

Kwani ni nini kimeleta ushindani kwa TTCL kama sio technology ya wireless? Unafikiri kukiwa na umeme wa wireless TANESCO hawataongeza ubunifu katika kutoa huduma zao?
 
Tanasco hawazalishi umeme "produce" anasambaza "supply".
Yeye pia ananunua huo umeme kutoka kwa wazalishaji.
Pili, Tanesco ili akopeshe umeme lazima awekeze hela ya kununua umeme toka kwa mzalishaji kwa minajiri ya mkopo tuu. Yaani kutakuwa na mtaji wa kuendesha mkopo wa umeme. Unaposikia Mpawa au Songesha katika mitandao ya pesa ujue ile ni "separate legal entity" yenye mandate ya kukopesha. Mara nyingi Kampuni za simu huwapa hilo deal mabenki.
Tatu,kwa kufanya hivyo inabidi Tanesco walipe kodi ya mapato yatakayotokana na mikopo ya umeme kwa muda fulani kitu hivyo hicho unachowaza kwamba ni "faida kubwa" haitakuwepo pesa nyingi italipa kodi (VAT na nyinginezo) na gharama za uendeshaji.
Nne,timing ya kumlipa mzalishaji itakuwa disrupted na mikopo ya umeme. Tanesco ili amlipe umeme mzalishaji lazima auuze. Fuatilia uendeshaji wa hili shirika ndio utajua kwanini selikali ime-monopolize huduma ya umeme. Kwanini hakuna soko huria la umeme. Yani kila mti azalishe na asambaze.
CHADEMA hamuishi vituko
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wa humu JamiiForums.

Kwanini TANESCO haikopeshi units za umeme wa LUKU kwa wateja wake? Mimi ninaona kama mchakato huu utawawezesha kupata faida kubwa sana kama riba kwa maana ni ngumu sana kwa mteja kukwepa marejesho.

Tofauti ya mteja wa TANESCO na mteja wa mtandao wa simu za mikononi kama Vodacom na Tigo ni kwamba, mteja wa mitandao hii ana nafasi kubwa sana ya kutokulipa deni kwa maana anaweza kubadili simcard au anaweza kufa kisha deni likawa limepotea tofauti na mteja wa TANESCO ambaye deni linakuwa limebebwa na nyumba kiasi kwamba hata akifa, deni litakatwa wakati wa ku-transfer property ownership.

Mteja wa mitandao ya simu za mikononi anaweza akakopa Vodacom kisha akahama mtandao akaanza kutumia Tigo, lakini mteja wa TANESCO hawezi kubadili number yake ya mita ya LUKU. Kama alikopa umeme wa 20,000/= kwa kutumia M-PESA inakuwa ngumu sana kukopa tena kwa kutumia mtandao mwingine kama vile TIGO PESA kwa maana atatumia number ile ile ya mita hivyo computer system itakataa kufanya muamala wa kumpa units.

TANESCO wanaweza kufanya special arrangement na kampuni husika ya mtandao wa simu kama Vodacom au Tigo kutoka mkopo wa pesa mahususi kwa kununua units za umeme tu na sio muamala mwingine wowote. Ukitumia pesa hiyo kwa muamala mwingine inakataa.

Mathalana TANESCO wanaweza kukukopesha umeme wa 15,000. Halafu utakatwa labda 25% kila utakaponunua tena mpaka deni liishe. Au ukiamua unalipa 100%.

Wataalam wa masuala ya uchumi pamoja na ICT mnaweza kulifafanua hili zaidi kwa maana hiyo sio taaluma yangu lakini ninapendekeza number itakayoruhusiwa kukopa iwe moja tu (Mmiliki wa nyumba) hususan kwa nyumba zenye wakazi (wapangaji) wengi

NB: Ndugu zangu waislam, Mungu awatangulie na kuwasimamia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Siku zote 30 za mfungo zikawe za kheri na baraka kwenu. Wishing you courage and strength so that you win every challenge of this life.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Unaweza ukawa na wazo zuri labda utufafanulie kidogo,unataka TANESCO ndo wapate faida au mwananchi asiye na uwezo wa kununua umeme ndo AFAIDIKE NA MKOPO??

Kumbuka huduma ya sasa ni "pre paid" hivyo TANESCO wanapata fedha nyingi sana kwa kukaa na fedha zetu tulizonunulia unit ambazo bado hatujazitumia.
 
Unaweza ukawa na wazo zuri labda utufafanulie kidogo,unataka TANESCO ndo wapate faida au mwananchi asiye na uwezo wa kununua umeme ndo AFAIDIKE NA MKOPO??
It's a two way traffic. TANESCO na MWANANCHI wote wananufaika.
 
Ukopeshaji infact ni hasara na upumbavu kwa Tanesco maana ina involve upumbavu wa kukatia watu umeme which infact ni hasara zaidi kwao....

Kopeshaneni huko,rushaneni,pelekaneni mahakamani,Tanesco akiingilia ni hasara kwake...

Tanesco katika ukopeshaji ni hasara kwao
Sawa mzee wa kutumia tusi "upumbavu" kama staha. Siwezi kujadiliana na mtu anayetanguliza matusi mbele.
 
Back
Top Bottom