Tanesco kuleta mfumo wa watu kununua umeme kama unalipia kingamuzi bila kuweka Token

TANESCO ni mwisho wa Sept 2026, kinachhoitwa mchakato kilianza April 2025, mpaka leo bila bila.

Tangu jana usiku najaribu kuingiza token kupitia "remote"bila mafanikio, asubuhi nimeongea na 180, fundi amefika saa 4 asb, anadai remote" imeharibika ninunue nyingine kwa tsh 80,000. Kaondoka kwamba umeme ukirudi, atarejea ajaze nilionunua sasa ni saa 3.30,baada ya umeme kurejea lakini, hajafika.

Nimeshawishiwa kuachana gesi ili nitumie umeme, familia haijapata msosi tangu asubuhi, vitu kwenye friji vinaharibika hapo machungu ya kulala giza nayafahamu mwenyewe.

Nauliza, huu mchakato wa kuachana na kujaza token, utamalizika lini?
 
TANESCO ni mwisho wa Sept 2026, kinachhoitwa mchakato kilianza April 2025, mpaka leo bila bila.

Tangu jana usiku najaribu kuingiza token kupitia "remote"bila mafanikio, asubuhi nimeongea na 180, fundi amefika saa 4 asb, anadai remote" imeharibika ninunue nyingine kwa tsh 80,000. Kaondoka kwamba umeme ukirudi, atarejea ajaze nilionunua sasa ni saa 3.30, hajafika.

Haya majamaa yalivyo ******* yame-like tu post yako halafu yamepita hivi!
 
TANESCO ni mwisho wa Sept 2026, kinachhoitwa mchakato kilianza April 2025, mpaka leo bila bila.

Tangu jana usiku najaribu kuingiza token kupitia "remote"bila mafanikio, asubuhi nimeongea na 180, fundi amefika saa 4 asb, anadai remote" imeharibika ninunue nyingine kwa tsh 80,000. Kaondoka kwamba umeme ukirudi, atarejea ajaze nilionunua sasa ni saa 3.30, hajafika.

Nimeshawishiwa kuachana gesi ili nitumie umeme, familia haijapata msosi tangu asubuhi, vitu kwenye friji vinaharibika hapo machungu ya kulala giza nayafahamu mwenyewe.

Nauliza, huu mchakato wa kuachana na kujaza token, utamalizika lini?
Habari, ndugu mteja na asante kwa kuwasiliana nasi.

Pole kwa changamoto hii. Tunaomba ututumie mawasiliano yako kupitia inbox yako tukupigie kwa msaada zaidi huku tunafuatilia suala hii.

Asante. ^CM
 
Nimetuma
 
Tanesco kuleta mfumo wa watu kununua umeme kama unalipia kingamuzi bila kuweka Token.

View attachment 3301359

Shirika la umeme Tanzania Tanesco wako kwenye mchakato wa kuleta mfumo wa kisasa wa watu kuweza kununua umeme kama kifurushi bila kuingizia token kwenye Mita namba ya nyumbani kwako.

Watumiaji watakua na uwezo wa kununua kama kifurushi vile vinavyopatikana kwenye kingamuzi, ambapo pale pale TU baada ya kununua Kifurushi chako umeme unawaka bila kuingiza token kwenye Mita.

View attachment 3301360

Mfumo huo utaweza kuiitwa Smart Meters ambazo wananchi wanapaswa kuzipata toka kwa ofisi za Tanesco wataweza kupewa Meter za kisasa watakua na uwezo wa kuweka umeme kama unalipia kingamuzi bila kuingiza token .
Mchakato ulivamiwa na mkakati ukaishia maporini.
 
Mchakato ulivamiwa na mkakati ukaishia maporini
Habari Hismastersvoice, asante kwa kuwasiliana nasi.

Tunapenda kukufahamisha kuwa zoezi la mfumo mpya wa matumizi ya mita janja (smart meter) tayari limeshaanza kwa baadhi ya Mikoa nchini.

Kwa sasa, huduma ya kufungiwa mita janja ni bure, inafanyika kwa hiari na kwa awamu. Hivyo, zoezi litakapofika katika eneo lako, nawe utafungiwa mita bila gharama yoyote.

Tunakuomba uwe na uvumilivu wakati zoezi hili linaendelea. Litakapokufikia katika eneo lako, usikose fursa ya kupata huduma hii.

Asante. ^FL
 
Duh hii ndio naisikia leo.

Nimewapigia jamaa zangu kibao mikoa tofauti wanashangaa nawaambia kitu gani...

Imebidi nikae kimya wasije wakadhani nimekuwa chizi...
 
Habari, Ndugu Mteja.

Tunapenda kukujulisha kuwa kampeni hii bado inaendelea, na baadhi ya wateja tayari wamepatiwa mita mpya na wanaendelea kunufaika na huduma hii.

Kampeni itakapofikia eneo lako, utapewa taarifa rasmi. Kuhamia kwenye mita mpya ni hiari ya mteja.

Asante. ^FL
 
Habari, ndugu mteja.

Tunashukuru na ofisi itakupigia kwa msaada zaidi leo
Ndugu, TANESCO, naomba kutoa mrejesho kuwa tatizo langu lumepata ufumbuzi kiasi cha dakika kama 20 zilizopita.
Naelewa kuna watu wengi wamehusika kufanikisha hili.

Niwapongeze. Tusonge mbele licha ya changamoto zikizojitokeza na hivyo kuchukua muda kupata ufumbuzi kwa hatua ya sasa.

Jambo la muhimu, mchakato wa token kuingia moja kwa moja bila kulazimika kutumia remote, uharakishwe ili kuondoa chabgamoto kama hizi.
Wasalaam
 
Habari, ndugu mteja. Asante sana kwa mrejesho wako.

Tunafurahi kufahamu kuwa umepata huduma na changamoto yako imetatuliwa. Endapo utahitaji msaada zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana nasi. Tupo tayari kukuhudumia.

Karibu sana na asante. ^CM
 
Back
Top Bottom