Tanesco mwongozo wa gharama mpya ya kuunganisha huduma ya umeme kuanzia tar 5/1/2022

Tanesco mwongozo wa gharama mpya ya kuunganisha huduma ya umeme kuanzia tar 5/1/2022

Mi nipo DSM na nimelipia jana[04/01/2022] hiyo 27k. Sijui itakuwaje. Ngoja nisubirie
Duuu we noma.
Mie nililipia elf 27 tokq mwezi wa 10 mwaka jana.sijafungiwa Sasa bei imebadirika sijui itakuaje
 
Uzuri wale wale walio sifia kuwa bi mkubwa anaupiga mwingi,wale waliokuwa na mimba za chuki za mwendazake na wale waliokuwa wakilalamika mitandaoni "vyuma vimekaza" nao wanalipa bei hiyo hiyo.

Kuna wale nao waliokuwa wakilalamika "nchi haina uhuru wa kujieleza "
Haya sasa kwa mujibu yao wana uhuru wa kujieleza, ila tozo zime ongezeka kimya, bei ya mafuta imeongezeka kimya,mgao wa umeme na maji kimya, kutokana na impact ya ongozeko la mafuta baadhi ya bidhaa zimepanda bei still kimya na leo hii tena TANESCO wameangusha kombora jingine au inawezekana sasa hivi hawa wanaharakati na baadhi ya wanasiasa waliokuwa wakilalamika enzi ya Mwendazake wanaishi Burundi.

Kuna mpuuzi mmoja alisema "acha legacy ijitete " alizani labda mzimu ndio utakao jutetea. Muda ndio una itetea legacy ya Mwendazake.

Ukizingatia shows ya Tanesco ipo chini ya mzee wa Schedule Maintenance, tuwe wapole tu.
Mwendazake anakusalimia , amenituma kuulizia habari za upendo wake kwa taifa lake.
Majibu yanamiminika yenyewe. Nani anawapenda na yupi anademka.
 
Kuna waya, vikombe, yale machuma ya kushikilia waya, kuna kuchimba mashimo, kuna kuweka stay wire, kuna kuu-treat huo mti ili ufae kutumika, kuna kuusafirisha toka kwa mkulima hati unaposimikwa...

Ni sawa na anayechanga mchango wa harusi halafu anahesabu bia na chakula tu alichokula.. anasahau kiti alichokalia kakichangia, MC, muziki, mapambo, ukumbi, vinywaji, usafiri, zawadi kwa maharusi etc
Wacheni porojo za kutetea ujinga! Serikali inao uwezo wa kushusha bei ya umeme ikitaka!
 
Lazima nchi iendeshwe kwa watu kuchangia kidogo walichonacho 😊
 
Kilichosababisha ni umeme kuwa pungufu, kama bei itakuwa bwerere muuzaji ataelekea kukosa bidhaa ya kupelekea wateja wapya
 
Ufafanuzi wa gharama unahitajika. Hapa ukweli mteja analipa gharama zote za kuungiwa umeme. Mapato yatokanayo na kuuza umeme yanakwenda wapi?
Mapato yanatumika ku run shirika katika issues mfano za maintenances, generation, transmission na distribution. Pia kuna gharama za uendeshaji za kawaida zinajulikana haina haja ya kuzitaja.
Nguzo za umeme kwa wakulima kununua haizidi elf 30 kwa mti mmoja.
Hii laki 530000 kwa nguzo moja inakaaje hii
Pamoja na hilo lakini ujue kuwa Tanesco wao hawauzi nguzo wala vitaa vya umeme. Tanesco ni utility company (shirika linalotoa huduma).

So simply ni kuwa wao huo mchanganuo sio kwaajili ya wewe kununua nguzo au kifaa chochote ni kwaajili ya wewe kupata huduma hiyo.

Hata ukisoma quotation kabla ya kulipia unaambiwa vifaa vyote kuanzia kwenye meter waya mpaka nguzo vinabaki kuwa mali ya shirika na ndio maana hata ikitokea nguzo imeoza au meter imeharibika wa replace wao bila wewe mteja kuingia gharama yoyote.

Hivyo basi muelewe kuwa hamnunui nguzo wala kifaa chochote bali gharama mnazotozwa ni kuchangia ili ufikishiwe huduma ya umeme.
 
EWURA si ndio regulator wa mambo haya kati ya mteja wa tanesco na tanesco wenyewe. EWURA ameridhia kweli bei hizi?
 
Back
Top Bottom