TANESCO mtihani wa umeme mliowaingiza watanzania ni mkubwa sana, ila Mungu anawaona

Wa kuibadilisha TZ ni wewe, usimsubiri Lisu.
Sisi ni waoga sana, elimu hatuna na pia hatupendi kusomesha wanetu.

Utandawazi umetuvaa mapema kabla hatujajipanga vizuri, mambo ni mengi muda mchache.
 
Tulishuhudia Makamba akiondolewa Wizara ya Nishati akiletwa Biteko, tukadhani nia ilikuwa njema kuboresha upatikanaji wa umeme
Biteko kakaa pale km gelesha tu hakuna anachoweza kuwaambia TANESCO wakamsikia TANESCO wanafanya wanavyojisikia wao na hakuna narudia tena hakuna mtu yeyote wa kuwaambia kitu, wanaishia kupewa matamko ya mdomo tu Ila wao ndio waamuzi wanaambiwa Mwezi wa pili wawashe kinu wao wanawasha watapojisikia wanaambiwa Mwezi wa sita fyokofyoko wao watafanya wanavyojisikia hao ndio TANESCO
 
Yes,above the law.Bahati mbaya sana kwa Watanzania.Ndio bwana,hii👇ndiyo TANESCO.
 

Attachments

  • VID-20240203-WA0000.mp4
    4.2 MB
Eti Mungu anawaona! Watanzania bwana. Mungu amekupa akili uzitumie. Hakuna nchi inayoendelea bila wananchi wake kuwawajibisha viongozi wao wanapofanya uzembe. Bila kukiwasha ni bure, utabaki kusema Mungu anawaona Mungu anawaona huku ukizidi kuteseka.
 
Eti Mungu anawaona! Watanzania bwana. Mungu amekupa akili uzitumie. Hakuna nchi inayoendelea bila wananchi wake kuwawajibisha viongozi wao wanapofanya uzembe. Bila kukiwasha ni bure, utabaki kusema Mungu anawaona Mungu anawaona huku ukizidi kuteseka.
Anza wewe basi halafu sisi tutafuata nyuma.Mkono mtupu haulambwi mkuu.

Anyway,hakuna jambo linalomshinda Mungu,he can do literally anything.Sasa kwa vile sisi Watanzania jinsi tulivyo aidha kwa
asili yetu au kwa kuwa tumefanywa kuwa mazombi kwa kutumia mwenge or whatever hatuwezi,tumeamua kumuachia muweza wa yote.
 
Yes,above the law.Bahati mbaya sana kwa Watanzania.Ndio bwana,hii👇ndiyo TANESCO.
Hakuna wa kuwafungulia mashtaka
Hakuna wa kuwapelekesha
Hakuna wa kuwashtua kwamba watu wanaumia
Wanafanya wanavyojisikia wao kufanya
Hakuna narudia tena hakuna mtu yeyote wa kuwaambia kitu TANESCO
Mtu huyo hayupo
Hao mabwana wameshashindikana
Kilichobakia ni kuishi nao kwa uvumilivu wakikata wewe vumilia tu kupigwa na mbu mpaka kukuche wao hawajali kuhusu hilo
Hawajali umelipia Pesa yako au namna gani
Utaambiwa viwanda vimeongezeka ndio maana umeme umekua wa mgao
Hawaishiwi visingizio vya kutungatunga uongo uongo
Utaambiwa maji yamejaa kwenye Bwawa la kuzalishwa umeme yanazuia mitambo isifanye kazi kwa hio ndio maana kuna mgao

Ngoja niishie hapo
 
Anza wewe basi halafu sisi tutafuata nyuma.Mkono mtupu haulambwi.Anyway,hakuna Jambo linalomshinda Mungu,he can do anything.Sasa kwa kuwa sisi Watanzania jinsi tulivyo hatuwezi,tumeamua kumuachia muweza wa yote.
Nilishanza. Maandamano ya Dar nilikuwepo, na Mwanza nitaenda.
 
Nilishanza. Maandamano ya Dar nilikuwepo, na Mwanza nitaenda.
Good luck.Ila naomba nikukumbushe kuwa viongozi waovu Mungu wakati mwingine anawaleta kwa kuwa watu tumekuwa waovu sana,so God is punishing us.The best way therefore
of tackling the problems we have in Tanzania is through changing our ways,not through demonstrations.In that way,God will give us leaders with heavenly wisdom.Taifa letu limemuasi Mungu kabisa,si wananchi wala viongozi,hakuna anayemtafuta Mungu.Ni lazima tutubu na kumgeukia Mungu wa kweli, si miungu hii ya kutembeza barabarani.
 
Huu ni uongo wa mchana kweupe. Mbona kuna nchi zimeendelea sana na zina mambo maovu na hata wanaokwenda kwenye nyumba za ibada ni wachache mno? BTW kama hao viongozi waovu wameletwa na Mungu kwa nini unawaambia tena eti ''Mungu anawaona?''. Si uwaache watunyooshe sasa?
 
Huwezi kunielewa.
 
Huwezi kunielewa.
Siwezi kwa sababu akili zako zimejaa consipiracy theories zisizo na ukweli wowote. Ninyi ni wale mnasoma vitabu vya dini na kuelewa ndivyo sivyo au mnawapa ''manabii'' akili zenu wazishike. Una tofauti gani na Gwajima aliyekuwa anasema ugonjwa wa korona unakwenda kuinuaMagufuli na Tanzania iwe nchi tajiri kuliko zote kwa sababu wamekataa chanjo? Kuwa eti nchi nyingine watageuka ndondocha wote.
 
Umeandika upupu mkuu,mimi siamini Nabii yeyote kati ya hawa unaowajua wewe,kwangu ni waganga wa kienyeji tu.Halafu nikupe nyeupe na kavu,kama umechanja pole,waliochanjwa wanapukutika polepole kwa myocarditis,
cancer nk.nk.
 
We mjinga TANESCO wana kosa gani? hujui watu wa kulaumu?
Hivi ninyi watu mna akili gani?Watanzania wanajua TANESCO ndio waliopewa jukumu la kuwapa umeme,hawaja deliver,Sasa nani alaumiwe?Tuambie wewe basi ambae tutamlalamikia kwa tatizo la umeme tulilo nalo
 
Umeandika upupu mkuu,mimi siamini Nabii yeyote kati ya hawa unaowajua wewe,kwangu ni waganga wa kienyeji tu.Halafu nikupe nyeupe na kavu,kama umechanja pole,waliochanjwa wanapukutika polepole kwa myocarditis,
cancer nk.nk.
Wewe ni hawa watu waliolimbukia kwenye vitabu vya dini. Halafu bado ni mshamba kweli kweli, umejifungia kanisa fulani ukilishwa uongo. Unajua Ulaya na USA walichanja watu wangapi? Ujinga ni mzigo!
 
Eti Mungu anawaona! Watanzania bwana. Mungu amekupa akili uzitumie. Hakuna nchi inayoendelea bila wananchi wake kuwawajibisha viongozi wao wanapofanya uzembe. Bila kukiwasha ni bure, utabaki kusema Mungu anawaona Mungu anawaona huku ukizidi kuteseka.
Hii nchi ni waoga kuliko hata mbwa koko
 
Nimekuwa najiuliza kwa nini serikali imekuwa na kikugumizi cha kuwaambia wananchi chanzo halisi cha tatizo la umeme?Katika hali ya kushangaza, TANESCO nayo ipo kimya,sisi wananchi are left guessing.Bomu limeshushwa,hili hapa chini👇.

Ni hujuma mbaya, mbaya kwa Watanzania ambayo Tanzania haijawahi kuishuhudia tangu uhuru.Kinachoshangaza ni kwa nini wahusika hawachukuliwi hatua,kwa kuwa ni wazi serikali inawajua!Ni nini hasa kinaendelea nyuma ya pazia??????

Hii inatupa picha kwamba serikali inafurahi au ni co-conspirator katika matatizo ya umeme yanayoendelea nchini.Lakini kwa nini serikali ifurahi ikiwa sisi ni wananchi wake????Au maagizo ya NWO kupitia WEF yamesha anza kutekelezwa, maana WEF ilishatoa maelekezo kwamba tunapoelekea kwenye One World Government during the Great Reset,serikali za Dunia zisiwajali kabisa wananchi wao,na mateso during the Great Reset ni lazima na ni sehemu ya the march towards the One World Government.It is so terrifying.
 

Attachments

  • VID-20240211-WA0001.mp4
    10.7 MB
Arusha Tujuane hapa,umeme ni changamoto muda huu sombetini hakuna umeme,Jana wamekata sa saba mchana ukarudi Leo sa Tano kasoro,mda huu Tena umekatika aisee ni kama mateso Kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…