mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
TANESCO wawe wawazi kuwa kuna mgao wa umeme unaoendelea hapa nchini kwa hivi sasa. Pengine itakuwa ni jambo jema zaidi kama ingetoa ratiba ya mgao huu ili watu waweze kujipanga zaidi kutokana na athari zinazojitokeza.
Tumeshuhudia busara kubwa iliyofanyika kupitia taarifa iliyotolewa na viongozi wa DAWASA kuhusu kupungua kwa kina cha maji katika mtambo wa Ruvu Chini. Taarifa hii ilienda sambamba na sababu za kitaalamu kuhusu athari zinazosababisha haja ya mgao wa maji, na hata kutoa ratiba ya mgao jinsi ambayo shirika lilivyojipanga na linavyohakikisha utakavyokuwa.
Hali ni tofauti mno kwa shirika dada la TANESCO. Tunapata hisia ya kuwa uhaba wa maji unaondelea hapa nchini kutokana na kukosekana kwa mvua za kutosha za vuli pengine pia una athari hasi katika uzalishaji wa "hydroelectric power". Hali ambayo inapelekea kuwepo kwa uhaba wa nishati hii muhimu.
Lakini tofauti na uongozi wa DAWASA, wao wamemua kuuchuna tu. Cha kushangaza zaidi ni kwamba, shirika hili sasa lipo chini viongozi wapya tena wengi wao wakitokea katika sekta binafsi, tulitarajia kuwa wangalikuwa "proactive" na kutuandaa kisaikolojia kuhusu adha ambayo wanaiona itakuja katika siku za mbele. Lakini wapi! Walishindwa kufanya hivyo kwa wakati.
Basi kwa sasa hata wawe "reactive" na kutoa maelezo kuhusu nini hasa ambacho kinaendelea kuhusiana na uwepo wa mgao wa umeme. Wananchi wanalalamika kila kona ya nchi, lakini wala wao hawaonyeshi kuguswa na jambo hili.
Serikali ya awamu ya 6 tunawasihi sana ilichukulie suala hili kama jambo la dharura. Tunaona imekuwa ni jambo la lililozoeleka hivi sasa, kila mazuri yote yakifanywa na serikali sifa zote na utukufu hurudi kwake Madam President, lakini mapungufu makubwa kama haya wala nayo hayawi tena "attributed" kwake. Hii si sawa hata kidogo.
Ukubwa ni jalala, kama mazuri tuna ya "attribute" kwake, basi hata mapumgufu pia ni lazima yaende kwake.
Uongozi wa TANESCO tafadhali sana mtuambie kwa uwazi kuhusu jambo hili. Kumbukeni tu ya kwamba mficha .... maradhi humuumbua.