TANESCO: Mtambo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme umewasili Nchini ukitokea Marekani

Khaaa Ni Marekani au Veta Chang'ombe ?
 
Nchi hii bado inaendeshwa kama familia ya Kiswahili mara kanunue kiberiti, kanunue chumvi ya kupima, mara rudi kalete pishi moja ya mafuta…
 
kakojoe kwenye mito ili tupate maji ya kusukuma mitambo.
Unaona kabisa ukame hata maji ya matumizi nyumbani mgogoro bado unawaza umeme wa maji!
Twendeni Polepole tutafika tu bila hata ya kukojoa !!
 
Tumenunua, Tumekodisha au tumefanyaje kwa Kiasi gani cha Pesa..., Na uzalizashaji wa hio mitambo utagharimu taifa kiasi gani...., Hii Kampuni inatumika kuwanufaisha watu wachache wakati wengi wanaumia
 
Hizi jitihada za muda mfupi zimetugharimu sana kama Taifa, hasa kupitia hili shirika la Umeme, nitashangaa kama mwisho wa siku haitakuja kuwa kashfa, ni suala la muda tu.
Kama halitakuja kuwa kashifa niite [emoji240]
 
Good
 
- Kwa nini hawasemi kama huo mtambo wa MW 20 kutoka USA wameununua au wamekodisha? Wanasema tu umewasili. Hawasemi wameunua kwa shillingi ngapi au wameukodisha kwa gharama gani na capacity charges zitakuwa billion ngapi kwa siku za kamtambo hako kadogo ka MW 20 tu?

- Ule mtambo wenye uwezo wa kuzalisha MW 80 uliokuwapo pale Nyakato Mwanza kwa nini hauwashwi kipindi hiki cha dharura? Au ulishayeyukia wapi? Kwa nini yale majenereta ya Kigoma waliyazima wakati kuna upungufu wa umeme?

- Hizi mvua zinazonyesha kwa wingi bado tu hazijajaza hayo mabwawa ya Kidatu, Mtera, Pangani na nyumba ya Mungu? Mbona yale ya Dawasa yamejaa na hakuna tena uhaba wa maji katika jiji la Dar es Salaam? Mbona mto Rufiji umejaa na mnategemea kuanza kujaza hilo bwawa la JNHPP wiki ijayo?

- Hiyo haraka haraka ya kwenda kukodisha hako ka mtambo kadogo kutoka USA imetoka wapi? Kabla ya kumaliza kukafunga hapo Kinyerezi mabwawa yote yatakuwa yameshajaa maji kwa mvua zinazoendelea na hali itakuwa imerejea kama mwanzo.
 
Hizi jitihada za muda mfupi zimetugharimu sana kama Taifa, hasa kupitia hili shirika la Umeme, nitashangaa kama mwisho wa siku haitakuja kuwa kashfa, ni suala la muda tu.

Km ulikuwepo kwenye kichwa changu mkuu…Richmond party two inanukia
 
TANESCO ni Taasisi maalum Kwa ajili ya kukamilisha mipango ya wizi wa rasilimali za muda
 
kwanini msitumie huu wa bei rahisi... mbona mnapenda kutumia vitu vya bei kubwa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…