TANESCO isifiche kuhusu mgao wa umeme

Unatusababishia hasara wengine bila Umeme kazi zinalala
 
TANESCO ni shirika la wahuni na wapiga dili. Wanaona kama shirika ni lao na hakuna kitu serikali itawafanya.
 
Nimeona ratiba ya umeme kwa maeneo ya oysterbay na Mbezi huko mitandaoni, je mgao umeanza au ni mambo ya kiufundi tu?

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Tuletee hapa tutathimini wenyewe, kwani mmeshaonywa kwa uchawa baada ya kuwa mnautumia vibaya.
 
litamgalimu sana niemongea na watu kule kwenye bwawa la nyerere wanasema winchi lipo na iyo milango ipo January anahujumu taifa
Ni kweli winch ipo na ilitumika kutelemsha hiyo milango na pia hutumika kwa kazi mbalimbali.

Mitambo ya kuzalisha umeme ni mizito kuliko hiyo milango. Hivyo basi, haiingii akilini hiyo kampuni kubwa, na ilitembelewa na Rais SSH alipokuwa Misri, ikose winch ya kufanyia kazi!!
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA TANESCO MKOA WA MOROGORO .

TAARIFA YA KUOMBA RADHI KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA UMEME MKOA WA MOROGORO.

Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa MOROGORO linaomba radhi wateja wake kwa kukosekana kwa huduma ya umeme kutokana na hitilafu iliyojitokeza katika kituo cha kupokea na kupooza umeme Msamvu.

Tarehe :16/11/2021

Siku :Jumannne.

Sababu: Hitilafu imejitokeza katika transfoma kubwa la T4 na team inaendelea na uchunguzi kubaini tatizo ili kuhakikisha huduma inarejea kama kawaida.

Maeneo yanayoathirika ni:
Manisipaa ya Morogoro, Wilaya ya Kilosa,Wilaya ya Morogoro vijijini,Baadhi ya Maeneo ya Wilaya ya Mvomero pamoja na maeneo yanayotumia laini hizo:


JUHUDI ZILIZOFANYIKA

Tayari team yetu ziko saiti kuemdelea kuhakikisha huduma inarejea.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu utakaokuwa umejitokeza.

Tahadhari usishike wala kukanyaga nyaya zilizolala chini toa Taarifa Emergency kupitia namba 0677063001/0684889272

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz,

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

Imetolewa na:
*OFISI YA UHUSIANO NA HUDUMA KWA WATEJA- MOROGORO.
 
Nimeona mada ya Mkuu Cannabis kuhusu matengezo yanayotarajiwa kufanywa na TANESCO. Taarifa kama hizi zikitolewa mapema inakuwa ni jambo jema sana. View attachment 2010313

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo kutolewa taarifa ya tarehe 15/11 ndiyo inabeba siku za mbele zinazofuata?

Jana Tarehe 15/11 hapakuwa na umeme kutwa nzima na leo tarehe 16 mpaka muda huu naandika hskuna umeme tangia asubuhi.
Nchi hii Tanesco walishatudharau sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lile tangazo la juzi kwamba tarehe 15/11 kuna mikoa 11 itakatiwa umeme kwa masaa12, leo tarehe 16/11 imekatiwa tena kimya kimya bila taarifa, karibu nusu ya nchi ipo gizani.

Kwa kanda zingine sielewi hali ipoje!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani JPM alikuwa ni wa chama gani? Mbona katika utawala wake hakukua na mgao wa umeme?
JPM mfuatilie kuanzia kwenye kampeni zake za uchaguzi za 2015, kupata urais hadi alipokuja kukoromewa na Mkapa kwenye kikao cha marais wastaafu.

Ilikuwa ni: "chagua JPM", T shirt zilichapishwa picha ya mwenge na M kubwa ikimaanisha Magufuli na siyo sisiem na kukawa na kauli za: "serikali yangu" kumaanisha alijitofautisha na chama kilichompa madaraka kilicholalamikiwa na wananchi.

Kama kungelikuwa na sheria za wagombea binafsi, sidhani kama Magufuli angeligombea kupitia sisiem.

Sisiem kwake ilikuwa ni kipandia daraja tu, lakini ilivyokuwa imeoza mwanzoni roho yake ilikuwa inaona hata kinyaa kukitaja, hadi alipokuja kuwakaba koo yeye mwenyewe alipokuwa na uwezo wa kuwamudu.

Tuone sasa baada yake kama hawatarudi kufanya kazi kwa mazoea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

"HANGAYA" kishasema "viatu vya mwendazake vinampwaya" unategemea nini?
Team "Msoga" wao ndio wanaongoza shoo, hakuna jipya , tumerudi mwaka 1963 tulipoungana na wazanzibar
 
Kwa namna ya kipekee kabisa tuendelee kusifu na kuabudu, huku tukiamkumbuka JPM kwa mema yote.

Naona maboza yameanza kazi rasmi kupelekea wateja maji.

Tuliwaambia, chimbeni visima mvune maji ya mvua!!
 
TANESCO wawe wawazi kuwa kuna mgao wa umeme unaoendelea hapa nchini kwa hivi sasa. Pengine itakuwa ni jambo jema zaidi kama ingetoa ratiba ya mgao huu ili watu waweze kujipanga zaidi kutokana na athari zinazojitokeza...
Waliomchukia Magufuli ndo wanamfanya azidi kukumbukwa na kuongezewa credit. Ni mwenye wizara ya nishati. Magufuli kafa na mgao wa umeme umeanza, kisingizio ni jua kali na ukame, kumbe hamna kitu ni wapiga madili tuuuuu.
 
Hii katika katika ya umeme ni kiboko inakumbusha enzi za Mkapa na Kikwete. Rais Samia angalau uturudishie Kalemani Kama naibu waziri wa Nishati akapambane na TANESCO, wamerelax sana baada ya mtu huyu kuondoka. Umeme umekuwa Kero. Makamba aendelee kuwa Waziri na ajikite kwenye mafuta kalemani awe naibu ajikite na umeme
 
Huo ni mkakati maalumu, makamba amesema watu sasahivi wanafanya kazi kwa weledi na si kwa hofu ya kutumbuliwa ndo mana hali iko hivo sababu wafanyakazi wako huru kwasasa furaha na tabasam limerejea nyusoni na mioyoni mwao.
 
Unajua kosa lililomtoa? Zingekuwa nchi nyingine angekuwa amenyongwa.
Msidhani mama mjinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…