wababayangu
JF-Expert Member
- Jul 17, 2021
- 814
- 1,107
Kwani JPM alikuwa ni wa chama gani? Mbona katika utawala wake hakukua na mgao wa umeme?Utaishaje as long as CCM iko madarakani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani JPM alikuwa ni wa chama gani? Mbona katika utawala wake hakukua na mgao wa umeme?Utaishaje as long as CCM iko madarakani?
usipanic sasa.CHADEMA WATAKUJA NA MITAMBO YAO AU SIO??
Tuletee hapa tutathimini wenyewe, kwani mmeshaonywa kwa uchawa baada ya kuwa mnautumia vibaya.Nimeona ratiba ya umeme kwa maeneo ya oysterbay na Mbezi huko mitandaoni, je mgao umeanza au ni mambo ya kiufundi tu?
Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Ni kweli winch ipo na ilitumika kutelemsha hiyo milango na pia hutumika kwa kazi mbalimbali.litamgalimu sana niemongea na watu kule kwenye bwawa la nyerere wanasema winchi lipo na iyo milango ipo January anahujumu taifa
Huku nilipo ni siku ya 3 umeme unakatika saa 12 asubuh na unarudi saa 2 usiku.Mgao huwa inatolewa ratiba kabisa na kuelezwa muda wa saa za mgao!
Kwa hiyo kutolewa taarifa ya tarehe 15/11 ndiyo inabeba siku za mbele zinazofuata?Nimeona mada ya Mkuu Cannabis kuhusu matengezo yanayotarajiwa kufanywa na TANESCO. Taarifa kama hizi zikitolewa mapema inakuwa ni jambo jema sana. View attachment 2010313
Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Lile tangazo la juzi kwamba tarehe 15/11 kuna mikoa 11 itakatiwa umeme kwa masaa12, leo tarehe 16/11 imekatiwa tena kimya kimya bila taarifa, karibu nusu ya nchi ipo gizani.Muda huu kuna maeneo mengi katika jiji la Dar es Salaam umeme umekatika hebu tupeane taarifa hali ilipo mtaani au kazini kwako ili tujue ukubwa wa tatizo na Tanesco waje kutupa mrejesho wa hali ilivyo na viongozi waone hali halisi iliyopo.Ni vizuri kutaja umekatika muda gani.
Karibuni
JPM mfuatilie kuanzia kwenye kampeni zake za uchaguzi za 2015, kupata urais hadi alipokuja kukoromewa na Mkapa kwenye kikao cha marais wastaafu.Kwani JPM alikuwa ni wa chama gani? Mbona katika utawala wake hakukua na mgao wa umeme?
TANESCO wawe wawazi kuwa kuna mgao wa umeme unaoendelea hapa nchini kwa hivi sasa. Pengine itakuwa ni jambo jema zaidi kama ingetoa ratiba ya mgao huu ili watu waweze kujipanga zaidi kutokana na athari zinazojitokeza.
Tumeshuhudia busara kubwa iliyofanyika kupitia taarifa iliyotolewa na viongozi wa DAWASA kuhusu kupungua kwa kina cha maji katika mtambo wa Ruvu Chini. Taarifa hii ilienda sambamba na sababu za kitaalamu kuhusu athari zinazosababisha haja ya mgao wa maji, na hata kutoa ratiba ya mgao jinsi ambayo shirika lilivyojipanga na linavyohakikisha utakavyokuwa.
Hali ni tofauti mno kwa shirika dada la TANESCO. Tunapata hisia ya kuwa uhaba wa maji unaondelea hapa nchini kutokana na kukosekana kwa mvua za kutosha za vuli pengine pia una athari hasi katika uzalishaji wa "hydroelectric power". Hali ambayo inapelekea kuwepo kwa uhaba wa nishati hii muhimu.
Lakini tofauti na uongozi wa DAWASA, wao wamemua kuuchuna tu. Cha kushangaza zaidi ni kwamba, shirika hili sasa lipo chini viongozi wapya tena wengi wao wakitokea katika sekta binafsi, tulitarajia kuwa wangalikuwa "proactive" na kutuandaa kisaikolojia kuhusu adha ambayo wanaiona itakuja katika siku za mbele. Lakini wapi! Walishindwa kufanya hivyo kwa wakati.
Basi kwa sasa hata wawe "reactive" na kutoa maelezo kuhusu nini hasa ambacho kinaendelea kuhusiana na uwepo wa mgao wa umeme. Wananchi wanalalamika kila kona ya nchi, lakini wala wao hawaonyeshi kuguswa na jambo hili.
Serikali ya awamu ya 6 tunawasihi sana ilichukulie suala hili kama jambo la dharura. Tunaona imekuwa ni jambo la lililozoeleka hivi sasa, kila mazuri yote yakifanywa na serikali sifa zote na utukufu hurudi kwake Madam President, lakini mapungufu makubwa kama haya wala nayo hayawi tena "attributed" kwake. Hii si sawa hata kidogo.
Ukubwa ni jalala, kama mazuri tuna ya "attribute" kwake, basi hata mapumgufu pia ni lazima yaende kwake.
Uongozi wa TANESCO tafadhali sana mtuambie kwa uwazi kuhusu jambo hili. Kumbukeni tu ya kwamba mficha .... maradhi humuumbua."Hang
Waliomchukia Magufuli ndo wanamfanya azidi kukumbukwa na kuongezewa credit. Ni mwenye wizara ya nishati. Magufuli kafa na mgao wa umeme umeanza, kisingizio ni jua kali na ukame, kumbe hamna kitu ni wapiga madili tuuuuu.TANESCO wawe wawazi kuwa kuna mgao wa umeme unaoendelea hapa nchini kwa hivi sasa. Pengine itakuwa ni jambo jema zaidi kama ingetoa ratiba ya mgao huu ili watu waweze kujipanga zaidi kutokana na athari zinazojitokeza...